Rais Anapokuwa Mwongo
Katika hotuba yake alisema kwamba pesa za miamala wananchi wengi walikuwa wanalalamika lakini yeye aliamua kuwapuuza na kupunguza kidogo na itaendelea kuwepo ati kwa sababu tu hata Uingereza (UK) wameanzisha kodi hiyo.
Huu ni uongo uliopitiliza na sijui kwa sababu gani Rais mwenye dhamana anakuwa mwongo hadharani. Je, ni Tony Blair aliyemdanganya? Au anafikiria anaongoza masokwe?
Kwa taarifa yake UK hawahitaji kutumiana pesa kwenye miamala ya simu kwa sababu, mosi kila raia ana account ya Benki, raia wengi wana uwezo wa kutuma pesa kwenye account yoyote ile kwa njia ya mtandao (log in with hand-held devices) and within 2hours the amount of money will be in the recipients account.
Kwanza kujilinganisha na nchi kama UK kwenye tasinia ya technology ni ujinga uliopitiliza. Rais wetu wacha ulimbukeni. Hawa vibaraka uliowaweka ie JM na MC wanakupeleka kubaya.
Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza NGO. Tozo ni wizi kwa sababu fedha hizo zimeshalipiwa kodi. (Double taxation ni dhuluma! Vile vile hakuna sheria iliyofuatwa kuona haki inatendeka kwa wote).
Rais SSH kama kweli anapenda kufuata yanayofanyika UK basi anza kutoa social welfare kwa kila mwananchi ambaye hana kipato.