KERO Rais Samia na CDF tusaidieni Watumishi Wastaafu wa Umma wa Wizara ya Ulinzi tupate stahiki zetu, tupo tayari kuonana nanyi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaandika ujumbe huu tukiwa na huzuni ya kiwango cha hali ya juu kutokana na yake tunayopitia, sisi ni wastaafu tuliokuwa Watumishi wa Umma ndani ya Wizara ya Ulinzi, tumefanya kazi kwa vipindi tofauti, baadhi ikiwa ni miaka 35 hadi 40 na kuendelea.

Wengi wetu tulikuwa ‘Nursing Assistants’ kwenye vikosi mbalimbali vya Jeshi, tuliajiriwa na kila mmoja alipewa barua ya kuajiriwa pia kila Mwajiriwa alikuwa na C/NO yake ya kupatia Mshahara kutoka Hazina (Pay Slip tunazo).

Tukiwa katika ajira tulikuwa tunapandishwa vyeo na pia tukapewa barua za kuthibitishwa kazini lakini baada ya sisi kustaafu wengi wetu hatukulipwa stahiki zetu kama inavyotakiwa, fikiria unafanya kazi Miaka 10 kisha unapewa Tsh. Milioni 5 hadi 10? Kweli hii ni sawa?

MADAI YETU YA MSINGI
  • Hela za likizo tulilipwa kidogo
  • Malipo ya NSSF / PSSF (wengi wetu tulipewa chini ya milioni 5)

Tunaomba ujumbe huu umfikie Rais wa Nchi, Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda, japokuwa mambo ya Jeshi kama haya huwa hayawekwi Mtandaoni lakini tumeona hii ndio njia pekee ya kuwasilisha ujumbe wetu kwenu.

WANAOHUSIKA WANATUGAWA
Taarifa tulizozisikia ni kuwa Rais Samia amepitisha malipo yetu akielekeza wote tunaodai tulipwe, baadhi ya Wahusika wanaosimamia wanatugawa kwa kuamua kutuambia baadhi yetu hawakuwa na barua za kuthibitishwa kazini na kundi lingine wanazo barua.

Wale walioambiwa wao wana barua za kuthibitishwa kazini wameambiwa wasubiri japokuwa muda unazidi kwenda hawajaambiwa chochote, wale wa upande wa pili wanaoambiwa hawana barua za uthibitisho kazini (licha ya kuwa walikuwa wakipandishwa vyeo kazini) ni kama wanaelekeza kuzimwa moja kwa moja.

KELELE ZA AWALI ZILISAIDIA
Tunaishukuru JamiiForums.com kwa kuwa awali wanaohusika hawakuwa na mpango nasi hata kidogo lakini baada ya kuweka andiko hapa, ujumbe ukafika na inadaiwa Rais Samia akaagiza tulipwe, kabla ya kuanza kuzungushwa na watu wa kati.

INADAIWA KUNA MTU AU WATU WANAKWAMISHA
Taarifa tulizozipata kwa kuwa nasi tuna vijana wetu tuliowaacha kwenye kazi, inadaiwa kuna watu au mtu ana maslahi binafsi, ndio maana anakwamisha akiamini wengi wetu ni wazee, hivyo hatuna uwezo wa kuendelea kudai haki yetu.

KELELE ZETU ZIMESAIDIA WALIPO KWENYE AJIRA
Inadaiwa kelele zetu na hiki kinachoendelea kimesababisha Watumishi waliopo kazini kwa sasa kuanza kusaidiwa, kupewa nyaraka za ajira mapema na maelekezo mengine ambayo sisi hatukuyapata.

Hoja zinazoendana, soma
~ Waziri Tax: Hakuna malimbikizo kwa wastaafu wanaohusiana na JWTZ
~ Vilio vya Wastaafu wa majeshi vitatuliwe haraka, kinachoendelea ipo siku kitatengeneza ‘matunda yasiyofaa
~ Kasoro kubwa katika Ofisi ya Hazina (Kitengo cha Malipo ya Pensheni za Wastaafu)
 
Barua ya kuthibitishwa kazini kwanini mwajiri asiwe nayo yeye ? Jeshi linaeendeshwa kizamani sana
 
Wabongo umuomba Mungu wapate kazi wakisha pata wana anza dharau na roho mbaya kukwamisha mambo ya wenzao utazani pesa ni zao ..kuna mtumishi wa mahakana kastaafu mwezi wa 7 kalipwa ml 5 nilishtuka sana aseee kumbe kuna watu mna pewa pesa kidogo ivyoo
 
Haya ndio mambo ambayo huwabadilisha vijana na kuanza kujilimbukizia mali kwa ufisadi pindi wakiona wazee wao wanavyo hangaika baada ya kustaafu.
Hii nchi ina mambo yanaumiza sana kwakweli, yaani miaka 40 unakuja kuambulia 5millions...🤔
 
Safi sana.

