Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Kwa trains zilizoonyeshwa hapo juu?

Hizo picha nilizoweka ni za Hyundai
Zina utofauti wa speed
Hata hii wameweka ya chini imewekwa kwenye taarifa tofauti kuwa ndio zinakuja Tz na speed itakuwa 160km per hour tofauti na za zamani 40km/hr

 
Mkuu kwa speed ya 350km/hr utaweza ku operate hiyo treni kwenye hii reli yetu ya SGR? au kuna namna njia yake inatengenezwa ili kuepusha maafa kwa raia na mifugo, maana ng'ombe kuvuka reli ni jambo la kawaida sana huku kijijini kwetu.....
Hata 160 km/h ni speed kubwa sana kwa treni yenye uzito mkubwa kama huu. Zingatia Moments of inertia wakati utakapo lisimamisha ghafla. Retardation distance yake ni kubwa sana.

Na treni zetu hazitakuwa na maximum speed ya 160 km/h bali ni zaidi kama 200 km/h hivi. Hiyo Figur ni average speed na sio maximum speed.
 
Sasa mkuu utafanyaje Kama serikali umeamua sikiliza watu primitive,kwamba badala ya kwenda mbele twaludi nyuma,twende na Bata mzinga
Hatulihitaji hilo dubwasha. Hatuna ulazima wa kulinunua kama hatuna pesa. Tunaweza kusubiri.
 
Mama ana kazi kubwa sana, come 2025 atakuwa amechoka sana, uraisi sio kazi ya kitoto, hasa kumuongoza mtanzania. Ukute kahujumiwa tayari...sio ajabu kukuta watanganyika wamemhujumu.
 
Ng’ombe akivuka mtaokota vipande tu maana ile itampasua! Hizo zinaitwa bullet trains mkuu ni hatari sana
Hata treni ya speed hii 160 km/h itamrarua vipande vipande. Zingatia kuwa mwili wa mnyama ni kama wa binadam tu asilimia kubwa ni maji, H2O.
 
Hyundai kwenye maswala ya mashine simuamini kabisa maana alishatuangushaga kwenye magari tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Atleast ningesikia kitu kama Mitsubishi Group ama China Holdings ningekuwa na imani ila kwa huyo Mkorea anachoweza ni simu za Samsung, TV, Mafriji na vitu vya LG tu!
 
Hata mie nahisi ile picha ni treni ya mizigo ndio imekaa ki old school ila ya abiria hasa waliotest akina mwingi inaonekana ina Recaro seats kabisa πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 

Mkuu hii kampuni ni ya zamani kidogo
Tangu 77 na wqnatengeneza vitu vingi mpaka vifaa vya jeshi sio treni tu
Wana kiwanda chao Philadelphia USA
Na train zao likija suala la speed ni nchi ya nne duniani kwa kutengeneza high speed train
France, Japan, China ikifuatiwa na hawa ambao wamevuka speed ya 430 km kwa saa

Hata kama hujaisikia ila unaweza kusoma historia yao tusiwabeze tu maana trains zao zipo USA na Canada pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…