Maneno makali sana haya!, maadam rais hupangwa na Mungu, kwani wewe ni Mungu?, au Mungu amekuambia amempangia nani?.
Nakubaliana na wewe
Why?
Tunasubiri kushangaa, usije kushangaa wewe!.
Nakubaliana na wewe
Why?
P
Mimi si Mungu, ila Mungu uongea kupitia wanadamu. Wanadamu wasipomsikiliza unyanyua hata jiwe. Kumbuka Mungu alimtumia punda kuongea.
Why? Jibu ni kwamba Makamba hana tunuku ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mimi sintoshangaa kwani naujua ukweli kuwa Rais atakuwa mwingine na si Makamba.
Niseme tu Makamba si mpakwa mafuta kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata atumie nguvu gani. Hato weza katu.
Mwaka 2007. Kuna baadhi ya watu niliwambia, Rais ajae baada ya Kikwete atakuwa Magufuli. 2010 Nikawakumbushia. Wengi walinicheka sana na kuniona sifai. Wengi walitabiri Edward Lowasa. Kwakua alikubalika na alikuwa mwana mikakati.
Nilisema Lowasa hawezi kuwa Rais wa hii nchi hata siku moja. Hajatunukiwa hilo. Ubishi wa wengi waliona kilichotokea.
Mungu akisema hapana au ndiyo hutumia njia nyingi kudhihirisha nguvu yake. Mungu uruhusu hata machafuko na mifarakano ili kutimiza agano lake au kusudi la kimungu.
Mnara wa Baberi ulianguka baada ya Mungu kuwachanganya watu wasisikilizane. Kwa sababu Mungu hakutaka huo mnara ujengwe.
Pascal Mayalla; Ni moja ya vichwa navyo vikubali na kuheshimu sana humu JF. Napenda uandishi wako na fikra zako. Ila tu niseme katika hii dunia uwa tunahitaji jicho la tatu kuona mbali. Sina chuki na Makamba. Lakini kila nikitazama simuoni. Makamba hayumo katika mpakwa mafuta.
Kuna matukio hutokea watu wakadhani ni binadamu ndo kafanya. Maandiko yanasema Mungu akafanya moyo wa Farao kuwa mgumu akawakatalia wana wa Israel wasiondoke. Wakati huyo huyo Mungu ndo anamtuma Musa awaondoe wana wa Israel lakini bado anafanya moyo wa Farao kuwa mgumu asiwaruhusu waisrael.
Mungu hutenda kwa njia tofauti. Kifo cha Magufuli nilianza kukiona miaka mitatu nyuma. Sikupenda lkn nikaoneshwa utawala wa mwanamke.
Kuna mambo mengi yanaonwa kwa jocho la tatu, lakini ni ngumu hata kuandika humu, JF si ile ya zamani, imekuwa sehemu ya upendeleo, kusifia na kutukana. Mada nzuri hufutwa haraka sana. Inafanya watu tusiandike mengi.
Jiulize kuna mtu alie kuwa na nguvu kama Lowasa hata kumtetemesha Rais wa nchi. Kwanini hakuwa Rais?
Kuna mzee Malecela huyu alijiandaa kila kitu alijua atakuwa Rais. Lakini wapi?
Nimejikita kiroho saana. Mambo mengi hapa duniani yanaenda kiroho. Japo wengi wetu tunapenda kuishi katika mwili na kuenenda katika mwili. Iwapo tutaruhusu jicho la tatu la kiroho ndipo tutakapo kuwa na utambuzi wa nini kinaendelea katika maisha yetu.