Pre GE2025 Rais Samia: Mnaotudai fidia kuweni na subira tumalize miradi ya maendeleo kwanza ndipo tuwalipe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimekutana na Clip ya Mheshimiwa Rais ikielekeza watanzania kutii na kuacha miradi ya serikali ipite kwenye maeneo yao na ikishakamilika ndo wadai fidia.

Nimejaribu kujiuliza hivi Rais amewaza nini kutoa agizo lile? Mradi umepita kwenye eneo langu, nyumbani kwangu nyumba inavunjwa mimi niondoke na familia bila fidia nikaishi wapi?

Kisa ni mradi kwa faida ya wananchi, nadhani pengine ingekuwa kwa faida yangu na familia yangu hapo ingekuwa sawa ningesema ngoja nivumilie nikisubiri (ROI0)

Lakini kwa faida ya watnzania alafu baadhi ya familia ndo zinaumia hii hapana hebu serikali iwe na huruma kidogo. Mtu pengine ni mstaafu nyumba inavunjwa na unatakiwa upishe mradi uishe, DUH

Pia soma > Wakili Madeleka: Huwezi kumvunjia mtu nyumba yake bila kumlipa fidia eti asubiri utamlipa baadae

---

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoidai Serikali fidia baada ya kupitiwa na miradi, wasubiri miradi hiyo ikamilike kwanza, kisha utaratibu utafanyika kuhakikisha wanalipwa.

Kinachosababisha uamuzi huo, amesema ni umuhimu wa miradi hiyo kwa wananchi, hivyo Serikali inaona ianze kuitekeleza kwanza kwa manufaa ya wengi, ndipo ichakate utaratibu wa fidia.

Mkuu huyo wa nchi ameibua hoja hiyo baada ya malalamiko ya wananchi wa wilaya mbalimbali mkoani Morogoro kudai malipo ya fidia baada ya kupitiwa na mradi wa umeme wa Kihansi.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 alipohutubia wananchi wa Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
“Wale wanaotudai fidia zao kwa maendeleo yao wenyewe tunaomba muwe na subira. Tuacheni tumalize miradi ya maendeleo, wananchi wengi wafaidike halafu tutaangalia masuala ya fidia,” amesema.

Katika maelezo yake, amegusia uwepo wa baadhi ya watu wanaoweka vikwazo vya utekelezwaji wa miradi husika kwa sababu hawajalipwa fidia.

“Tuacheni tufanye miradi, mambo ya fidia mimi nawahakikishieni hatonyimwa mtu haki yake. Tukiwa tayari tutalipa fidia, kwa hiyo niwaombe sana wananchi achieni miradi ijengwe kwa manufaa yenu, fidia itakuja kulipwa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

-----
Yaani nina nyumba moja, kwa mfano, halafu inavunjwa na baada ya mradi ndio nilipwe fidia ili nikajenge nyumba nyingine sehemu nyingine. Je, baada ya kuvunjwa nyumba hiyo nitaishi wapi? Sheria inasema ikipita miezi sita baada ya valuation, fidia hailipwi mpaka valuation nyingine ifanyike. Ni kwamba, fidia inalipwa ndani ya miezi sita baada ya valuation.
 
Huo udundulizaji uende sambamba na kudunduliza fidia kwa watakaoathirika kwenye kila hatua.......kwa hiyo kama mradi unachukua miaka kumi, huyu mnyonge aendelee kuteseka kusubiri fidia kwa miaka kumi?
 
Yaani nina nyumba moja, kwa mfano, halafu inavunjwa na baada ya mradi ndio nilipwe fidia ili nikajenge nyumba nyingine seheme nyingine. Je, baada ya kuvunjwa nyumba hiyo nitaishi wapi? Sheria inasema ikipita miezi sita baada ya valuation, fidia hailipwi mpaka valuation nyingine ifanyike. Ni kwamba, fidia inalipwa ndani ya miezi sita baada ya valuation.
No, baada ya miezi sita kupita, haitakiwi kufanyika Valuation nyingine upya, Bali Taarifa ya Uthamini iliyopo itauhishwa kwa kuwekewa viwango vipya vya Fidia vyenye riba (Compound Interest) kwa kuzingatia viwango vya riba vilivyopo kwenye Benki za kibiashara zilizopo hapa nchini. Yaani inachukuliwa kama vile Fidia yako unayopaswa kulipwa ni kama Amana yako uliyoweka katika akaunti ya Benki.
Uhai au Ukomo wa Ripoti ya Uthamini kwa mujibu wa Sheria ya Uthamini ni miaka miwili (2), baada ya hapo ripoti hiyo inaisha muda wake (expires) na hapo ndipo zoezi la Uthamini wa Mali linapaswa kufanyika upya.
 
Walivyopiga marufuku Mikutano ya vyama vya siasa mlikuwa mnacheka mnaona ni sawa.sasa mmeguswa kwenye maslahi yenu,mnawaka! Siasa ni ajira na maisha ya watu.
Usilazimishe nifikirie kile unachofikiria wewe, lakini jitahidi kutoishi kwa mazoea na kufuata trending, jaribu kuwa mtu unayejipa muda kutafakari kabla ya kucomment na kushare.
 
