Rais Samia Mgeni Rasmi Kongamano la Kiswahili Havana Cuba Novemba 7-10, 2024

Rais Samia Mgeni Rasmi Kongamano la Kiswahili Havana Cuba Novemba 7-10, 2024

Ndugu zangu Watanzania,



Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Si kwamba wengi hawapendi tu Maandiko yako marefu bali pia hawapendi Maandiko marefu yenye Pumba tupu na Upumbavu mwingi kama yako Wewe Mwanafunzi wangu uliyekuwa Dhaifu Darasani Kwangu Chuoni Ilala kati ya mwaka 2011 hadi 2012.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, Anatarajiwa kuwa mgeni R

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tumepigwa kingi !!!!!!!!!!
Kwishne!!!!
Mlisema anaenda Marekani - kumbe ilikuwa transit- China-Urusi - Cuba; akitoka hapo North Korea!!!!!!!!

Kwishaaaaaaaaaaa
 
Hakuna wazungumzaji wa kiswahili zaidi ya 150m hapa duniani. Hizi taarifa za kupika kapelekeeni wajinga huko vijijini wasiotambua.
Inawezekana wapo, maana wazungu kutoka Harvard wanasema wapo 200m

1000013781.jpg

 
Mimi sio bendera fuata upepo kama ww. Narudia tenaz kadanganye mafala kuhusu hiyi idadi. Kwa Tanzania waongea kiswahili hawavuki 60m, kenya kama wamejitahidi ni 20-30 tena kwa kuokoteza. Hakuna nchi nyingine yoyote kwenye nchi chache sana zinazosemwa kuzungunza kiswahili, wazungamzaji wa lugha hiyo wanafika ama hata kusogelea 1m.
Ndege inaruka hadi Havana, rais akiambatana na watu mbalimbali, kuna posho, malazi na chakula bado machawa bila shaka wataongozana naye. Yote hayo kwa ajili ya kuzungumza kiswahili ambacho nje ya Afrika ya mashariki hakuna mwenye uhitaji nacho. Kweli Tz yeyote anaweza kuiongoza.
 
Ndege inaruka hadi Havana, rais akiambatana na watu mbalimbali, kuna posho, malazi na chakula bado machawa bila shaka wataongozana naye. Yote hayo kwa ajili ya kuzungumza kiswahili ambacho nje ya Afrika ya mashariki hakuna mwenye uhitaji nacho. Kweli Tz yeyote anaweza kuiongoza.
Anatumia vibaya sn kodi za watanzania yaani ni hovyo kupita kiasi
 
Anatumia vibaya sn kodi za watanzania yaani ni hovyo kupita kiasi
Ziara kama hiyo angeweza kutuma mwakilishi tu hata balozi aliyeko nchi husika. Nchi zilizo serious huwezi kukuta rais anasafiri safiri tu. Matumizi ya rais ni makubwa sana. Hayaendani kabisa na hali ya uchumi wa taifa.

Ziara za ndani tu zinatumia pesa nyingi sana. Watu wanalipa kodi ila matumizi yake ndio kama hayo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, Anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika kongamano la kwanza la kiswahili kimataifa litakalofanyika Havana Nchini Cuba kuanzia Tarehe 7 November hadi 10 November.

Ambapo kongamano hilo litawakutanisha washirika zaidi ya mia 6 yaani 600 kutoka maeneo mbalimbali.lakini pia katika kongamano hilo litahudhuriwa pia na Rais wa Nchi hiyo ya Cuba.

Ikumbukwe ya kuwa kiswahili kimefanikiwa kutambulika au kutambuliwa na UNESCO kuwa Lugha ya saba ya kimataifa,ikiwa na wazungumzaji zaidi ya Millioni 500 Duniani kwote.hivyo hatua hii ni katika muendelezo wa kukipeleka na kukitambulisha kiswahili katika anga la kimataifa.

