Rais Samia muulize Bilionea Alhaj Aliko Dangote alitaka umpe nini ambacho hajapewa?

Simfahamu

Ila nimefata hoja sio mtoa hoja
Hakuna mchumia tumbo mwenye hoja , Magufuli alimwalika Dangote , akamwalika Rostam hadi mdogo wake jangili wa meno ya tembo akafutiwa kesi ya ujangili , na ccm ikahongwa Channel 10 , uliona Huyu njaa kali Maghembe akiandika huu utopolo wake ? unadhani ni kwanini ?
 
dangote ameenda siku moja unadai kila siku?
check your facts kwanza
 
Barua ya mualiko ulitoa wewe?
Acha kujifanya unajua kumbe pangu pakavu,sisi ndo wafanya biashara tunaelewa haya,wewe mkusanya documents ofisini subiri mshahara mwisho wa mwezi
Nyinyi ni wafanya biashara, au wanyang'anyi wa mali za waTanzania?

Kama wewe ni mfanya biashara huwezi kuogopa kufanya mambo yako kwenye uwazi na taratibu zinazofahamika.

Haya, tueleze wewe 'mnyang'anyi' unayejipambanua kuwa mfanya biashara, hiyo mialiko mnayopewa kwenda huko, inatofauti gani na taratibu za kibishara mnayoitumia sasa, maanake sisi hatuijui, au ni siri yenu nyinyi pekee na huyo anayewapa hiyo mialiko?

Tukilisemea hilo unatoana ni wajinga na kutuona "wakusanya 'documents' ofisini"?
 
Mkuu hebu weka wazi jinsi awamu ya tano ilivyo kiuka makubaliano baini ya serikali na Dangote.tunaome uyaweke wazi tuache hisia...
Swala la kuletewa gas kiwandani kwake lilifanywa awamu gani na nani aliagiza?
swala la kupewa mgodi wa kuchimba coal lilifanywa awamu gani? nani aliaGIZA?
Alipo kuwa anaingiza magari yake nakumbuka serikali iliingilia kati nakuamuru yatolewe pale bandarini mtwara haraka... hivi hii ilikuwa awamu gani?
Hebu twambieni Magufuli alimnyima nini Dangote ambacho Mama anataka kumpatia?
Ni serikali ipi imekuwa ikitatua kila leo migogoro ya wafanyakazi wake pale kiwandani?
Nakumbuka hadi wawekezaji wa ndani walianza kulalamika kuwa Dangote anapendelewa sana ...
Naomba useme hapa serikali ya awamu ya tano ilimfanyia nini kibaya Dangote?
 
Hoja ya msingi mnakimbia matusi,Kwa nn hao Twiga,Tanga,mbeya,camel cement n.k walowekeza miaka hawaendi endi Ikulu kulialia,anaenda Dangote ambaye hata nchini mwao wanamtilia shaka biashara zake za kubebwa
Na hapa nataka waweke wazi ni kitu gani kibaya Dangote kafanyiwa na awamu ya tano?
 
Na hayo uliyoomba yakishasemwa hapa, tunaomba pia ni yapi aliyoahidiwa hivi juzi hadi akafurahi na kusifu sana, na kuahidi kuvuta wawekezaji zaidi waje kuwekeza.

Haya ndiyo tunayotaka kuyafahamu, yasiwe mambo ya kufanyia gizani tu, huku tukisifu vitu tusivyovijuwa!
 
Ex prezida wa Nigeria ni big shareholder ndio maana kila mgogoro ukiibuka Obasanjo huja Tz .
"Ikulu kuna nini , ikulu ni eeo takatifu." Nyerere voice
 
Watanzania wezi sana...fanya biashara halafu muweke mtanzania wiki tu utaanza kulia

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ampe nini mengine ni faragha zao
 
Kwani Kiwanda cha saruji cha Dangote kilianza uzalishaji rasmi lini hapa nchini?

Mwanzo huwa ni mgumu mara nyingi.

Si sawa kulinganisha kiwanda cha saruji Twiga ambacho kina zaidi ya miaka 50 ya uzalishaji n.k

Mwanzoni kunakuwa na gharama nyingi za uzalishaji ambazo ni fixed bila kujali umezalisha au la unlike kina twiga wenyewe wapo kwenye longrun production ambapo in most cases costs zao ni variable.

Kwa hiyo sishangai kama wamekuwa wakipata hasara mfululizo, ni kawaida kabisa sometimes.

Cha maana ni kuwepo na independent auditors wa kuhakiki hizo hasara kama ni genuine au la.

Mimi naona kwenda kwake Ikulu hakuna neno na uwepo wa kiwanda chake una manufaa ila kama mkataba unakasoro upitiwe urekebishwe.
 
Unafikiri ujenzi wa nyumba unaitaji cement peke yake?
 
Umesahau waliimpa eneo la bahari iwe bandari yake kwa kijiji cha MSIJUTE
 
Huu ushuzi .....
 
Pamoja na kuwa tajiri zaidi mweusi ulimwenguni Dangote ana tabia ya kukwepa kulipa kodi na kuwatumia viongozi wengiwa nchi za Kiafrika kwa njia anazojua yeye za asilimia 10, kuna wakati aliwahi kukimbilia nje kutokana na tuhuma za milungura na ukwepaji kodi huko kwao. Dangote si tu ni mjanja kwenye mambo ya biashara bali yeye anachojua ni kushindatu kwa kila dili analolifanya, kifupi Dangote sio mwekezaji mzuri bali ni dhulumati mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…