Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Hizo zilishanunuliwa na awamu ya 5,mama kafanyiwa delivery tu..sema kweli halina mvuto,likekaa kaa tu kama kontena la Maersk[emoji23][emoji23]
[emoji38][emoji38][emoji38]
Hapana. Sikubaliani na hoja yako. Najua jinsi Hayati alivyokuwa na taste nzuri ya vitu. Kama treni tuliyo nunua ni hii, haitakuwa imenunuliwa kwenye awamu ya tano.
Angalia vitu ambavyo Hayati Magufuli amevifanya kama Dreamliner, Design ya Meli mpya Victoria, Madaraja na kadhalika. Magufuli alikuwa na Taste nzuri na alipenda vitu vizuri. Asingependa sisi tuwe na vitu vibaya hiyo nina uhakika.
 
Hiki kizazi kimejaa watu wapumbavu sana. Hiyo tender ilipita wakati wa Magufuli na mnataka kumlaumu Rais wa sasa ili mfiche madhambi ya mungu wenu aliyekufa kwa Covid.

Tafuteni lini hiyo tender ilikuwa awarded kwa hao Hyundai ndio muelewe.
 
Yaani hilo li kichwa la ng'ombe ndio kitaingia kwenye jengo la Tanzanite???
Kadogosa na wenzake wote wametutapeli kisaikolojia. Kama matreni yenyewe ndo haya basi si wangetuambia kitambo.

Wametuaminisha kwamba wanaleta kitu cha kisasa, wakatuwekea na mapicha. Wakatuletea na models zake halafu mwisho wa siku ndo haya.

Hii sio fea. Bora mngeuchuna tu, lakini sio kwa promo ile. Kwa kweli mmetuvunja moyo sana.
 
Mbona linafanana na "mitungi ya chang'aa" ya majirani yanayotumia diesel!

Ila kwenye hiyo link hawajaelezea ni model ipi italetwa maana hao Hyundai Rotem Wana design kibao tu.

Kama ni hiyo juu ikipakwa "marangi" ya TRL na akina Kadogosa,itakuwa madude ya kunyamazishia Watoto.

BTW: Nimefarijika kuona hiyo 160Km/h kumbe siyo fix.
 
Boss wangu umeenguliwa kwenye zabuni Nini? Maana sio kwa kulalamika huko.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hapana ni disappoitment tu. Kwanhali hii afazali ibaki reli peke yake mpaka hapo tutakapo kuwa na uwezo wa kununua vitu vya uhakika. Ni haibu kweli kweli.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Je! Wameeleza mchakato wa ugavi na ununuzi ulivyofanyika? Au ndo yaleyale ya jiwe na bombadia

Watuweke wazi tujue ni shi ngapi, sio watupige hela alafu baadae CAG atulete kumbukumbu zake hatutaki huo mchezo. Msichezee Kodi zetu!!!
 
Unajua hiyo picha ni nyuma ya Train?
 
Mzee
Hebu tuwekee picha ya mwonekano wa mbele

Hapa umetuwekea kichogo
 
Boss wangu umeenguliwa kwenye zabuni Nini? Maana sio kwa kulalamika huko.
Jamaa ameleta picha ya nyuma ya Train, mimi sijawahi kufika Ulaya ila nazionaga hizo Train kwenye movies na kiuhalisia kwa nyuma ni mbaya zote. Hakuna Train nzuri nyuma, kitu cha msingi ni kwamba zinasafirisha watu haraka na kwa usalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…