Rais Samia Mgeni Rasmi Sherehe ya Miaka 50 ya Uhuru wa Umoja wa Visiwa vya Comoro Julai 6, 2025

Rais Samia Mgeni Rasmi Sherehe ya Miaka 50 ya Uhuru wa Umoja wa Visiwa vya Comoro Julai 6, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais Samia Mgeni Rasmi Sherehe ya Miaka 50 ya Uhuru wa Umoja wa Visiwa vya Comoro Julai 6, 2025


Sehemu ya Hotuba ya Rais Samia
Rais Samia amependekeza Comoro wafundishe lugha ya kiswahili nchini mwao na Tanzania ipo tayari kuwasaidia kwa kuwapa vifaa na walimu.

Amesema Tanzania iko tayari kusaidia kwa kutoa walimu na vifaa vya kufundishia. Aidha, amesisitiza kuwa Kiswahili ni urithi wa pamoja na daraja la maendeleo baina ya mataifa ya Afrika.

"Ili kujenga umoja nitumie fursa hii kupendekeza kwamba kiswahili lugha ya mawasiliano, elimu na biashara kati yetu ifundishwe mashuleni na kutambulika rasmi hapa Comoro. Tanzania ipo tayari kusaidia kutoa walimu na vifaa vya kufundishia. Tukumbuke kwamba Kiswahili ni urithi wetu wa pamoja na ni daraja la maendeleao baina yetu." Rais Samia


Rais Samia amewahimiza wananchi wa Comoro walio ndani na nje ya nchi hiyo kuilinda na kuijenga nchi yao.

"Kumbukeni kwamba nchi hujengwa na wananchi wake wito wangu kwa Wanacomoro walio ndani na nje ya nchi yani Diaspora kuendelea kuishi kwa upendo kuaminiana na kuheshimiana. Comoro itajengwa na Wanacomoro na si watu wengine wowote, ni wenyewe Wanacomoro watakaoleta utulivu wa kisiasa ndani ya visiwa hivi. Ni wanacomoro wenyewe ndiyo watakaoweza kujenga uchumi ndani ya visiwa hivi." Rais Samia
 
Halafu za Uhuru wa Tanganyika, kila mwaka anaahirisha! Mapinduzi ya Zenj, kila mwaka yapo palepale!! Ok.
 
Back
Top Bottom