Rais Samia mpige chini Humphrey Polepole, ni jipu!

Rais Samia mpige chini Humphrey Polepole, ni jipu!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
20220131_134235.jpg
Wakati sisi wana CCM tulielewa vyema maana ya Rsis kuwaasa mawaziri wake kutoingiliana kimamlaka na utendaji alipoongea na baraza lake la mawaziri, kwa uwazi, wengine wameamua kumwekea Mama Samia maneno mdomoni, kwa maana hasi na isiyostahili utumishi wa umma.

Polepole, mbunge wa kuteuliwa na Rais Samia amekuwa akimnanga Mama Samia kila apatapo nafasi hiyo, na kumpinga Mama waziwazi.

Mimi mmoja wa tulioukubali, kuupokea na kuunga mkono utawala wa Awamu ya Sita, naona huyu Polepole ni msaliti, apigwe chini.

Polepole, kama Ndugai wana mipango ambayo haiko wazi.

Wakae nje ya uongozi ili mambo yao wakayasuke vizuri.
 
Huyu chawa hana madhara ubunge wa kupewa
 
View attachment 2102588
Wakati sisi wana CCM tulielewa vyema maana ya Rsis kuwaasa mawaziri wake kutoingiliana kimamlaka na utendaji alipoongea na baraza lake la mawaziri, kwa uwazi, wengine wameamua kumwekea Mama Samia maneno mdomoni, kwa maana hasi na isiyostahili utumishi wa umma...
Ingawa naelewa kwa dhati kabisa Polepole ni mnafiki aliyetukuka lakini hii haki yake ya kutoa maoni haiwezi kupokwa kwa namna yeyote kwani ni haki ya kikatiba na ndivyo CCM ilivyowajenga vijana wake kuwa na fikra tunduizi pasina kusahau kuhoji hojaji zenye hoja.

Au nasema uongo ndugu yangu johnthebaptist ?
 
Kwahio yoyote mwenye kauli mbadala apigwe chini?

Sio kwamba nasema polepole ana hoja za nguvu lakini sio vema kuzima hoja kwa kutumia nguvu.

Na wewe kama mwananchi unaona sawa kabisa mtu apigwe chini sababu ya mawazo yake (kesho ukipigwa wewe chini sababu kama hio je?); Unaona tunaweza kujenga nchi kwa kupigana chini? Huoni kwamba njia sahihi ni kuonyesha uduni wa hilo lisemwalo na sio kuzibana midomo?
 
View attachment 2102588
Wakati sisi wana CCM tulielewa vyema maana ya Rsis kuwaasa mawaziri wake kutoingiliana kimamlaka na utendaji alipoongea na baraza lake la mawaziri, kwa uwazi, wengine wameamua kumwekea Mama Samia maneno mdomoni, kwa maana hasi na isiyostahili utumishi wa umma...
Polepole ni mbunge wa kuteuliwa ila hajateuliwa na Samia
 
Amesema mawaziri wajitokeze kukemea kauli ya raisi, kwamba kauli yake ina utata, sasa waziri gani anaweza kukemea kauli ya raisi?
 
Polepole endeleza kukoleza kuni mbichi kwenye tanuru - bado wanaibuka !!
 
Back
Top Bottom