Mnapaswa msipewe hata mia.

Mna maujinga mengi kazi kulinda CCM.
 
Mimi hayo mambo ya kuajiliwa sitaki kuyasikia...tena kwenye ulinzi ndo worse kabisa.
Mnawalinda wanasiasa halafu wanawageuka baadae
 
Tunaandika ujumbe huu tukiwa na huzuni ya kiwango cha hali ya juu kutokana na yake tunayopitia, sisi ni wastaafu tuliokuwa Watumishi wa Umma ndani ya Wizara ya Ulinzi, tumefanya kazi kwa vipindi tofauti, baadhi ikiwa ni miaka 35 hadi 40 na kuendelea.

Wengi wetu tulikuwa ‘Nursing Assistants’ kwenye vikosi mbalimbali vya Jeshi, tuliajiriwa na kila mmoja alipewa barua ya kuajiriwa pia kila Mwajiriwa alikuwa na C/NO yake ya kupatia Mshahara kutoka Hazina (Pay Slip tunazo).

Tukiwa katika ajira tulikuwa tunapandishwa vyeo na pia tukapewa barua za kuthibitishwa kazini lakini baada ya sisi kustaafu wengi wetu hatukulipwa stahiki zetu kama inavyotakiwa, fikiria unafanya kazi Miaka 10 kisha unapewa Tsh. Milioni 5 hadi 10? Kweli hii ni sawa?

MADAI YETU YA MSINGI
  • Hela za likizo tulilipwa kidogo
  • Malipo ya NSSF / PSSF (wengi wetu tulipewa chini ya milioni 5)

Tunaomba ujumbe huu umfikie Rais wa Nchi, Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda, japokuwa mambo ya Jeshi kama haya huwa hayawekwi Mtandaoni lakini tumeona hii ndio njia pekee ya kuwasilisha ujumbe wetu kwenu.

WANAOHUSIKA WANATUGAWA
Taarifa tulizozisikia ni kuwa Rais Samia amepitisha malipo yetu akielekeza wote tunaodai tulipwe, baadhi ya Wahusika wanaosimamia wanatugawa kwa kuamua kutuambia baadhi yetu hawakuwa na barua za kuthibitishwa kazini na kundi lingine wanazo barua.

Wale walioambiwa wao wana barua za kuthibitishwa kazini wameambiwa wasubiri japokuwa muda unazidi kwenda hawajaambiwa chochote, wale wa upande wa pili wanaoambiwa hawana barua za uthibitisho kazini (licha ya kuwa walikuwa wakipandishwa vyeo kazini) ni kama wanaelekeza kuzimwa moja kwa moja.

KELELE ZA AWALI ZILISAIDIA
Tunaishukuru JamiiForums.com kwa kuwa awali wanaohusika hawakuwa na mpango nasi hata kidogo lakini baada ya kuweka andiko hapa, ujumbe ukafika na inadaiwa Rais Samia akaagiza tulipwe, kabla ya kuanza kuzungushwa na watu wa kati.

INADAIWA KUNA MTU AU WATU WANAKWAMISHA
Taarifa tulizozipata kwa kuwa nasi tuna vijana wetu tuliowaacha kwenye kazi, inadaiwa kuna watu au mtu ana maslahi binafsi, ndio maana anakwamisha akiamini wengi wetu ni wazee, hivyo hatuna uwezo wa kuendelea kudai haki yetu.

KELELE ZETU ZIMESAIDIA WALIPO KWENYE AJIRA
Inadaiwa kelele zetu na hiki kinachoendelea kimesababisha Watumishi waliopo kazini kwa sasa kuanza kusaidiwa, kupewa nyaraka za ajira mapema na maelekezo mengine ambayo sisi hatukuyapata.

Hoja zinazoendana, soma
~ Waziri Tax: Hakuna malimbikizo kwa wastaafu wanaohusiana na JWTZ
~ Vilio vya Wastaafu wa majeshi vitatuliwe haraka, kinachoendelea ipo siku kitatengeneza ‘matunda yasiyofaa
~ Kasoro kubwa katika Ofisi ya Hazina (Kitengo cha Malipo ya Pensheni za Wastaafu)
maandamano yakiitishwa mnakaa kimya
 
Back
Top Bottom