Rais wa JMT amekataa ombi la kuipandisha hadhi Manispaa ya Morogoro Kuwa Jiji kama ambavyo mamlaka zimekuwa zikiomba akisema Morogoro Bado sana kufikia hadhi hiyo na kuwataka watimize wajibu wao.
---
Your browser is not able to display this video.
Mbunge wa viti maalum Christine Ishengoma amewasilisha ombi la kutaka Halmashauri ya mji wa Morogoro ibadilishwe na kuwa jiji kama ilivyo kwa majiji mengine ya Dar es salaam na Arusha hata hivyo Rais amesema kuwa maombi yote yamepokelewa na yatafanyiwa kazi isipokuwa hili la Morogoro kuwa jiji ambapo amewaambia wana Morogoro wafanye kazi kwanza kuipa Morogoro hadhi kisha serikali itatenda wajibu wake.
"Kwa vipimo tulivyoviweka suala la Morogoro kuwa jiji bado kwahiyo kazi iko kwenu. Kuna kazi ya kufanya waziri wa Tamisemi atatoa ufafanuzi nini cha kufanya ili Morogoro iweze kuwa jiji lakini kwa sasa bado kwahiyo timizeni wajibu wenu na serikali tuje tutimize wajibu wetu". Alisema Rais Samia
Mwanahalisi
My Take
Naunga mkono hoja:Hakuna kulipa Hadhi ya Jiji Manispaa Yeyote ambayo ina Mapato ya ndani Chini ya Bilioni 15.
Sifa ya Jiji wanatakiwa wajitosheleze Kwa mapato ya Ndani walau 40% ya Bajeti Yao.
Nchi ina watu wa hovyo sana! Dr Ishengoma na usomi wake anaamini Morogoro ni jiji kweli? Huyu mama amewahi kuwa RC pwani na mhadhiri wa chuo!! Hizi ndo akili Africa tunazitumia kuamua kwa niaba yetu!!! Hovyo sana!

Tangu Rais Dr. John Pombe Magufuli kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es Salaam, kumekuwa na mijadala kemkem kuhusu jambo hilo runingani, redioni na hata mitandaoni. Mjadala hasa unajikita katika kuelewa...
Rais wa JMT amekataa ombi la kuipandisha hadhi Manispaa ya Morogoro Kuwa Jiji kama ambavyo mamlaka zimekuwa zikiomba akisema Morogoro Bado sana kufikia hadhi hiyo na kuwataka watimize wajibu wao.