Siku hiyo na siku hizo za kongamano kutafanyika pia semina mbalimbali pamoja na uzinduzi wa kamusi ya kiswahili na kispaniola iliyoandaliwa na chuo kikuu cha Dar es salaam.

Mimi Mwashambwa Lucas Napongeza sana hatua hii ya Mheshimiwa Rais na juhudi zake za kukipeleka kiswahili kimataifa.lakini Rai yangu ni kuomba sisi kama Taifa kuwa mstari wa mbele katika kukitumia katika maeneo mbalimbali ya kiutawala na maamuzi.

Mfano bado haijafahamika vizuri kwanini mpaka leo unakuta kesi mahakamani inasikilizwa kwa kiswahili halafu hukumu na mwendo mzima wa kesi unatolewa kwa lugha ya kiingereza.jambo ambalo linawanyima haki watu wasio na uelewa na lugha hiyo ya kiingereza hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa hata tu waliosoma na kufika vyuo vikuu unakuta umahiri katika lugha hii ya kigeni ni tia maji tia maji tu.

maana wengi wamekariri na walikariri kwa ajili ya kujibia mitihani ya darasani tu.ambapo unakuta mtu amemaliza chuo kikuu lakini hawezi kuongea hata kwa dakika mbili kiingereza kilichonyooka kama rula bila kusoma mahali popote pale.

Sasa kwanini tuendelee kuwatesa watanzania na kuwapa kazi ya kutafuta wakalimani wa lugha ya kiingereza kuwafafanulia kilichoandikwa na jaji.kwanini hukumu na mwenendo mzima wa kesi usiandikwe kwa kiswahili tu ieleweke.

Pili huwa nashangaa unakuta viongozi wetu wengine yupo kwenye hadhira ya huko vijijini lakini unakuta anachanganya na kutoa ufafanuzi kwa kuchanganya kiswahili na maneno ya kiingereza.sasa lengo Sijuwi huwa ni nini.maana jambo hilo huwaacha wananchi hewani kwa kushindwa kuelewa baadhi ya hoja.

Pia sisi kama Taifa tunatakiwa ndio viongozi wetu wawe mstari wa mbele katika kutumia lugha hii ya kiswahili katika hotuba zao hususani kunapokuwa na wageni wameingia Nchini mwetu.cha kufanya ni kutafuta wakalimani wa kufanya kazi hiyo ya kufasili. Ofisi zote za umma na matangazo yao nayo pia yawe yanatolewa kwa kiswahili.

Tuache kukitukuza sana kiingereza.maana imefika wakati inaonekana mtu anayezungumza kiingereza ana akili sana na msomi sana kuliko yule anayezungumza kiswahili.ndio maana ukizungumza kwa kiingereza jambo hata la kijinga utaonekana una akili nyingi na utaona watu wakikushangilia na kukusifia sana kwa kuwa tu umeongea kiingereza.

Naomba niishie hapa kwanza maana najuwa wengi hawapendi maandiko marefu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Anza na bunge kwanza
 
Ziara kama hiyo angeweza kutuma mwakilishi tu hata balozi aliyeko nchi husika. Nchi zilizo serious huwezi kukuta rais anasafiri safiri tu. Matumizi ya rais ni makubwa sana. Hayaendani kabisa na hali ya uchumi wa taifa.

Ziara za ndani tu zinatumia pesa nyingi sana. Watu wanalipa kodi ila matumizi yake ndio kama hayo.
Rais ambaye mshahara wake haukatwi kodi ni hatari sn hana uchungu wowote na fedha za umma
 
Huku kunawaka moto

#HABARI: Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutoka Chanika, Buguruni, Tandika na Ukonga, wamevamia ofisi za CCM, Mkoa wa Dar es Salaam kwa madai ya kutaka uchaguzi urudiwe baada ya kutokea fujo na wizi wa kura katika uchaguzi wa ndani uliofanyika hivi karibuni.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow RadioOneStereo
 
Back
Top Bottom