Rais Samia: nataka itumike "Single Source." Je, "Force Account" za JPM na "Zabuni Shindanishi" za JK zimeishia wapi? Sheria ya manunuzi imefutwa?

Single source hukubalika tu iwapo anakosekana aliye na uwezo wa kufanana na anayechaguliwa kwenye tendainayohitaji utaalamu mkubwa ama kama chombo kinachohitajika hakipatikani kwingine!!
 
Walioleta hizo procurement units katika serikali na taasisi za umma ni hao hao IMF na World Bank. Bila kufuata taratibu za manunuzi IMF na World Bank hawatoi fedha. Sasa sijui wamebadilika lini?

Time frame kuwa IMF wametukopesha fedha zitumike ndani ya miezi 9 ni uongo wa mchana kweupe! Lazima kuna nongwa hapa kwa nini single source?
 
Katika hizo sifa ulizoainisha ujenzi wa madarasa na vyoo vya shule ni nyeti?
 
Mkuu nani kakwambia hapa anatoa maoni kwa lengo la kubomoa ?
 
Unaongea as if unazungumzia nchi nyingine siyo Tanzania
 



Single source? dangerous......a joke! Unless is unaccounted money...
 
Wanajaribu kututisha ili tuogope KUHOJI madudu yao Mkuu lakini wanasahau baadhi ya Watanzania wa 2021 si kama wale wa miaka ya nyuma.

Ndiyo maana wamekuwa wakali sana siku hizi
 
Wanajaribu kututisha ili tuogope KUHOJI madudu yao Mkuu lakini wanasahau baadhi ya Watanzania wa 2021 si kama wale wa miaka ya nyuma.
Jamaa wamejipanga kuiba kweli kweli kwenye hii awamu.

Muda utasema aisee
 
Reactions: BAK
Hizo zote ni taratibu za manunuzi na zipo kisheria
 
Wewe ndio unapotosha. Single source hauiti watu zaidi ya mmoja watoe watoe bei zao. Ukifanya hivyo itakuwa "competitive bidding " na sio single source. Ni kweli single force inatumika kwa kazi za dharura ambazo haziruhusu kufanya tathmini ya maombi tofauti. Kwa mfano, kuna kisima cha mafuta kinawaka moto na mkichelewa kuuzima kitaleta athari kubwa kwa maisha na mali za watu.

Sehemu nyingine ni pale huduma hiyo au kivaa hicho kinapatikana kwa mtu mmoja. Mathlani mnataka spare part ya ndege ya Boeing. Bila shaka mtamuambia Boeing alete quotation yake na sio Airbus au Embraer. Sehemu nyingine ni unyeti wa mradi. Single source itatumika ili kupunguza idadi ya watu kujua mnachonunua. Kwa wenzetu hata silaha za kivita wanashi wazabuni.

Kwenye hili, sioni udharura au unyeti wa kujenga madarasa au ununuzi wa vifaa vya x-ray n.k. Aidha, hauwezi kusema kuwa kuna watu wachache tu wenye uwezo wa kujenga madarasa au kutuuzia vifaa tunavyotaka kununua. Kama tunataka madarasa ya dharura basi ni bora tungegeuza makontena kuwa madarasa.

Mwisho ni kuwa mpangilio wa matumizi ya hizi fedha ni uamuzi wetu. Tungeweza kuamua kuwasaidia wenye biashara za utalii kupunguza madeni waliyoingia baada ya watalii kuacha kuja Tanzania. Tungeweza kuzipa hospitali binafsi pesa ili zipunguze gharama za huduma kwa ajili ya watu wenye wagonjwa hawa. Tungeweza kuwasaidia wakulima wa mbogamboga na matunda kufidia hasara waliyopata baada ya ndege kuacha kuja Tanzania. Hatulazimishwi kujenga majengo yeyote. Kama tunaona yana umuhimu, basi tungetumia kwa ajili ya awamu za mwanzo za ujenzi halafu tungemalizia kwa fedha zetu baada ya muda uliowekwa kama sharti la mkopo utakapomalizika. Single source kwa hali hii sio nzuri.

Amandla...
 
Single source na force account zipo kwenye sheria mkuu. Ulishaona tenda za vifaa vya majeshi ya ulinzi na usalama vinatangazwa magazetini mkuu?
Zinatangazwa sana tu
 
Rais ameona mbali, uzalendo na adabu ya kutumia pesa lazima, usipofanya unafungwa over
 
Hapa sawa
 
Kwa mtindo huu rushwa itatamalaki na vikampuni vya mifukoni vingi vitaanzishwa, mwendazake alilaumiwa kwa Mayanga Construction huyu nae anajitengenezea mazingira.
Vikianzishwa sio tatizo ishu ya muhimu wafanye delivery na value for money ionekane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…