Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Mtu au taasisi yenye umri wa miaka 60 hupenda vitu vilivyofanana na umri wake.
 
Treni ya umeme mkuu ina Main Transformer ambalo kazi yake ni ku step down ile 25KV inayotokea katika overhed wires kupitia katika catenary hadi 1260VAC Kisha kuna diodes ambazo zina change ile AC voltage to DC Link voltage sasa itategemea unatumia Traction motors za aina gani ila kama ni Three phase Induction motors kuna inverter zina change hiyo DC voltage kwenda kuwa 3 phase AC kwa ajili ya ku zi feed Motors.
 
Hizo treni sio za Intercity na hazipigi masafa marefu. Hizo wenyewe wajerumani wanaziita Regionalbahn kwa kifupi RB yaani za masafa mafupi. Kuna RB za ina mbili, ziko za Private na zile za DB Deutsche Bahn.

(Weil du in Deutschland lebt, hätte ich von dir erwartet, dass du voll informiert bist mit über den öffentlichen Verkehr der Deutchen Bahn und dass du den Unterschied kennst.)

REGIONAL TRAINS zinatoa Services kwenye majimbo au states zao tu. Kama Nordrhein westfalen basi ni kwenye miji ya majimbo hayo na pengine majimbo yanayo pakana nayo. Kama Berlin na Brandenburg.

Wajerumani kila majimbo ya System yake ya utawala na Tickets. Usichanganye vitu. Soma kwenye hii link ujifunze.

 
Hapana sijapinga mkuu labda umenielewa tofauti lengo langu lilikuwa kutoa sababu kwanini kwasasa treni zilizokuwepo za meter gauge zinakwenda spidi ya 35-40km/hr katika hizo electric sina cha kusema mimi nilikuwa trained na Diesel Electric Locomotives kipindi cha nyuma hivyo kama mtaalamu siwezi kubeza mpaka nipopewa TECHNICAL DATA nipitie nifanye na majaribio ndiyo ninaweza kukwambia kitafaa au hakifai.
 
Wanakupa kile kinachoendana na uwezo wako wa kiuchumi. Tube train haiwezi kutumia reli ya 1.435 M hii ni kwa ajili ya Boxcab (Diesel/Electric Locomotives) tu na ndio itakayonunuliwa na TRC. Tube trains kwa Afrika bado tutasubiri sana.
Walio soma HKL na HJK tunaomba ufafanuzi zaidi katika haya maelezo.
 
Good walau engineer wewe umejitoa. Sisi wanachi tunachotoka kusikia ni ahadi za serikari kama zinatekelezeka.

Wataalamu mtuambie:

Train inazoagiza zinaweza kwenda Dar to Dodoma in three hours

Kuna cheaper alternatives which are better for whatever engineering reasons.

Maintanance cost of your alternatives zipoje and so forth.

Lakini atutaki kuongombewa train iliyonunua serikali sio bora kisa kuna nyingine only because it’s designs looks more appealing than the government purchase; hizo sio shida zetu kwakweli.

Mambo kama hayo yanakuwa na uhalali gani wa kukosoa manunuzi ya serikali, kutokana na ilichoahidi kutupa wananchi.

Kama serikali inaleta kile ilichoahidi kubisha inakuwa ni upuuzi; pingeni on merit of your expertise ila sio kupinga tu.
 
Uko sahihi kabisa huwezi kupinga kitu kabla hujakiona pia kujua technical data na kushiriki katika majaribio yake hapo ndipo utajua strength na weakness kisha mtafanya decision.

Naamini hakuna anayejua zinakuja electric train za aina gani ndo maana nilisema awali sina cha kusema kuhusu hilo.
 
Surely hiyo train ina specification zake na speed ability, tunaweza kukusamehe kama engineer kuhusu maintance and upkeep ya kitu ambacho ujawahi kukigusa.

Lakini atuwezi kukusamehe kama mshauri iwapo uwezi kujua hizo train zinaweza kwenda Dar to Dodoma in three hours; surely google could give you that info and more in engineering perspective.

Ndio haya tunayosema watu mnaotakiwa kutupa elimu wavivu wa kutafuta information si ndio maana kama taifa kila siku tunaingizwa chaka kwenye mikataba kama wataalamu wetu amtaki kujiongeza.

Usikarike kiongozi; mchana mwema kuna wasaa lazima tuwaambie ukweli acheni uvivu kwenye kujiongeza kama nchi tunahitaji ushauri wa watu mnaojiamini sio watu ambao tukiwauliza maswali hamna majibu.

Jumapili njema 👋
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] hapana mkuu upo sawa.

