Rais Samia: Miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli ni urithi wetu

Rais Samia: Miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli ni urithi wetu

Kijogoodi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,362
Reaction score
2,373
Rais Samia amehawakikishia watanzania kuwa miradi yote aliyoacha Hayati Rais Magufuli lazima itekelezwe na kumalizwa kwa sababu ni urithi wa watanzania na tukiitelekeza tutaambulia laana kutoka kwa Mungu na kutoka kwa aliyeanzisha hiyo miradi.

Rais Samia - Rais Dkt. John Magufuli ametuachia urithi, ametuachia miradi mikubwa miwili, na mwingine wa mkakati ipo, ule ni urithi, na wanasema ukifanya mchezo kwenye urithi Mungu anakulaani au yule aliyekuachia urithi hana radhi na wewe na Mungu hatukuwa na wewe

Bwawa la Nyerere, SGR ,Uwanja wa Msalato, daraja la Kigongo Busisi lazima ikamilike.

---
 
Hasa la umeme ni nchi nzima aisee, soda zitauzwa150, wazee wa ulabu utashukavpia🏌🏌🏌
 
Duh
FB_IMG_1617728213402.jpg
 
Najaribu kutafakari jinsi ambavyo marehemu alivyojisifu kwa kujenga miundombinu mingi, hata ile aliyoikuta ipo mwishoni kukamilika yeye akamalizia asilimia 5% wapambe waliimba na kusifu kwamba kajenga yeye.

Sasa kuna miradi na yeye kaacha haijakamilika mingine ndo kwaanza ipo asilimia 0% kama daraja la busisi.

Ikikamilika tusifu na kuimba mapambio kwa mwendazake km kawa au?
 
Unauliza swali au jibu! MAMA!! Mbona na aliyetangulia alijichukulia ujiko kwenye ile Flyover ya Tazara na lile daraja la Mto. Kilombero?
 
Back
Top Bottom