Nimekutana na Clip ya Mheshimiwa Rais ikielekeza watanzania kutii na kuacha miradi ya serikali ipite kwenye maeneo yao na ikishakamilika ndo wadai fidia.

Nimejaribu kujiuliza hivi Rais amewaza nini kutoa agizo lile? Mradi umepita kwenye eneo langu, nyumbani kwangu nyumba inavunjwa mimi niondoke na familia bila fidia nikaishi wapi?

Kisa ni mradi kwa faida ya wananchi, nadhani pengine ingekuwa kwa faida yangu na familia yangu hapo ingekuwa sawa ningesema ngoja nivumilie nikisubiri (ROI0)

Lakini kwa faida ya watnzania alafu baadhi ya familia ndo zinaumia hii hapana hebu serikali iwe na huruma kidogo. Mtu pengine ni mstaafu nyumba inavunjwa na unatakiwa upishe mradi uishe, DUH

Pia soma > Wakili Madeleka: Huwezi kumvunjia mtu nyumba yake bila kumlipa fidia eti asubiri utamlipa baadae

---

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoidai Serikali fidia baada ya kupitiwa na miradi, wasubiri miradi hiyo ikamilike kwanza, kisha utaratibu utafanyika kuhakikisha wanalipwa.

Kinachosababisha uamuzi huo, amesema ni umuhimu wa miradi hiyo kwa wananchi, hivyo Serikali inaona ianze kuitekeleza kwanza kwa manufaa ya wengi, ndipo ichakate utaratibu wa fidia.

Mkuu huyo wa nchi ameibua hoja hiyo baada ya malalamiko ya wananchi wa wilaya mbalimbali mkoani Morogoro kudai malipo ya fidia baada ya kupitiwa na mradi wa umeme wa Kihansi.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 alipohutubia wananchi wa Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
“Wale wanaotudai fidia zao kwa maendeleo yao wenyewe tunaomba muwe na subira. Tuacheni tumalize miradi ya maendeleo, wananchi wengi wafaidike halafu tutaangalia masuala ya fidia,” amesema.

Katika maelezo yake, amegusia uwepo wa baadhi ya watu wanaoweka vikwazo vya utekelezwaji wa miradi husika kwa sababu hawajalipwa fidia.

“Tuacheni tufanye miradi, mambo ya fidia mimi nawahakikishieni hatonyimwa mtu haki yake. Tukiwa tayari tutalipa fidia, kwa hiyo niwaombe sana wananchi achieni miradi ijengwe kwa manufaa yenu, fidia itakuja kulipwa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

-----
Alafu jamiiforums kuweni wastaarabu basi mmebadilisha bandiko langu kuanzia kichwa cha habari na mtiririko mzima japo maudhui yamebaki yale yale. Alafu mnasema source Mwananchi nyie mnajuaje Source yangu ya habari ni mwananchi? Hao mwananchi mimi sijaona hata kama nao wameripoti hii taarifa
 
Wananchi wakiambiwa katiba mpya inayotamka kila raia atakuwa mmiliki wa ardhi yake kikatiba bila kuingiliwa na rais kwa kisingizio cha kuwa rais ni msimamizi wa ardhi yote kwa niaba yao, watakataa watasema CHADEMA ina uroho wa madaraka.

Huu ni mfano bora wa haja ya katiba mpya ambayo itagusa maeneo mengi kupunguza madaraka ya raia mfalme kama katiba ya 1977 ilivyomrundikia mambo kibao rais.

Chagua CHADEMA, chagua Katiba Mpya kwa maendeleo yako raia na demokrasia kwa ujumla 2024 / 2025.
 
Inashangaza sana hii, Hivi Rais wa nchi si anaapa kuilinda Katiba na watu wake?
Inakuwaje sasa huyu mtu awe mtetezi wa Serikali tena kwenye suala la ardhi ambapo mwananchi ndio mmiliki wa ardhi?.
Serikali kwa kuwa haina ardhi inalazimika kumlipa fidia kamilifu mmiliki bila kusubirishwa pale inapotaka kutwaa ardhi kwa maendeleo!! 😲🤯😮🤯
 
Tayari huu utaratibu unatumika kwenye utwaani wa maeneo kul
e ujenzi wa SGR Isaka-Mwanza

Likipitiwa eneo lisilo na nyumba unakopwa tingatinga linapita,kupata majaaliwa.

Makaburi yaliyohamishwa June 2022 walikopwa na sijui kama wamelipwa maana mradi wenyewe umesimama.

Wanaambiwa Rais anaweza kuamua tu kubadili matumizi ya hiyo ardhi yako na ukakosa hata fidia

Haya ndiyo mambo TLS wangefanyia kazi
 
Yaani nina nyumba moja, kwa mfano, halafu inavunjwa na baada ya mradi ndio nilipwe fidia ili nikajenge nyumba nyingine sehemu nyingine. Je, baada ya kuvunjwa nyumba hiyo nitaishi wapi? Sheria inasema ikipita miezi sita baada ya valuation, fidia hailipwi mpaka valuation nyingine ifanyike. Ni kwamba, fidia inalipwa ndani ya miezi sita baada ya valuation.
Hata kama ungekuwa nazo 50 chief, Bado unapaswa kulipwa fidia kwanza.
 
Back
Top Bottom