Rais Samia na Serikali yake wamefanya lipi jema mpaka sasa?

Amefanya vizuri kwenye mambo madogo ila makubwa anakosea, hajali haki za binadamu, na anawanyima wengine uhuru wao wa kutoa maoni.
Nitajie ni binadamu gani waliokosa haki toka Rais SSH aingie madarakani?

Vipi kuhusu yafuatayo;
  • UAMSHO walioshikiliwa toka 2012 wako nje
  • RUFAA ya akina Mbowe kesi ya Akwilina walishinda na fedha kurudi
  • Kesi 149 za kubambikiza TAKUKURU zilifutwa
  • Uhuru wa maoni, watu wanaongea sana bila kutishiwa
  • Kundi la wasiojukikana halipo tena
  • Utawala wa Sheria unafuatwa

Binadamu ameumbwa kutoridhika, hata ukimbeba mgongoni atakuambia umenibana na mbeleko
 
Think tank wa CCM ni nani?
 
1) Amerudisha uhusiano mzuri na nchi jirani zetu hasa Kenya- na kurudusha biashara mpakani.
2) Amejali Afya za wananchi kwa kukubali sayansi na technologia ndiyo njia sahihi ya kupambana na Uviko 19 ( chanjo za kuzuia uviko 19 zimeletwa nchini), Tanzania imepona kutengwa na nchi nyingi za kimataifa kwa kuwa na misimamo isiokubaliki na Shirika la afya duniani. Serikali itagharamia afya za wananchi kwa kutoa chanjo bure - siyo kila mtu kujigharamia kwa kununua bubiji,covidol na kuni kwa ajili ya kujifukiza.
3) Ameahidi kuifanyia kazi Katiba ya nchi.
4) Amejitahidi kurudisha utawala wa sheria.
5) Amerejesha uhuru wa vyombo vya habari- madudu ya serikali sasa yanaripotiwa.
6) kuna mengine mengi - ambayo sijaorodhesha.
7) uchumi wa dunia umeanza kufufuka baada ya kulala kwa karibu mwaka mmoja - bei ya mafuta imepanda duniani- hii itaathiri Jitihada za serikali kuzibiti mfumuko wa bei nchini.
 
Tutambue kuwa Samia si Magufuli japo aliwahi kusema kuwa yeye na hayati John Magufuli ni kitu kimoja. Linalowatofautisha ni uwezo wa kufanya uamuzi na kuusimamia.

Magufuli alifanya maamuzi magumu kwa mambo mengi. Moja kuu ni kurudisha nidhamu ya utendaji Serikalini. Kwa upande wake Samia, kama anavyojadiliwa na wachambuzi wa siasa, hana “maamuzi.” Mara nyingi anafika kwenye “briefings” za wateule wake akiwa hana kitu huku akitegemea wamsaidie kujua na kuamua.Wateule wanamuongoza kufikia uamuzi au kumlisha uamuzi na kwenda kuutekeleza. Yeye huishia kuwaambia haya ndugu zanguni nendeni mtekeleze hayo mlosema.

Wabongo hawatawaliwi kimama mama. Kwa aina hii ya utawala, utendaji wa mazoea umerejea na hakuna wa kukemea na kuchukua hatua
 
MPAKA SASA WAMEWEZA KUMZIBITIGAIDI MBOWE
 
Mengi sana, huoni sasa Airbus ikitoka Malawi inatua Zanzibar.
 
Amefanya vizuri kwenye mambo madogo ila makubwa anakosea, hajali haki za binadamu, na anawanyima wengine uhuru wao wa kutoa maoni.
Hajali haki za binadamu kwani mpaka sasa ameshamuua au kumpiga risasi nani ?
 
Kwenye kilimo, mfano wakulima wa mbaazi bei zumepanda toka tsh200/kg mpaka 1200/kg alafu bado mtu anasema hajafanya kitu
 
Wamemiss zile kiki za shujaa
 
Hyo shida ni ya nan? mfano anakuja gavana wa bot na ushauri wa kiuchumi, unataka rais alete ujuaji wakati kuna wasomi na wabonezi kwenye fani husika. sema watz uwajibikaji zero, mnataka rais awe mjuaji Kama bwana yule mchumi,mwanasheria,mkandarasi,askari ni yeye tu ndyo mjue mna rais
 
Kwenye kilimo, mfano wakulima wa mbaazi bei zumepanda toka tsh200/kg mpaka 1200/kg alafu bado mtu anasema hajafanya kitu
Ujue ukiwa humu mitandaoni unaweza dhani maisha huko kitaa ni hovyo balaa kumbe ni wapuuzi tuu wachache wanaompinga ndio wanazusha mambo ambayo hayapo.

Ni sekta nyingi tuu zinafanya poa,niliona hata kwenye ufuta wakulima wamepata bei nzuri,nimeona wameletewa pembejeo kwa wakati wale wa corosho nk.

Mambo mengine ambayo ni impacts ya global economy Rais hahusiki kama bei za mbolea.

Kilichokosekana saizi ni propaganda za majigambo kama ya Magu sasa ndio watu wanaona kama kuko kimya
 
Hamna kitu. katiba irekebishwe ikitokea Rais alieko madarakani anafikwa na la kufikwa uitishwe uchaguzi maana inaonekana kwa katiba ya sasa Rais alieko madarakani anateua makamu wa Rais goigoi kwa sababu wanazojua wao.
Yani turudie uchaguzi wakati mwaka haujapita hujui kuwa uchaguzi ni gharama hii system ni nzuri kuliko kuchoshana na uchaguzi Plus gharama
 
Amewaleteeni chanjo ya uviko 19 na tozo za miamala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…