Rais Samia: Morogoro Kuwa Jiji bado

Rais Samia: Morogoro Kuwa Jiji bado

Kuwa na heshima kwa Iringa
Iringa ni Kijiji tena kimepauka hakina hata mzunguko wa hela wa maana,watu wachache nk.

Mkitaka Iringa Ichangamke kiuchumi hakikisheni yafuatayo;

1.Ongezeni Ukubwa wa Mji Kwa kuchukua maeneo ya Wilaya Jirani,

2.Hamasisheni jamii zinazozaliana sana kama Wasukuma wahamie,

3.Barabara ya kwenda Moro imetoboka kwa lami

4..Barabara ya Kwenda Ruaha NP Ina lami na

5.Mwisho Barabara Mpya ya kuunganisha na Mpanda kama inavyoonekana kwenye hii ramani hapa chini 👇👇
Screenshot_20240709-061801.jpg
 
Kahama hama mji pale? Mji umejaa mashimo ya vyoo kila kona hata sawage system hakuna halafu unataka uwe jiji? Kweli?
Naunga mkono hoja.Wanaotaka Kahama iwe Jiji ukiwaukiza kwa kipi hasa hakuna anaekuja na jawabu 😆😆
 
Rais wa JMT amekataa ombi la kuipandisha hadhi Manispaa ya Morogoro Kuwa Jiji kama ambavyo mamlaka zimekuwa zikiomba akisema Morogoro Bado sana kufikia hadhi hiyo na kuwataka watimize wajibu wao.
---

Mbunge wa viti maalum Christine Ishengoma amewasilisha ombi la kutaka Halmashauri ya mji wa Morogoro ibadilishwe na kuwa jiji kama ilivyo kwa majiji mengine ya Dar es salaam na Arusha hata hivyo Rais amesema kuwa maombi yote yamepokelewa na yatafanyiwa kazi isipokuwa hili la Morogoro kuwa jiji ambapo amewaambia wana Morogoro wafanye kazi kwanza kuipa Morogoro hadhi kisha serikali itatenda wajibu wake.

"Kwa vipimo tulivyoviweka suala la Morogoro kuwa jiji bado kwahiyo kazi iko kwenu. Kuna kazi ya kufanya waziri wa Tamisemi atatoa ufafanuzi nini cha kufanya ili Morogoro iweze kuwa jiji lakini kwa sasa bado kwahiyo timizeni wajibu wenu na serikali tuje tutimize wajibu wetu". Alisema Rais Samia

Mwanahalisi

My Take
Naunga mkono hoja:Hakuna kulipa Hadhi ya Jiji Manispaa Yeyote ambayo ina Mapato ya ndani Chini ya Bilioni 15.

Sifa ya Jiji wanatakiwa wajitosheleze Kwa mapato ya Ndani walau 40% ya Bajeti Yao.

Pia soma RC Malima: Kama Morogoro mnataka kuwa Jiji acheni uchafu na ongezeni makusanyo ya Nndani
Bongo bwana, kila mkoa unataka kua jiji, ni vituko.

Kiukweli haya ya kwetu sio majini, ni vijiji vilivyochangamka.

Kwa hiyo Morogoro iwe jiji kama Capetown ama New York, ama London? Tuwe tunaita New York City, Morogoro City?

Morogoro iwe jiji kama Paris?

Tuna masihara sana. Hadhi ya neno jiji tunaidhalilisha sana.
Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya kuainisha mji kuwa jiji, nchini Tanzania hakuna hata mji mmoja ambao umekidhi vigezo hivyo vya kuweza kuitwa jiji. Hakuna kabisa.
 
Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya kuainisha mji kuwa jiji, nchini Tanzania hakuna hata mji mmoja ambao umekidhi vigezo hivyo vya kuweza kuitwa jiji. Hakuna kabisa.
Acha uongo,kwamba hata Dar sio Jiji? By the way Kila Nchi Ina vigezo vyake Kwa sababu zake.
 
Acha uongo,kwamba hata Dar sio Jiji? By the way Kila Nchi Ina vigezo vyake Kwa sababu zake.
Ndiyo, hata Dsm pia haijakidhi vigezo vya kimataifa vya kuweza kuwa Jiji.
Yaani haijakidhi kabisa.

Kwa Mfano, Ukichukua kigezo kimoja tu Cha kupangilika kwa mji, pamoja na kupangilika kwa miundombinu yake ya Makazi, usafiri na usafirishaji, n.k, tayari mji huo unakuwa ume-disqualify kwa takribani asilimia 90 ya kuweza kuwa Jiji, achilia mbali na vigezo vingine vingi ambavyo sijavigusia hapa.
 
Sasa hivyo sio vigezo vya msingi saana
 
Back
Top Bottom