Ishu ambayo nakwambia ni ndogo sana hujanielewa kuna vitu ni basic sana katika Electric locomotives lazima uvifahamu tu kuna vitu kama

Traction Transformer Specifications,
Bogies & Wheelsets, Wheel Configurations and maximum curve negotiations, compressed air system, Maximum continues speed n.k

Lazima uyafahamu tu ila sasa kuna wahusika zaidi ambao hao ndiyo wanakwenda huko na michoro na data mbali mbali ili kushauriana na mtengenezaji.
 
Are you sure it's Samia who brought those machines?

Can you confirm hiyo picha ndicho kitakachokuja?

Are you sure hiyo look ni old fashion?

Tuna watu mnapenda Sana chokochoko
Naomba kukujibu swali lako la kwanza kama ifuatavyo, mimi sina uhakika huo, ila najua kuwa kwenye miradi mikubwa na ya kimkakati kama hii hakuna kitu kinaweza kufanyIka bila idhini yake. Na kama haitoshi, yeye ndiye anaye manage hizo hela ambazo, zitatuwezesha sisi kama nchi, kugharimia miradi hii na kwamba zitumike vipi.

Hakuna mtu ambaye anweza aka confirm kuwa hicho ndicho kitu kitakacho kuja, lakini ni swala linalo onekana dhahiri kuwa inawezekana ndiyo treni tuliyo nunu kwa sababu mtoa taarifa na hiyo picha ni mwuundaji mwenyewe. Sasa sioni kama mwuundaji na ambaye anafanya bishara ya kutaka products zake ziuzike aweke picha nyingine ambayo haihusiki kabisa na manunuzi tuliyo yafanya. Does it make any sense?

Kama wewe unafuatilia maendeleo ya aina za treni ambazo dunia hata ndugubzetu wengine Afrka wanazo, nafikiri usinge kuja na swali kama hilo? Kwani bila kujali uelewa wako wa New trend kwenye usafiri wa treni duniani na elimu yako uliyo ipata darasani kwa kuuliza swali kama hili kwenye karne hii 21 wakati picha ya hiyo treni unaiona, kwangu kusema ule ukweli inatia mashaka.

Sinanuhakika kama uwezo wako wa kutambua vitu vilivyo pitwa na wakati kulingana na mwonekano wa vitu uko in order. Inawezekana ukawa na deficit ya kutambua hilo, kitu ambacho mimi siwezi kulijadili. Ni wewe mwenyewe ndiye mwenye uwezo huo.

Jibu la Statement yako ya mwisho ni kwamba inategemea jisni wewe unavyo tafsiri mjadala kama huu in a Demokratie way. Kuna watu inawawia vigumu kufahamu au kuuiana mjadala wa kimaendeleo na democracy.

Kama sisi wananchi tuna mamlaka ya kumchagua Rais tunaye mtaka nadhani kidemokrasia tuna uwezo pia wa kuhoji kulikoni, kwa mambo ambayo tunayaona hayana tija kwenye ulimwengu ambao tunaambaa nao kwenye karne hii.
 
Hizo zilishanunuliwa na awamu ya 5,mama kafanyiwa delivery tu..sema kweli halina mvuto,likekaa kaa tu kama kontena la Maersk[emoji23][emoji23]
Si bora treni zetu za Tazara? Wakat mnawacheka Kenya mlikuwa mnakenua,ndo hivyo design ya 1.435 inataka hizi
 
Ndiyo mimi nami nilikuwa mstari wa mbele sana kupinga Design ya Ubungo Flyover. Ili niweze kukuthibitishia kuwa nami nilihusika katika jitihada ya kubadili mwonekano wa hiyo Flyover kwa kuangalia Funktionalität yake, anagalia hii link hapa chini;

 
kama ni hii kitu ni kweli sijui tutaficha wapi sura zetu wakija kina MK254 maana tulikuwa tunawakashu sn yale matreni yao ya makaa ya mawe....tumekwisha
Wote tunatakiwa tuwe na soni, tunawezaje kuchekana kwa kununua vitu vilivyotengenezwa na wanaume wa Asia wakati huo sisi kazi yetu kuzaliana kama kuku
 
Mmmmm!!!yaani kwa mawazo yako lile jengo la vioo la pale station ndio la kwanza la aina hiyo duniani?!!au unaishi SANGAMWARUGESHA?kwa hiyo kuona hiyo dreamliner kwao imewasaidia nini?ninachoweza kukwambia MUNGU FUNDI
Nionyeshe jengo jingine lolote lile linalo karibia kufanana na hili jengo letu.

Kuhusu Dreamliner hiyo itahitaji mjadala mwingine. Hapa tunazungumzia mwonekano wa High Speed Train.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…