Rais Samia: Mbaazi sasa siyo mboga ni zao la biashara

Street brain

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2022
Posts
584
Reaction score
767
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya wanaJF,

Mbaazi siyo mboga ni zao la biashara ila kuna muda Mama anajiona kila kitu kashamaliza. Anaona maskini hawezi kufanya chochote ndiyo maana kila kitu akijisikia kuongea anaongea tu.

Anyway, ni Rais wetu na sisi ni wapiga kura, ajaribu kuwa na staha hata kidogo atusitiri japo kidogo tu.

Mbaazi sisi wengine ndizo zimetukuza mpaka hapa tulipo.

Nawasilisha kwenu Jamhuri.

---
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesimama kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Nanguruwe Mkoani Mtwara leo September 16,2023 ambapo amewataka Wakazi wa Mikoa ya Kusini kuondokana na dhana kuwa mbaazi ni mboga pekee na kuliona kwamba ni zao la biashara na kuwataka walime zao hilo kwa wingi kwakuwa soko lake ni la uhakika.

“Mbaazi sasa sio mboga ni zao la biashara kwahiyo wekeni jitihada kwenye kilimo kikubwa cha mbaazi soko lipo tumeshaweka mikataba na Nchi zinazonunua kwahiyo soko la uhakika lipo”

“Kama ilivyopanda bei mwaka huu bei zitaendelea kuwa hivyo kwahiyo kalimeni sana mbaazi, ufuta na korosho, jinsi tunavyoongeza thamani ya zao letu ndivyo bei zitakavyopanda”
 
Hivi huyu mama anatuchukuliaje labda, mimi mbaazi kwangu bonge la mlo na mawazo hakuna.
 
Mbaazi zina bei nzuri sana uhindini na uchina kama ilivyo kwa ufuta Marekani. Tanzania imechelewa sana kwenye kuuza mbaazi nje ya nchi.
 
Wakulima wa MBAZI KITETO hakuna rangi wamewacha kuona safari, keji, kiburi na dharau za wazi kutoka viongozi wa Wilaya, kulazimishwa kupeleka mbazi ghalani kwa Kutumia Nguvu, huku wajanja wachache wakizichua hizo mbazi toka ghalani Kwa mlangi wa nyuma na kuzipeleka Dar es Salaam halafu wanauza Kwa Bei 2400/ halafu mkulima anakuja kulipwa baada ya wiki Tshs 2100-2130 Kwa KG.

Watu wanatumia nafasi zao kuwanyonya wakulima wa. Kiteto, hawatemani Tena Kulima mbazi, wengine wamepewa kesi na mbazi zao kuchukuliwa Kwa Nguvu, na mifano
 
Mbaazi zina bei nzuri sana uhindini na uchina kama ilivyo kwa ufuta marekani. Tanzania imechelewa sana kwenye kuuza mbaazi nje ya nchi.
Wilayani KITETO wamelata Stakabadhi ghalani badala ya kutafuta masoko ya nje ya Nchi, Viongozi Wamepeleka mbaazi za wakulima Kwa madalali Dar es Salaam, hadi hapa wakulima waliochukuliwa mbaazi zao Kwa Nguvu na kupelekwa ghalani wanachanga muda umepita hamna hela, wakiuliza mbaazi wanaambiwa imeenda kuuzwa Dar es Salaam na madalali
 
So sad
 
Daaaaah so sad mkuu yaani apo ni ufisadi mwanzo mwisho
 
---
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesimama kuwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Nanguruwe Mkoani Mtwara leo September 16,2023 ambapo amewataka Wakazi wa Mikoa ya Kusini kuondokana na dhana kuwa mbaazi ni mboga pekee na kuliona kwamba ni zao la biashara na kuwataka walime zao hilo kwa wingi kwakuwa soko lake ni la uhakika.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…