Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 829
- 1,564
Nimekutana na Clip ya Mheshimiwa Rais ikielekeza watanzania kutii na kuacha miradi ya serikali ipite kwenye maeneo yao na ikishakamilika ndo wadai fidia.
Nimejaribu kujiuliza hivi Rais amewaza nini kutoa agizo lile? Mradi umepita kwenye eneo langu, nyumbani kwangu nyumba inavunjwa mimi niondoke na familia bila fidia nikaishi wapi?
Kisa ni mradi kwa faida ya wananchi, nadhani pengine ingekuwa kwa faida yangu na familia yangu hapo ingekuwa sawa ningesema ngoja nivumilie nikisubiri (ROI0)
Lakini kwa faida ya watnzania alafu baadhi ya familia ndo zinaumia hii hapana hebu serikali iwe na huruma kidogo. Mtu pengine ni mstaafu nyumba inavunjwa na unatakiwa upishe mradi uishe, DUH
Pia soma > Wakili Madeleka: Huwezi kumvunjia mtu nyumba yake bila kumlipa fidia eti asubiri utamlipa baadae
---
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoidai Serikali fidia baada ya kupitiwa na miradi, wasubiri miradi hiyo ikamilike kwanza, kisha utaratibu utafanyika kuhakikisha wanalipwa.
Kinachosababisha uamuzi huo, amesema ni umuhimu wa miradi hiyo kwa wananchi, hivyo Serikali inaona ianze kuitekeleza kwanza kwa manufaa ya wengi, ndipo ichakate utaratibu wa fidia.
Mkuu huyo wa nchi ameibua hoja hiyo baada ya malalamiko ya wananchi wa wilaya mbalimbali mkoani Morogoro kudai malipo ya fidia baada ya kupitiwa na mradi wa umeme wa Kihansi.
Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 alipohutubia wananchi wa Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
“Wale wanaotudai fidia zao kwa maendeleo yao wenyewe tunaomba muwe na subira. Tuacheni tumalize miradi ya maendeleo, wananchi wengi wafaidike halafu tutaangalia masuala ya fidia,” amesema.
Katika maelezo yake, amegusia uwepo wa baadhi ya watu wanaoweka vikwazo vya utekelezwaji wa miradi husika kwa sababu hawajalipwa fidia.
“Tuacheni tufanye miradi, mambo ya fidia mimi nawahakikishieni hatonyimwa mtu haki yake. Tukiwa tayari tutalipa fidia, kwa hiyo niwaombe sana wananchi achieni miradi ijengwe kwa manufaa yenu, fidia itakuja kulipwa,” amesema.
Chanzo: Mwananchi
-----