Mkuu yote tisa, kinacho nitia wasi wasi mkubwa sana sana ni hili la kusema kwamba wawekezaji lukusa kumilikishwa aridhi - hivi viongozi wetu wanajua hatari ya kuruhusu wageni kumiliki aridhi? JPM na wenzake walikuwa wakali kupindukia katika suala la wageni kumiliki aridhi,walikuwa wakali for a good reason,aliye taka kukosea kidogo ni Rais Kikwete alipo toa pendekezo kwamba magorofa ya NHC pale Morroco wanaweza kuwauzia wageni/majirani zetu, alishtuka alipo kumbushwa kwamba ukiuzia mgeni flat mnunuzi anakuwa na haki ya kumiliki kipande cha aridhi,ndipo zoezi lilipo sitishwa.
Masuala ya aridhi ni hatari sana sana siya kuchezea hata kidogo, tukumbuke kwamba vita vya ukombozi Zimbabwe na South Afrika vilisababishwa, among other things umiliki wa aridhi - we utamwambiaje mgeni kwamba ruksa kumiliki aridhi!!! Taifa la Kenya ni semi desert unafikiri ukitoa ruhuza za ajabu kama hizo kutatokea nini mwisho wa siku? Four fifth ya majirani wetu hao watahamia Tanzania kwa kisingizio cha kuwekeza kwenye Commercial farming/Mechanised Agriculture kama kisingizio cha kumilikishwa aridhi si tunasema wawekezaji kwenye aridhi ruksa kumiliki aridhi mwisho wa siku Taifa tutajikuta tunajifungulia a pandora box - wajukuu zetu wajikute wanaigia vitani kukomboa aridhi yao kutoka kwa wagine wakati sisi tumekwisha toweka Duniani - bottom line is: tuachane na uwekezaji ambao utakuja kuwa a ticking time bomb, nawambieni. Uwekezaji sawa, lakini tusifikie hatua ya kuruhusu kwamba in Tanzania everything goes!!
Mwanzoni mwa miaka ya themanini na tisini Viongozi wa Uchina (Deng Tsio Ping) alianzisha crusade ya wageni kuja kuwekeza kwa wingi huko Uchina kwenye nyanja za viwanda, sayansi na teknolojia,kuanzisha vyuo vya ufundi,kawapeleka wanafunzi wengi wakichina masomoni huko Marekani na Ulaya wengi nilisoma nao na walikuwa wanatwambia kwamba wakimaliza masomo watarudi kwao Uchina kujenga/endeleza Taifa lao. Deng Tsio Ping hakuwahi hata siku moja kuwambia wawekezaji kwamba China itawamilikisha aridhi wageni ambao wanataka kuwekeza Nchini Uchina - hakuwahi kwa kuwa alijuwa hatari ya kutoa tamko kama hilo.