Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo.

Hakuna tija ya kuwa na vifaa vipya kabla ya kujifunza kwanza kuvitumia.

Tuondoane ujinga kwanza ndio twende huko.
😍👏👊
 
Rais Samia kauliza swali zuri sana!

Katiba mpya ndio kila kitu.

Katiba Mpya ni muarobaini wa matatizo mengi likiwemo la kuwa na Uchaguzi halali utakaopatikana tu kama kuna TUME HURU YA UCHAGUZI!! Sasa kwanini SSH na handlers wake wanaiogopa Katiba Mpya hata kama sio kila kitu?

Hizo wanazosema siasa za kistaarabu maana yake siasa ambazo hazitabadilisha mfumo wa kuwanyonya wananchi na kuhakikisha ccm haitoki madarakani!! A true opposition party cannot accept the status quo!!
 
Katiba Mpya ni muarobaini wa matatizo menig likiwemo la kuwa na Uchaguzi halali utakaopatikana tu kama kuna TUME HURU YA UCHAGUZI!! Sasa kwanini SSH na handlers wake wanaiogopa Katiba Mpya hata kama sio kila kitu?
Poleni Watz... Mwenyekiti wa CCM na Rais wa sasa,wakati wa Bunge la Katiba naona labda alijiridhisha kwamba wananchi Tz, hawataki Katiba mpya bali wanachotaka ni maji, chakula nk..... hahahahaaaa...
 
Huyu mama na CCM hawawezi kuiachia hii system ya sasa ambayo ndio inawaweka pale, wanajua siku wakikubali uchaguzi huru kwa katiba au tume ndio utakuwa mwisho wao, dawa ni kuwaburuza tuu kama alivyoburuzwa mkoloni
 
Poleni Watz... Mwenyekiti wa CCM na Rais wa sasa,wakati wa Bunge la Katiba naona labda alijiridhisha kwamba wananchi Tz, hawataki Katiba mpya bali wanachotaka ni maji, chakula nk..... hahahahaaaa...

Kuna handlers wake SSH ndiyo wanamyumbisha kwani wameisha gundua weakness yake!!
 
"Wananchi wangu wana Uelewa mdogo sana wa masuala ya Siasa, Uongozi na Demokrasia hebu naomba Kazi kubwa kabla ya Katiba Mpya ianzie katika Kuwaelimisha"

Mpaka 2025 tutatukanwa mara Milioni.
 
Kaongea Ukweli. Maana Kama Ni Uongo CCM ingekuwa ishatoka Madarakani. Watanzania wengi ni Mbumbumbu kwenye Siasa
 
Kaongea Ukweli. Maana Kama Ni Uongo CCM ingekuwa ishatoka Madarakani. Watanzania wengi ni Mbumbumbu kwenye Siasa
Kwanza wananjaa sana. Hizo akili za kujadili siasa wanazitoa wapi.

Lakini mbona kwenye Makongamano ya Katiba ya Warioba walishiriki kikamilifu?
 
Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo.

Hakuna tija ya kuwa na vifaa vipya kabla ya kujifunza kwanza kuvitumia.

Tuondoane ujinga kwanza ndio twende huko.
Waliotoa maoni ya Katiba ya Warioba walikuwa kutoka Kenya??

Aruhusu tu wiki moja tu tuingie mtaani kwenye makongamano ndio aje ashangazwe na hawa watanzania.

Atabaki mdomo wazi.
 
Rais Samia kauliza swali zuri sana!

Katiba mpya ndio kila kitu.
Hakuna swali zuri hapo, Ni kufail kwa thinking capacity, làbda kwa nyinyi wenye vichwa vya panzi.

Yaliyotokea kwetu 2019 na 2020 hayawezi kutokea Kenya, Ghana and the like countries. Aliyeshinda anatangazwa, ni hicho tu what is to be realised at the end of the day.

Na ili upate hicho lazima kuwe na tume HURU ndani ya Katiba which is derived from all stakeholders ie it catters for all citizens interests
 
Kwani hapa aliyeshinda hatangazwi?
 
nchi zenye tume huru na bado zina migogoro, basi zina migogoro isiyo ya kiuchaguzi na kama wana migogoro ya kiuchaguzi basi tume hizo huru si mazao ya katiba ya wananchi.
Hizo ndizo tume ambazo tunataka kuziunda hapa Tanzania. Huwezi kuunda tume huru ambayo katiba haijaruhusu uhuru wake kuanzia kwenye uundwaji wake, viongozi na watendaji wake, na usimamizi wake nk
 
Naunga mkono hoja
 
Sasa kama tume huru haizuii migogoro, si aiondoe kabisa, kwa nini tunayo?

Tume huru ndizo zinasababisha migogoro?

Hao majirani zetu kweli wana tume huru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…