Rais Samia mtupie jicho la tatu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa Mwanza Sekou Toure Dkt. Bahati Msacky

Rais Samia mtupie jicho la tatu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa Mwanza Sekou Toure Dkt. Bahati Msacky

Anaeloga na ashindwe, akitupa bomu lirudi kwake mara mbili, muacheni huyo dada wa watu. Jitume na wewe usifiwe, acheni wivu!!
 
View attachment 3085672

Kwanini anachat muda wa kazi?
Alisikika mpinzani wake akisema
1725354698617.png
 
Ana mume huyo dokta?
Kama anafanya kazi vizuri na kwa bidii ndio lengo kuu la yeye kuajiriwa na sio kuwa kiongozi mkubwa wa afya.
Tuachie muda uamue.
 
Huyu dada alizaliwa kutumikia wananchi!Huyu ni kati ya watumishi walio katika ngazi za juu kiuongozi wanaoitendea haki sekta ya afya nchini kikamilifu. Hapa namzungumzia Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza, Sekou Toure.

Huyu dada ndani ya muda mfupi kaifanya Sekou Toure iwe hospitali pendwa kanda ya ziwa ikigeuka kimbilio la wagonjwa wengi na kuipiku hospitali kubwa na kongwe yenye facilities nyingi zaidi ya ya Bugando katika utoaji wa huduma za kiafya Kwa wagonjwa!

Tatizo la Watanzania tuna kasumba ya kusubiri mtu aharibu au akosee ndipo tumshambulie au kumdhalilisha! Akifanya vizuri tunakuwa vipofu! Wakitokea wachache kupongeza mazuri yanayofanywa na mhusika linakuwa tatizo jingine! Siyo fair. Yaani hata sasa kuna watu wanatamani kuona Rais Samia Suluhu Hassan kila siku anaongelewa kwa mabaya hapo ndipo wanakuwa na relief moyoni.Ikitokea Rais kapongezwa Kwa mema aliyoyafanya kwao inageuka kuwa kero!

Bado naamini huyu dada anastahili kabisa kubeba mikoba kamili ya uwaziri wa afya au ukatibu mkuu kule wizara ya afya. Maono yake yatasaidia kulinufaisha Taifa badala ya kunufaisha eneo dogo tu la Mwanza na viunga vyake.Umri wake mdogo, haiba yake,nidhamu yake kazini, juhudi na vitaongeza ufanisi katika sekta ya afya.Tuliwahi kushauri kuhusu Dr.Faustine Ndugulile kupewa nyadhifa za juu Kwa maslahi ya Taifa watu wakabeza.

Leo ni mkurugenzi Shirika la afya la Umoja wa Mataifa(WHO) kanda ya Afrika.Mifano ipo mingi!

I stand to be corrected🙏

FB_IMG_1725447682052.jpg
 
Huyu dada yuko poa sana kuna siku nilikuwa na ukaguzi nilifurahia sana ushirikiano wake ni transparent,inteligent,pia ni loyal sana, big up anastahili elevetion
 
Kwanza utueleze wewe ulikuwa mgonjwa hapo Sekeou Toure au wewe ni mtumishi mwenza na huyo Dr Msaky. Tuanzie hapo
 
Huyu dada alizaliwa kutumikia wananchi!Huyu ni kati ya watumishi walio katika ngazi za juu kiuongozi wanaoitendea haki sekta ya afya nchini kikamilifu.Hapa namzungumzia Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza,Sekou Toure.Huyu dada ndani ya muda mfupi kaifanya Sekou Toure iwe hospitali pendwa kanda ya ziwa ikigeuka kimbilio la wagonjwa wengi na kuipiku hospitali kubwa na kongwe yenye facilities nyingi zaidi ya ya Bugando katika utoaji wa huduma za kiafya Kwa wagonjwa!
Tatizo la Watanzania tuna kasumba ya kusubiri mtu aharibu au akosee ndipo tumshambulie au kumdhalilisha! Akifanya vizuri tunakuwa vipofu!Wakitokea wachache kupongeza mazuri yanayofanywa na mhusika linakuwa tatizo jingine! Siyo fair!Yaani hata sasa kuna watu wanatamani kuona Rais Samia Suluhu Hassan kila siku anaongelewa kwa mabaya hapo ndipo wanakuwa na relief moyoni.Ikitokea Rais kapongezwa Kwa mema aliyoyafanya kwao inageuka kuwa kero!
Bado naamini huyu dada anastahili kabisa kubeba mikoba kamili ya uwaziri wa afya au ukatibu mkuu kule wizara ya afya.Maono yake yatasaidia kulinufaisha Taifa badala ya kunufaisha eneo dogo tu la Mwanza na viunga vyake.Umri wake mdogo, haiba yake,nidhamu yake kazini,juhudi na vitaongeza ufanisi katika sekta ya afya.Tuliwahi kushauri kuhusu Dr.Faustine Ndugulile kupewa nyadhifa za juu Kwa maslahi ya Taifa watu wakabeza,Leo ni mkurugenzi Shirika la afya la Umoja wa Mataifa(WHO) kanda ya Afrika.Mifano ipo mingi!
I stand to be corrected🙏
Story nyingi ,hoja hamna ,sema ni kipi amefanya ambacho ni tofauti ili tumpongeze , badala ya kusema nini amefanya upo mara awe katibu mkuu, mara waziri .

Unasema seketure inaeleke ipiku BMC kwa flow ya wangonjwa , elewa BMC ni Zonal hospital, so na gharama za matibabu lazima zichangamke kama ambavyo ,huduma za matibabu zimechangamka , kwa kigezo ichi tu kwanza lazima flow ya wagonjwa Seketure referal hospital iwe juu .

Aya leta sifa nyingine sasa ili uyo mfawidhi tumsifu
 
Jumatatu tarehe 02 Sept, 2024 ulileta uzi wa kumwaga sifa kama huu, leo tarehe 04 Sept 2024 just 2 days after umeleta tena uzi wenye same theme. My friend miluzi mingi hupoteza Mbwa. Nenda taratibu utamuharibia huyo Dada!
 
Back
Top Bottom