Rais Samia: Morogoro Kuwa Jiji bado

Rais Samia: Morogoro Kuwa Jiji bado

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Rais wa JMT amekataa ombi la kuipandisha hadhi Manispaa ya Morogoro Kuwa Jiji kama ambavyo mamlaka zimekuwa zikiomba akisema Morogoro Bado sana kufikia hadhi hiyo na kuwataka watimize wajibu wao.
---

Mbunge wa viti maalum Christine Ishengoma amewasilisha ombi la kutaka Halmashauri ya mji wa Morogoro ibadilishwe na kuwa jiji kama ilivyo kwa majiji mengine ya Dar es salaam na Arusha hata hivyo Rais amesema kuwa maombi yote yamepokelewa na yatafanyiwa kazi isipokuwa hili la Morogoro kuwa jiji ambapo amewaambia wana Morogoro wafanye kazi kwanza kuipa Morogoro hadhi kisha serikali itatenda wajibu wake.

"Kwa vipimo tulivyoviweka suala la Morogoro kuwa jiji bado kwahiyo kazi iko kwenu. Kuna kazi ya kufanya waziri wa Tamisemi atatoa ufafanuzi nini cha kufanya ili Morogoro iweze kuwa jiji lakini kwa sasa bado kwahiyo timizeni wajibu wenu na serikali tuje tutimize wajibu wetu". Alisema Rais Samia

Mwanahalisi

My Take
Naunga mkono hoja:Hakuna kulipa Hadhi ya Jiji Manispaa Yeyote ambayo ina Mapato ya ndani Chini ya Bilioni 15.

Sifa ya Jiji wanatakiwa wajitosheleze Kwa mapato ya Ndani walau 40% ya Bajeti Yao.

Pia soma RC Malima: Kama Morogoro mnataka kuwa Jiji acheni uchafu na ongezeni makusanyo ya Nndani
 
Nchi ina watu wa hovyo sana! Dr Ishengoma na usomi wake anaamini Morogoro ni jiji kweli? Huyu mama amewahi kuwa RC pwani na mhadhiri wa chuo!! Hizi ndo akili Africa tunazitumia kuamua kwa niaba yetu!!! Hovyo sana!
 
Sio swala la Imani ni swala la vigezo.Mambo ya Imani ndio maana mnapigwa za uso na wajasiliadini.
 
Moro watulie kwanza wakue na wapunguzi punguze ule mkoa n mkubwa sana
 
Rais wa JMT amekataa ombi la kuipandisha hadhi Manispaa ya Morogoro Kuwa Jiji kama ambavyo mamlaka zimekuwa zikiomba akisema Morogoro Bado sana kufikia hadhi hiyo na kuwataka watimize wajibu wao.
Mbeya na Tanga ni vigezo Gani vilitumika vikawa JIJI?
 
Bongo bwana, kila mkoa unataka kua jiji, ni vituko.

Kiukweli haya ya kwetu sio majini, ni vijiji vilivyochangamka.

Kwa hiyo Morogoro iwe jiji kama Capetown ama New York, ama London? Tuwe tunaita New York City, Morogoro City?

Morogoro iwe jiji kama Paris?

Tuna masihara sana. Hadhi ya neno jiji tunaidhalilisha sana.
 
Back
Top Bottom