Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Tunaanza kuimba wimbo mmoja, kipindi kile mlikuwa mnajitoa ufahamu
20210413_185552.jpg
 
Siku ya kuwafukuza Covid 19 Ubunge Mama nae atumie huo mwanya ili Bashiru na Polepole warudi Mtaani huku ili tuwagawane.
 
Hii kauli sijaielewa imekaa kijazba
By the way takwimu za makusanyo kila mwezi siku izi hatupati kulikoni?
 
Si mlifungiwa mna corona nyie!? Mkazuiwa kuingia kule🤔🤔
Au corona imeisha
Mimi baada ya Iddi naelekea Nairobi kutafuta Mwekezaji aje ili tuingie nae ubia kwenye Shamba langu la Mbaazi.
 
Mkuu yote tisa, kinacho nitia wasi wasi mkubwa sana sana ni hili la kusema kwamba wawekezaji lukusa kumilikishwa aridhi - hivi viongozi wetu wanajua hatari ya kuruhusu wageni kumiliki aridhi? JPM na wenzake walikuwa wakali kupindukia katika suala la wageni kumiliki aridhi,walikuwa wakali for a good reason,aliye taka kukosea kidogo ni Rais Kikwete alipo toa pendekezo kwamba magorofa ya NHC pale Morroco wanaweza kuwauzia wageni/majirani zetu, alishtuka alipo kumbushwa kwamba ukiuzia mgeni flat mnunuzi anakuwa na haki ya kumiliki kipande cha aridhi,ndipo zoezi lilipo sitishwa.

Masuala ya aridhi ni hatari sana sana siya kuchezea hata kidogo, tukumbuke kwamba vita vya ukombozi Zimbabwe na South Afrika vilisababishwa, among other things umiliki wa aridhi - we utamwambiaje mgeni kwamba ruksa kumiliki aridhi!!! Taifa la Kenya ni semi desert unafikiri ukitoa ruhuza za ajabu kama hizo kutatokea nini mwisho wa siku? Four fifth ya majirani wetu hao watahamia Tanzania kwa kisingizio cha kuwekeza kwenye Commercial farming/Mechanised Agriculture kama kisingizio cha kumilikishwa aridhi si tunasema wawekezaji kwenye aridhi ruksa kumiliki aridhi mwisho wa siku Taifa tutajikuta tunajifungulia a pandora box - wajukuu zetu wajikute wanaigia vitani kukomboa aridhi yao kutoka kwa wagine wakati sisi tumekwisha toweka Duniani - bottom line is: tuachane na uwekezaji ambao utakuja kuwa a ticking time bomb, nawambieni. Uwekezaji sawa, lakini tusifikie hatua ya kuruhusu kwamba in Tanzania everything goes!!

Mwanzoni mwa miaka ya themanini na tisini Viongozi wa Uchina (Deng Tsio Ping) alianzisha crusade ya wageni kuja kuwekeza kwa wingi huko Uchina kwenye nyanja za viwanda, sayansi na teknolojia,kuanzisha vyuo vya ufundi,kawapeleka wanafunzi wengi wakichina masomoni huko Marekani na Ulaya wengi nilisoma nao na walikuwa wanatwambia kwamba wakimaliza masomo watarudi kwao Uchina kujenga/endeleza Taifa lao. Deng Tsio Ping hakuwahi hata siku moja kuwambia wawekezaji kwamba China itawamilikisha aridhi wageni ambao wanataka kuwekeza Nchini Uchina - hakuwahi kwa kuwa alijuwa hatari ya kutoa tamko kama hilo.
 
Mama wacha achape kazi, hao watoto wa marehemu wanaosumbuliwa na jinamizi LA baba yao asiwasikilize awapuuze ajue sisi wanae tuna matumaini makubwa sana na yeye. Hao lengo lao wanataka kumtoa kwenye reli ili asitufikishe nchi ya ahadi.
Marehemu alikuwa mwendawazimu na watoto wake wameeithishwa uwendawazimu.

Rais SSH hawezi kufeli ndiyo maana ameacha FREE PRESS ili anayoyafanya yakosolewe.

