Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

Janga gani na wewe? Yaani huoni haya mabadiliko ya tabia ya nchi? Joto kali sana na maeneo mengine kama Morogoro mvua haijanyesha kabisa, na hii ni November inaenda mwishoni. Yeye afanyeje kama maji yamepungua kutokana na sababu hizo? Kazi tu kukariri corus bila ya kufanya tafakari.
Kwa hiyo ziwa victoria nalo limekauka sababu ya ukame? Au unafikiri wote wanategemea maji ya kutoka kwenye mito?

Maji ya mradi wa ziwa Victoria nayo hayatoki Sasa hivi, hebu tupe sababu
 
Dar es salaam kuna mgao mkubwa wa maji kwa sababu mto Ruvu umevamiwa na binadamu na kuchepusha maji.

Pili maelfu ya mifugo yanayoingizwa kwenye mito kunywa maji yamepunguza kiasi cha maji kwani ng'ombe mmoja kwa mfano hunywa lita 40 za maji kwa siku.
Kwa namna ambavyo wanadamu tunaendesha maisha yetu hivi sasa mabadiliko ya tabia ya nchi hayaepukiki, lakini kwa kutumia akili tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu tunaweza kupunguza athari zake!

Nchi zilizoendelea zinapaswa kutafuta vyanzo vipya vya nishati na kupunguza kabisa matumizi ya nishani zinazoongeza hewa ya ukaa. Nazo nchi zinazoendelea kutengeneza mipango endelevu ya matumizi bora ya maji.

Tanzania kwa mfano tunaweza kupunguza usambazaji mkubwa wa maji ya mito yetu kwa kumwagilia mashamba kwa kutumia mifereji isiyo jengelewa kiasi cha kusababisha maji kupotea kwa njia ya mvuke na kufyonzwa ardhini. Pia tunaweza kuchimba visima vingi vya maji kwa ajili ya kumwagilia mashamba nk.
 
Mnamsingizia Mungu bure. Tanzania kwa Afrika inapitwa na Congo tu kwa kuwa na maji baridi Mengi. Sasa mnataka nini awafanyie?

Kinachoendelea hapa ni mfano halisi wa "In abundance of water the fool is thirsty."

Tatizo siyo Mungu wala ukaidi, tatizo ni uzembe.
 
Kwa hiyo ziwa victoria nalo limekauka sababu ya ukame? Au unafikiri wote wanategemea maji ya kutoka kwenye mito?
Maji ya mradi wa ziwa Victoria nayo hayatoki Sasa hivi, hebu tupe sababu
Aisee wewe jamaa wa ajabu sana. Kwa hiyo ulitegemea Mama Samia awe amefikisha maji ya ziwa victoria Dar na maeneo mengine ndani ya kipindi kifupi alichoshika madaraka? Mbona walaumu bila kuwa na sababu za msingi?

Au ni chuki zako tu kwake? Au hujui pia mabadiliko ya tabia ya nchi yaweza kusababisha hata kina cha maji ya ziwa kupungua sana na kuicha mitambo ya kutape maji ikielea tu?
 
Mnaimiza vijana wajiajiri kupitia kilimo, Kijan akipambana kuchimba mfereji kuchukua maji ya mto kwa ajili ya umwagiliaji wa shamba lake leo hii anaonekana Mbaya.

Hiyo mifereji mnayoiziba maji yasiende kumwagilia mashamba ya watu wamejiajiri kupitia kilimo, mazao yao yatakauka watakosa chakula njaa itawakumba kipato chao kitashuka matokeo yake Ndoa zitavunjika na family.

Wakianza kuuza vitu Kuwa wamachinga vibanda vyao mnavunja na kuwafukuza mjini hawa vijana waende wapi

Rais na watendaji wako mnakula vizuri hiyo mifereji mnao zuia maji wezenu wanategemea kilimo
Mungu anawaona
Miaka yote hiyo mifereji ya maji kwa ajili ya umwangiliaji ilikuwa hakuna
 
Back
Top Bottom