Huyu dada alizaliwa kutumikia wananchi!Huyu ni kati ya watumishi walio katika ngazi za juu kiuongozi wanaoitendea haki sekta ya afya nchini kikamilifu.Hapa namzungumzia Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza,Sekou Toure.Huyu dada ndani ya muda mfupi kaifanya Sekou Toure iwe hospitali pendwa kanda ya ziwa ikigeuka kimbilio la wagonjwa wengi na kuipiku hospitali kubwa na kongwe yenye facilities nyingi zaidi ya ya Bugando katika utoaji wa huduma za kiafya Kwa wagonjwa!
Tatizo la Watanzania tuna kasumba ya kusubiri mtu aharibu au akosee ndipo tumshambulie au kumdhalilisha! Akifanya vizuri tunakuwa vipofu!Wakitokea wachache kupongeza mazuri yanayofanywa na mhusika linakuwa tatizo jingine! Siyo fair!Yaani hata sasa kuna watu wanatamani kuona Rais Samia Suluhu Hassan kila siku anaongelewa kwa mabaya hapo ndipo wanakuwa na relief moyoni.Ikitokea Rais kapongezwa Kwa mema aliyoyafanya kwao inageuka kuwa kero!
Bado naamini huyu dada anastahili kabisa kubeba mikoba kamili ya uwaziri wa afya au ukatibu mkuu kule wizara ya afya.Maono yake yatasaidia kulinufaisha Taifa badala ya kunufaisha eneo dogo tu la Mwanza na viunga vyake.Umri wake mdogo, haiba yake,nidhamu yake kazini,juhudi na vitaongeza ufanisi katika sekta ya afya.Tuliwahi kushauri kuhusu Dr.Faustine Ndugulile kupewa nyadhifa za juu Kwa maslahi ya Taifa watu wakabeza,Leo ni mkurugenzi Shirika la afya la Umoja wa Mataifa(WHO) kanda ya Afrika.Mifano ipo mingi!
I stand to be corrected🙏