Mwendazake aliminya Uhuru wa vyombo vya habari kwa sababu alijuwa kuwa anafanya UFISADI, utekaji, KUUA wakosoaji na kubagua Watanzania.
 
Raisi anayejiandaa kufurahisha kila mtu ni mtu anayeleta balaa. Hakuna rais wa aina hiyo, yaonekana hana ajenda na matamanio ya muda mrefu. anasikiliza wansema nini na kuhangaika kuwafurahisha. Tumekwisha!
 
Ni kama anafanya mambo mengi ili tu tumtambue kuwa yeye ni Rais...

Naona pia kama anahisi wenzake walikosea mahali fulani na fulani lakini yeye anaona anaweza rekebisha...

Sasa hizi mbio mbio zake ndio zanipa mashaka kidogo, maana akimbiaye huenda anakimbizwa au anakimbia kwa sababu zake




Sent using Jamii Forums mobile app
Tumpe muda ni mapema sana kuanza kuwa na wasiwasi so far so good .
 
... that's what we need! Vigezo na masharti kuzingatiwa.
"Vigezio na Masharti Kuzingatiwa"...., nimekuwa nikisubiri maneno haya kwa hamu sana.
Wewe umeyaona au kusikia popote akiyakazia haya maneno?

Baada ya hii yote, bado nasubiri nimsikie anayo mikakati gani ya kuyazingatia hayo uliyoandika.

Wasiwasi wangu mkubwa upo hapa; kwamba hakujiandaa kwa chochote juu ya hili. Na hapo ndipo tutakapoangamizwa huku tukishangilia!
 
Kama hatukuwahi kuinuka, basi tutakwenda chini zaidi.

Maana anayoyafanya leo, JK aliyafanya miaka 10 na nchi ikawa ya hovyo kabisa.
Nchi ilikuwa ya hovyo zaidi ya alivyoiharibu magufuli.mateso aliyotupa magufuli miaka mitano inatosha
 
ila tuache utani jiwe hakustahili kuwa raisi .(jpm) namfananisha na mwalimu anayechukua mkopo kujengea nyumba huku watoto wanakosa chakula bora.

kikwete nilimkubali aisee,unakula elfu kumi leo kesho una uhakika wa kuipata tena .michongo ilikuw mingi mitaani.


anawaambia ye n rais wa wanyonge( hapa unakuta na mwanaume kabsa anashangilia kuitwa mnyonge)



unajua jk alikuw anadeal na matajiri,matajiri nao wanaleta michongo mitaani.sasa huyo jiwe wenu aliwakandamiza matajiri nao wakaminya pesa.leo hii ww mnyonge unahangaika kumtafuta tajiri amuajir mtoto wako[emoji1][emoji1][emoji1]

MAZA NAONA KAMA ANAPAMBANIA KULETA AMANK ILIYOTOWEKA
 
Unaongea nadharia zaidi.
Unajua kuwa aafisa wanaojenga mitaani a vitongojini ni wa TRA?
Na rates za rushwa ni ngapi?

Na tukueleze kama hujui, TRA wanapiga WIZI sana kwa makampuni kwenye kukokotoa Witholding Tax.
Ndio maana na kwambia tatizo ni mifumo haipo, lakini tax officer akija offisini kwako kukagua anajua umepita wapi na umekwepa wapi , sasa anachofanya yeye au wewe ni kumwambia hii 100m badala ya kwenda serikakini tugawane wewe upate na yeye apate, sasa hapi ataacha kujenga.

Na issue ya withholding tax ni hivyo hivyo mfumo haujakamilika au watu wanafanya makusudi kwa faida zao.

Sasa hapo effective leader or efficient one atapigia kelele mifumo itengenezwe ili hayo mapungufu yasiwepo .
 
... wazee wa legacy fake Mkuu! Hawaamini mambo muhimu Mama aliyoyafanya ndani ya muda mfupi tangu akalie kiti. At least furaha imerejea nchini kwao ni uchungu kweli kweli wazee wa visasi!
Ulikuwa hucheki ?????
 
Back
Top Bottom