Hawa trafiki kazi yao imebaki kuokota za kubrashia viatu, maeneo ya barabara ya mlimani city wanavizia asubuhi asubuhi magari kwenye taa za kwenye zebra.....afisa unaamka alfajiri kwenda kuvizia magari yanayowahi makazini (rush hours) kwa kukamata magari kwenye zebra kwa kisingizio cha taa nyekundu wakati hakuna watu wanaovuka, nafikiri tukubaliane kwamba kubambika makosa na kudai rushwa ndo utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi wa hili jeshi la polisi.....naunga mkono huyo ateuliwe kama ana commitment ya kuondoa hii aibu ya rushwa kwa matrafiki wanaojazana huko mabarabarani.