Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Walisema historia hiwa inajirudia. Sasa alianza Nyerere, watu wakawa wananunua kwa foleni. Wahujumu uchumi wakawindwa. Uchumi ukawa kama umedumaa. Akaja Mwinyi akafungulia 'ruksa'. Mambo yakapoa. Akaja Mkapa akabinafsisha na kuweka misingi fulani sawa kama vile malaka za umma. Akaja JK, ila sijajua alifanya nini hasa. Pengine alifanya mengi sana ila hakuwa anajitangaza huyu. Kisha akaja bulldoza. Kabana sana uchumi hadi watu wakalia na kufariki. Sasa kaja Samia anabanua uchumi na watu wanafurahi
 
Ungeweka hicho kitu ambacho hukielewi wazi ili tusaidiane mawazo.
Ni kama anafanya mambo mengi ili tu tumtambue kuwa yeye ni Rais...

Naona pia kama anahisi wenzake walikosea mahali fulani na fulani lakini yeye anaona anaweza rekebisha...

Sasa hizi mbio mbio zake ndio zanipa mashaka kidogo, maana akimbiaye huenda anakimbizwa au anakimbia kwa sababu zake




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila watanzania tukiambiwa ni waoga kuliko jibwa Koko ndio muamini. Yaan Rais anapambana kufungua milango ya biashara watu waweze kufanya biashara hata nje ya nchi sisi kazi ni kuogopa tu. Hatuwezi kuendelea kwa woga huo
 
Basi sawa, fungulia kila k2 then tupate mafuriko ya wawekezaji hapa TZ
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa kujifungia.

Dubai ilifanikiwa kuendelea ndani ya miaka 15 kwa kuweka sera rafiki sana za uwekezaji.

Sera zile za marehemu, za kufanya kila kitu kuwa kigumu, uonevu na uporaji wa mitaji, tusingefika popote.
 
tapatalk_1414808479.jpg
 
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa kujifungia.
Hizi "theories" za 'kujifungia na kufungulia' nchi nimeanza kuzisikia jana.

Hapo kabla sikuwa natambua kwamba Tanzania ilikuwa 'imefungwa'.

Nilicho na uhakika nacho ni kuwa, uwekezaji wa kitapeli ulikuwa umedhibitiwa.

Wizi wa madini kwenda nje ya nchi ulikuwa umedhibitiwa.

Biashara haramu (za kutoka nje ya nchi) zinazokwepa kodi zilidhibitiwa.

Utapeli wa ardhi ya watanzania ulidhibitiwa.

Utoroshaji wa nyara za serikali ulidhibitiwa.

Ujanja ujanja bandarini ulidhibitiwa!

Uingizaji na utoaji wa madawa ya kulevya ulidhibitiwa.

Hii dhana mpya ya "kufungulia nchi" bado sijaielewa vizuri.
 
Si mlifungiwa mna corona nyie!? Mkazuiwa kuingia kule🤔🤔
Au corona imeisha
Tulizuiwa lini?! Ulishawahi kwenda KE ukazuiwa?

Walichokuwa wanafanya KE kinafanyika duniani kote, kwamba, ukiingia nchi ya kigeni lazima uoneshe cheti kuonesha umepima na hauna maambukizi!!

Mbona mnahangaika sana kutafuta visababu visivyo na kichwa wala miguu!!

And FYI, suala la vyeti hadi sasa linaendelea tofauti ni kwamba, Serikali ya Magu ilikuwa haiaminiki kwenye ku-handle corona, kwahiyo yale makaratasi yenu watu walikuwa hawayataki, na ndo maana ukitoka na kikaratasi Bongo kinachodai eti umepima corona, watu wanakuambia "ajuaaa... tunaanza upya"

Hivi sasa inaelekea wanaanza kutuamini... wanajua hatutaleta tena mambo ya eti tumempima bata na kenge ili kuvitoa kasoro vifaa!!!

Kutokana na kuaminika huko, ukishapima TZ na kuwa na cheti, basi cheti hicho hicho kinatosha!!
 
Ni kama anafanya mambo mengi ili tu tumtambue kuwa yeye ni Rais...

Naona pia kama anahisi wenzake walikosea mahali fulani na fulani lakini yeye anaona anaweza rekebisha...

Sasa hizi mbio mbio zake ndio zanipa mashaka kidogo, maana akimbiaye huenda anakimbizwa au anakimbia kwa sababu zake




Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka Samia amekuwa makamu wa Rais wa serikali hiyo hiyo kwa miaka 6 hivyo ni suala la kurekebisha tu.

Tofauti na kama angekuwa ni mtu mpya anayeingia madarakani kwa mara ya kwanza.
 
Mashamba makubwa yamilikiwe na wa Tz na yale yenye kuhitaji foreign input basi yawe asilimia 51% wa tz .
Na kwenye viwanda iwepo component ya local kuwemo au shirika la umma liwe mbia
Utalazimisha Mtz aniliki shamba wakati hana uwezo wa kuliendeleza hilo shamba?
 
JK Heart Institute inatakiwa kujipanga manake kuna kila dalili ya kuongezeka kwa magonjwa ya moyo kutoka kwa Misukule ya Jiwe aliyoiacha inatapatapa huku ikiwa haiamini kwamba Jiwe is no more!!

CAG katoa ripoti... watu povu juu!!

SSH kawaagiza TRA watumie akili badala ya nguvu... watu mapovu juu!!

SSH katembelea KE na kutangaza kuifungua TZ... watu mapovu juu!!

Hivi nyie viumbe mna matatizo gani?!

Hata watoto wa Darasa la IV wakisikia wanayopinga hawa viumbe, I'm sure hata watoto wenyewe watashangaa!!!
 
Unaongea nadharia zaidi.
Unajua kuwa aafisa wanaojenga mitaani a vitongojini ni wa TRA?
Na rates za rushwa ni ngapi?

Na tukueleze kama hujui, TRA wanapiga WIZI sana kwa makampuni kwenye kukokotoa Witholding Tax.
 
Mlilishwa ujinga, mkaupokea ujinga, mkawa waumini wa ujinga.

Toa mfano japo mmoja tu wa uwekezaji wa kitapeli, vigezo vilivyotumika kutambua uwekezaji wa kitapeli, na tulipomgundua huyo mwekezaji wa kitapeli alishtakiwa wapi, alihukumiwa nini?

Marehemu aliendesha siasa za kitapeli. Siasa za kuwahadaa watu ili kutafuta sifa kutoka kwa wajinga.

Mambo ya yale ya kubambikia watu kesi asiowataka na kuwaita wahujumu uchumi, zile zilikuwa ni siasa za kishetani, zisizorakiwa kuwepo katika jamii yoyote iliyostaarabika.

Marehemu aliipeleka nchi kwenye primitive politics and primitive rule.
 
Back
Top Bottom