Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza umemtupia zigo la lawama? Elewa tu watu wanaamini ana baraka zako

Rais Samia napenda kukushauri, kwa sababu katiba ndo ilikupa hiyo nafasi na wala hukuwa potential candidate kwenye nafasi ya urais hata kama magufuli angemaliza muda wake, ni bora ungejikita kuweka misingi ya kiuongozi ambayo inaleta maelewano na kupunguza vurugu na chuki miongoni mwa jamii. Misingi hiyo ni pamoja na katiba mpya inayoridhiwa na makundi yote ya wananchi ambayo italeta tume huru ya uchaguzi isiyopendelea upande wowote. Usijaribu kukumbatia mifumo ambayo inakupa nguvu za kutawala kimabavu ili uendelee kukumbatia madaraka maana inaweza ku back-fire ikakuondolea credibility yako uliyoanza kuijenga kama kiongozi unayejali na kusikiliza changamoto za makundi yote ya watu katika jamii na utaishia kuingia kwenye kundi la watawala wakandamizaji jambo ambalo siyo zuri ukizingatia pia na jinsia yako....
 
Acha ujinga muda wanini tangu Uhuru tunamiaka mingapi kama Taifa na hatusogei Kisha unaleta blah blah za muda
 
Hawakusoma alama za nyakati
 
Usikute rais hata hajui Kama mwenyekiti wenu yuko ndan yy yuko busy na eid
 
Chadema ni kama mtoto wa mwisho yani anadeka deka tuuu kutwa kulia lia tuuuu dah alafu mwanaume ndo wanalia zaidi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mbowe anatangaza kuwa kuna Corona then yeye mwenyewe ndo anataka kukusanya watu
Kwa hiyo corona inabagua?kusanyiko likiwa LA ccm hakuna corona....TUMIA AKILI,ACHA KUTUMIA MAKALIO
 
Ni makosa makubwa kuzuia mifumo rasimi ya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba. Mambo ya Mwendazake amani na kuaminiana kwa Watanzania kulipungua Sana.
 
Vuguvugu hili lipo kwenye mitandao ya simu ambao hao ni makada. Ukija mtaani raia hawana habari na hili mnalolipigania kwenye mitandao na Chama kama Chama.

Unadhani tatizo ni nini?
Binafsi huwa najiuliza Chadema wana lengo gani hasa na Harakati zao hizi za Siasa. Huwa nawaza mambo mawili, Aidha wanafanya siasa zao kwa lengo la kuwaridhisha watu fulani ambao wanawafadhili ili waendelee kuwapa fedha au Hawajui watanzania ni watu wa namna gani inapokuja suala la Siasa.

Unapojiita chama ambacho ni cha kuwasemea watanzania, na unaitisha Maandamano au uko kwenye kuonewa na dola na unaitisha Maandamano lakini watu hao hawajitokezi, lazima ujiulize mara mbili, nini shida? Je, ninachokipigania ndicho wanachokihitaji? Je, njia ninayoitumia ndio wanayoitaka? Je, wako tayari kujitolea kiasi gani? Mimi nina aamini Chadema ni chama kikubwa kioganaizesheni, hivyo kinafanya tathmini na tafiti na kujua nini hasa watu wanataka.

Ukisoma mitandaoni juu ya katiba, unaona mjadala huu unazungumziwa zaidi Twitter, ukichunguza mitandao ya Instagram au Facebook ni nadra kukuta mjadala huu. Je, watanzania wanagapi wanatumia Twitter? Hao wanaotweet kuhusu Katiba ni watu wa kundi lipi? Je, ukifanya reflection huku mtaani Katiba inazungumziwa? Pita kwenye vijiwe, pita sokoni, nenda kwenye mabaa, zungukia kwenye makusanyiko ya harusi au misiba, je kuna mjadala wa katiba? Kama upo inajadiliwa katiba kama hitaji au kama tukio la mvutano wa kisiasa? Ukitathmini yote unaona kuna disconnect kubwa kati ya kinachodaiwa na Chadema na wananchi wenyewe huku mtaani.


Mwaka jana Lissu alizuiwa Kiluvya, jana yake alikuwa na kusunyiko kubwa la watu, lakini hawakujitokeza kupingana na Polisi, Mikutano yote Lissu alikuwa na 'mafuriko' ya watu, lakini alipoitisha Maandamano ya amani Nov 2, 2020 hata wanachama wa chama chake hawakujitokeza. Haya ndio mambo yanaleta maswali juu ya approach ya Chadema kwenye siasa za Tanzania.
 
Sawa kabisa mkuu.
 
Vuguvugu hili lipo kwenye mitandao ya simu ambao hao ni makada. Ukija mtaani raia hawana habari na hili mnalolipigania kwenye mitandao na Chama kama Chama.

Unadhani tatizo ni nini?
Kama mtaani raia hawana habari, sasa hao police wa nini?
Si wangewaacha CDM wakutane, waongee then warudi makwao.
Maana wanainchi hawana habari.

Sasa Police na Serikali wana hofu gani na kongamano la Katiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vuguvugu hili lipo kwenye mitandao ya simu ambao hao ni makada. Ukija mtaani raia hawana habari na hili mnalolipigania kwenye mitandao na Chama kama Chama.

Unadhani tatizo ni nini?
Hivi kwako tafsiri ya "raia mitaani" ni ipi? Hao wanaoingia kwenye hizo kumbi hawatoki mitaani wanatoka wapi Mkuu?
 
Kama mtaani raia hawana habari, sasa hao police wa nini?
Si wangewaacha CDM wakutane, waongee then warudi makwao.
Maana wanainchi hawana habari.

Sasa Police na Serikali wana hofu gani na kongamano la Katiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali haifanyi kwa kuigopa Chadema ukiliangalia hili suala kwa mapana yake. Serikali inafanya kutokana na kauli ya CHADEMA, nayo Serikali imeamua iwatunishie msuli.
 
Jeshi la Polisi lilimkamata Lowassa wakati fulanl. Lowassa alikamatwa na Polisi au na Makonda?
Inawezekana hapa Mbowe ametekwa alipokywa mikononi mwa Polisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…