Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Kama ukifika Znz anacho kisema na uhalisia haviendeni kabisa. Yani Mwalim Nyerere aliwahi kusema hakuna nchi inaitwa Znz nakama wanabisha wajitenge. Ndipo watagunduwa kuna waunguja na wapemba na hawa hawafanani na hata ukienda utaliona hilo... Well ni haki kuzungumza. Mdomo mali yake.
 
..Maza anatuhumiwa kupendelea Waznz.

..katikati ya manung'uniko hayo Maza anasema yeye ni Mzanzibari!!

..Na Mznz kutokuwa na kabila haimaanisha kwamba hawezi kuonea kabila fulani.

Mkuu JokaKuu ,upo sahihi kabisa.
Tuhuma za Mh. Rais Samia ni kuhusu kupendelea Wazanzibar na Zanzibar kama eneo.
Kwa yeye kusema kwamba ni Mzanzibar hiyo inamaanisha wanaopiga kelele za upendeleo kwa Zanzibar na Wazanzibari wana hoja.
Kutokuwepo kwa makabila Zanzibar au kutojiita yeye ni Mkojani/Mpemba/Mshiraz/Mtumbatu/Mcomoro hakuondoi hoja ya "upendeleo kwa Wazanzibar".
Upendeleo wa aina yoyote ile ni sawa na "ukabila" na "udini".
Ukipendelea wanawake zaidi ya wanaume kisa tu unataka kulevel au haki sawa kijinsia, huo ni upendeleo sawa na udini na ukabila.
Uwezeshaji ukiwa na lengo na kuinua kundi moja katika jamii zaidi ya kundi/makundi mengine,huo ni upendeleo.
 
Mzanzibari ni utaifa wako, hivyo inaonyesha ulivyo,wewe siyo Rais wa wazanzibari bali Rais wa watanzania. Ilikuwa sahihi Rais ukasema ni Mtanzania. Hapo utakuwa unaendeleza uzanzibari na utangamanyika. Rais wangu siku nyingine rekebisha
 
Ukweli ni kwamba!Dr.Hussein Mwinyi na Mama ni mtu na Dada yake!!Baba mmoja!!!MZEE MWINYI ALIKULA PISI KALI SANA!!UNAONA HILO JICHO UNAFIKIRI MAMA YAKE MAMA ATAKUAJE???
 
Hiii mitandao hii! Mimi namuomba Mama atumie tu ile huwa ninaiita JK style "NI UPEPO, UTAPITA', basi!
 
Mtamsema sana mh.Rais ila ndio mjue yeye ndiye RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI......

ENDELEENI kuufukuza upepo......


#NchiKwanza
#KaziInaendelea kwa Kasi &Weledi zaidi
Kwani kuna mtu anakataa ?
 
Naona mama ana jaribu kuwajibu sana watu wa mitandao, mi nadhani ange wapotezea hawafiki hata 10% ya watanzania
Kama watumia simu janja wako zaidi ya 30M, unawezaje kusema watumia mitandao ni 10% tu ya watanzania...?

Na hebu tuashumu kweli ni 10%. Je, unajua nguvu (influence) ya watumia mitandao...?

Ukitaka kujua kuwa social media ina nguvu, fanya kituko hapo ulipo kwa kutembea uchi. Nakuhakikishia in just a minute, dunia zima [siyo Tanzania tu] itakuwa imeshajua...!!

Don't underestimate the power of social media hata kama ni 10% [japo takwimu yako hii ni uongo] ya population ya 60M ndiyo watumia simu na computer zenye access to internet...!!
 
Sasa uta jibu kila kitu, maana wanao comment hujui hata wako kwenye hali gani. Kwa mfano hiyo ya sukuma gang huku kitaa hakuna hata mtu ana time nayo sasa viki pata airtime kwa raisi vina weza leta madhara
 
Nilitegemea jibu hili, na ninakubaliana nawe; lakini hiyo haiondoi msingi wa hoja kuu. Yeye anajitambulisha kuwa mtu wa nchi nyingine! Why?
 
Nilitegemea jibu hili, na ninakubaliana nawe; lakini hiyo haiondoi msingi wa hoja kuu. Yeye anajitambulisha kuwa mtu wa nchi nyingine! Why?

Lakini mkuu,,bila ya kujitambulisha c inajulikana yeye ni mzanzibari!! Haya yote hayasaidii muhimu aliongoze taifa kwenye mctari, ndicho 2nachotaka.
 
Hata uzanzibari ni ukabila
 
Lakini mkuu,,bila ya kujitambulisha c inajulikana yeye ni mzanzibari!! Haya yote hayasaidii muhimu aliongoze taifa kwenye mctari, ndicho 2nachotaka.
Mkuu 'Dalmine', huyu mama anapoteza fursa muhimu sana anazopewa kujipambanua yeye kuwa kiongozi ambaye nchi hii ingemtambua na kumkumbuka katika historia yake.

Kwani kweli maswala kama hilo la kujitambulisha, yeye akisisitiza na kueleza kinagaubaga kwamba yeye ni mTanzania mwanzo na mwisho, atakuwa amepoteza kitu gani hapo?
Huko kujipambanua kwamba yeye ni mZanzibari kunamwongezea sifa zipi za kuwa kiongozi anayetaka mafanikio, mshikamano wa taifa analoliongoza!
Kwa hiyo, yeye na mtangulizi wake Magufuli tofauti yao ni ipi hasa katika kuhimiza umoja wa nchi yetu na kuachana na usukuma wa Magufuli?

Hataweza "kuliongoza taifa kwenye mstari" kama atakuwa kila mara anaangalia uZanzibar wake.
 
Naona mama ana jaribu kuwajibu sana watu wa mitandao, mi nadhani ange wapotezea hawafiki hata 10% ya watanzania
Inaweza kuwa asilimia ndogo lakini yenye ushawishi mkubwa,ndio maana serikali inalazimika kuzima mitandao,katika kipindi cha uchaguzi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…