Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Sasa nisemeje maana kila kitu wataalamu na waamuzi wa mwisho utafikiri wamo humu [emoji23][emoji23]
Imagine mtu anampa Amri Rais
Rais ni mtumishi wa umma ambao ndiyo sisi. Yeye sio Queen. Sisi tumempa Mandate ya kutuongoza na sio kutuamulia mambo tusiyo yataka. Akiendelea hivyo tuna uwezo wa kumtoa kwa kura zetu na kumchagua mwingine.
 
Hii point wanaipita tu,, hawajui ndio point ya msingi...

Yatima hadeki,, Kawaida maskini huwa unapata unachostahili na sio unachotaka.
Unakuta kuna wanataka mabasi ya mwendo kasi yawe na AC halafu nauli ibaki mia sita😀😀
 
Tena ni light-speed kama tunazoletewa na muonekano mzuri pia
Watu wanaponda muonekano tu ila tutamuita fundi maiko asawazishe [emoji23][emoji23]
Wakileta hio mzee baba itakuwa Magoli sana! Hata wale majirani Kunyans tutawanyoosha kilomolomo
 
Mtoa mada treni unazozitamani zina spidi ambayo reli yetu haiwezi kuhimili. Sasa huoni kama ni upotevu wa rasilimali. Unanunua treni ya zaidi kilomita 300 kwa saa wakati reli yako uwezo wake ni kuhimili chini ya kilomita 200 kwa saa?
 
Tumeshindwa kufika bei kwenye miundo inayovutia. Umesahau msemo MKIA WA MBUZI UNAJIKUNA UNAPOISHIA!!?
 
Rais ni mtumishi wa umma ambao ndiyo sisi. Yeye sio Queen. Sisi tumempa Mandate ya kutuongoza na sio kutuamulia mambo tusiyo yataka. Akiendelea hivyo tuna uwezo wa kumtoa kwa kura zetu na kumchagua mwingine.

Sio kwetu mkuu
Humu tunajifurahisha tu
Hata alietangulia alituburuza alivyotaka na tulishindwa kufanya kitu

Hii ni jamhuri ya JF acha tufurahie uhuru wetu hapa tukiwa kwenye bubble
 
Kwanini sasa tuwe na reli kama za Ulaya?
 
Hahaaaaa!!!hicho kitu kwa hii SGR yenu ni sawa gari aina ya limozini kuitumia ktk barabara za DRC!!hasa za mashariki mwa congo!!haitaweza kutembea hata hatua moja!!!weeee usilete utanii na hilo dude kichwa tu kama MJUSI KAFIRI!!!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Badala ya kujua specifications za hizo treni anaangalia muonekano. Halafu hela ya kununua treni anayotaka hana. Kazi kweli kweli
Ndugu Ndhani usidhani baada ya Rais kuapishwa March 19 ndo mchakato wa kununua mabehewa hayo ulipoanza. La hasha. Michakato kama hii huanza takribani mwaka mmoja kabla kabla ya ununuzi kufanyika. Hivyo hapa mchakato utakuwa ulianza tangu mwaka jana. It is a long process. Rais Samia amerithi kile kilichoanza na inambidi aendeleze tu.
 
kama ni hii kitu ni kweli sijui tutaficha wapi sura zetu wakija kina MK254 maana tulikuwa tunawakashu sn yale matreni yao ya makaa ya mawe....tumekwisha
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wabongo sijui huwa hatuna uwezo wa kufikiri, mtu kawekewa just a random photo "courtesy of..." tayari kashatunga na habari tokea kwenye picha...

"Electric trains are worth 215.7 billion won and electric locomotives 119.7 billion won. They will be delivered to Tanzania by 2024.", hadi sasa hakuna behewa lililoundwa...
 
Garama gani unazozizungumzia? Kwani watu watapanda hizo treni kusafirisha mizigo yao bure? Sie kitega uchumi cha taifa ili kituingizie mapato?
Kuna vitu vinaangaliwa ili wasiwabebeshe mzigo wanyonge kulipishwa kodi ili serikali iweze kutoa ruzuku kwa TRC ikijiiendesha kwa hasara, si umeona shirika la ndege ripoti ya CAG inasemaje? Kikubwa hivyo vichwa vihimili mikikimikiki ya kwetu mara gari limegonga treni mara ng'ombe wamegonga treni tena kwenye kichwa pale mbele nashauri waweke chuma cha pua atakae jipendekeza afyekelewe mbali na treni iendelee na safari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…