Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

😍
 
Mimi ni ccm ila kwa huyu mama nitakuwa mstari wa mbele kuhakikisha 2025 hatoboi.
CCM inaenda na mama hadi 2030
Aendelee kufungua nchi iliyokuwa kifungoni.

Ikiwezekana aongezwe 10 mingine.
 
Ng'ombe mmoja anakunywa lita 40 kwa siku [emoji1787][emoji1787] ama kweli mama kafungua nchi wallah!!
Kwenye kipindi cha kiangazi ng'ombe anaweza kunywa mpaka lita 80 kwa siku...
 
Jamani watu ni hatari, kwa maana kwa kipindi cha miezi nane ni kama walishauriana kumuangusha Mama na kuvamia mitoni na kupunguza maji. Si hao pia wavugaji sijui waliwahamisha ngombe toka Mwanza na Shinyanga ili kuvamia maji kwa kipindi hiki cha miezi 8.

Na hawa wakataji miti sijui nao walifuatana na wachunga ng`ombe toka Mwanza na Shinyanga na kufanya hujuma kwa miezi hii 8. Du, ni ajabuuuuuuu!!!!!!!!!! Kwa hilo mmefanikiwa kusumbua akili ya Mama, yaani inaitwa MGOMO NA HUJUMA BILA MATANGAZO.
 
Naagiza Wakuu wote wa mikoa kuweka ulinzi katika mito yote ili kulinda maji ya watu wetu……… waagize wakasimamie upandaji wa miti kwenye vyanzo vya maji badala ya kwenda kulinda mito tu.
Utekelezaji wa maagizo ndicho kinacho takiwa kuzingatiwa .
 
Mama tumewahi kuwa na.ukame na.mifugo ilikuwepo, Hakuna hata wakati mmoja wanyama walimaliza maji. Mifugo inategemea mipango ya wanadamu kuhusu uwepo wao,sasa tumefikia hatua ya kuilaumu mifugo? Basi tumekwama kama Taifa. Ni wapi mliutengea maji yao na sasa wanayaacha na kuja kunywa ya wanadamu?

Katika hili sikuuungi mkono. Lakini pia lazima ujue kama wewe ulivyo na hiyi ajira unalipwa mshahara unasomesha wanao ,na mfugaji naye ajira yake ni mifugo ,analisha watu wake,anawasimesha. Anajitibu ,anawabisha kutokana na mifugo. Tangu kuimbwa kwa ulimwengu mifugo ipo.

Ama ukataji wa miti serikali inapaswa kulaumiwa badala ya mwananchi anayekata miti kwa ajili ya mkaa au kuni au ujenzi. Serikali imeshindwa kusambaza gas ya bei nafuu kwa wananchi iliiwe mbadala wa nishati ya kuni. Mmeshindwa kabisa ,badala yake gas ni ghali sana wakati inazalishwa hapa nyumbani.

Vifaa vya ujenzi vingeondokewa kodi ,iwe ni mpango maalumu kwa kipindi cha miaka kumi. Ili watu wamudu gharama za ujenzi hasa vijijini ili kuepuka ukataji wa miti kama vifaa vya ujenzi.
 

Hii ni ishara nzuri kwa kiongozi wa nchi kuwa mstari wa mbele kuliombea taifa. Ni vyema kuwa na maombi ya kitaifa ya kufunga na kuomba ili kuomba Rehema za Mungu dhidi la hili janga la ukosefu wa mvua na majanga mengine yanayotukabili kama taifa.
Mungu Ibariki Tanzania.
Amen
 
Kabla ya kuomba mvua Hangaya tubu dhambi ya kutotambua Mungu aliiponya Tanzania janga la Corona, unalazimisha kwamba Corona ni tishio mpaka Sasa, unalazimisha watu wavae barakoa,watu wachanjwe misumu,ili uwafurahishe wazungu.
Usipotubu Mungu atakufedhehesha kila Kona.
 
Hayo maombi mbona aliyakataa kwenye corona? Akataka sayansi
Kwa nini kwenye maji na umeme hataki sayansi?
 
Hiyo ndiyo tofauti ya Uongozi wa magufuli na wapuumbavuu
Magufuli ni MAJIBU
Ila uongozi tulionao ni MASWALI
 
Moja ya njia ya ku solve tatizo n kukubali tatizo lipo
Huyu ni MJAMBIANI ni kiongozi asiye na majibu yeye ni lile genge la mazuzu walio na maswali tu without answers
 
mkuu hivi unauelewa vizuri kichwani
 
Gesi asilia toka igunduliwe miaka ya sabini haijawahi kuwekwa kwenye mtungi,gesi inayotumika inatoka nje. Labda tuwaulize hao serikali kwanini imeshindikana au tuna ombwe la uongozi?
Kuna mradi wa kumwezesha magari madogo kutumia gesi badala ya petroli lakini mwaka wa kumi na ushee huu kituo Cha kuuzia gesi Ni kimoja TUUH na magari yaliyofungwa hayafiki mia
 
KINACHOENDELEA KTK TAIFA LETU HASA KWENYE ISSUE YA UMEME TUNA ANDALIWA TARATIBU,KIJANJAJANJA KUAMINISHWA UPUUZI KWAMBA MAJI HAYATOSHI,MARA MIUNDOMBINU CHAKAVU.WATANZANIA TUNAPASWA KUELEWA KWAMBA WALE WALIOKUWA WANAFANYA JUHUDI ILI TAIFA KUBWA KAMA HILI LISIJITEGEMEE KWA NISHATI YAKE YA UMEME NDIO WAMEPEWA KITENGO HICHO,TUKUMBUKE MCHWA WAMEVAMIA NYUMBA.TUANDAE MAJENERETA YAKUTOSHA MAANA NDIO LENGO KUU LILILOPO MEZANI.
 
TAIFA linaendelea kupendeza na bidhaa nyingi zinaendelea kushuka bei mfano mbolea bei ilikuwa Tshs 65000/=zamani sasa imeshuka mpaka 130,000/=,Bati tulinunua Tshs 350,000/=,sasa bei imeshuka hadi Tshs 420,000/= na bado watanzania eti wanataka mbolea ishuke hadi Tshs 300,000/=na Bati lishuke hadi Tshs 600,000/= kwa bandro 1 sijui tunataka serikali itutendee nini ndio tuelewe kwa inatupenda kuliko kawaida.
 
inamana kwani hata ziwa viktoria kina cha maji kimepungua kiasi cha wakazi wa maeneo lengwa kukosa maji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…