Bongo-mpya
JF-Expert Member
- Nov 10, 2020
- 311
- 244
Single source hukubalika tu iwapo anakosekana aliye na uwezo wa kufanana na anayechaguliwa kwenye tendainayohitaji utaalamu mkubwa ama kama chombo kinachohitajika hakipatikani kwingine!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walioleta hizo procurement units katika serikali na taasisi za umma ni hao hao IMF na World Bank. Bila kufuata taratibu za manunuzi IMF na World Bank hawatoi fedha. Sasa sijui wamebadilika lini?Mkuu mbona alifafanua vizuri kabisa,kwamba hizi pesa tulizopewa inabidi tuzitumie kwa muda wa miezi Tisa kukamilisha hiyo mipango yetu...
Sasa tukisema tufuate taratibu za manunuzi ya serikali au kugawa tenda basi miezi Tisa itafika na tutakua hatujafanya jambo lolote maana taratibu za ugawaji tenda au manunuzi za serikalin zinatumia muda mrefu.
Kwaio akapendekeza itumike njia ya single source ili kukimbizana na muda ...shughuli nyingine za kwenye miradi mingine wataendelea kama kawaida na force account.
Katika hizo sifa ulizoainisha ujenzi wa madarasa na vyoo vya shule ni nyeti?Mbona MTU ukitumia akili vyema utajua sifa za mradi kuwa either nyeti au dharura..! Dharura ni pale umepewa muda maalumu wa kukamilisha mradi ambao ukiúpima unauona ni mdogo ukicompare na scope ya kazi yakufanyika, au mradi kuwa na ulazima wa kukamilika kwa haraka. Na case ya unyeti ni mradi ambao sio kila mtu anapaswa kuona michoro yake kwa ajili ya usalama mfano ujenzi wa ikulu, gereza, benki kuu na mengineyo ya mtindo huo, hivyo hukifanya tenda shindani yakupasa kuweka na drawings kwa ajili ya makadirio ya gharama kwa wazabuni ambapo michoro hiyo kutakuwa na chance ya kuingia mikono ya watu wabaya.
Mkuu nani kakwambia hapa anatoa maoni kwa lengo la kubomoa ?Tusipende kila wakati kuwa wapotoshaji. Mama amelisema hili wazi na kwa ufasaha kwamva ile sheria ina ruhusu single sourcing kwahiyo kusema shetia iko wapi ndiyo hiyo ina options na sababu za kutumia hizo options amezisema ni kuhakikisha madarasa yanajengwa kabla ya watoto kuanza shule January.
Tuache kuyumbisha viongozi kwa sababu zisizo za msingi. Kweli tutoe maoni ila maoni hayo yawe na lengo la kujenga siyo kubomoa
Mwehu wewe!Single source na force account zipo kwenye sheria mkuu. Ulishaona tenda za vifaa vya majeshi ya ulinzi na usalama vinatangazwa magazetini mkuu?
Unaongea as if unazungumzia nchi nyingine siyo TanzaniaJapo nakubaliana na wewe kwa hili, ila urgency ya Mh. Rais pia inamashiko. Chamsingi ni hata hao single sourced wawekwe wazi ni akina nani ili kupunguza upendeleo wa watu wenye makampuni yao.
All in all corruptions hata kwenye hizo tendering zipo tu. Vyombo vyetu vya usalama vikifanya kazi yake vizuri na kulazimisha uwazi wala hakuna tatizo
Rada za kijeshi au zile za Airports? Rada za kijeshi haziwezi kutangazwa ng'oo!!Tenda ya kufunga rada ilitangazwa
Ndiyo maana wamekuwa wakali sana siku hiziSiku hizi Mkuu ni 90% kibindoni.
Sawa mimi mwehu. Wewe je?Mwehu wewe!
Leo wakati Rais akizindua mpango wa maendeleo (tafsiri "matumizi") ya pesa ya Covid kutoka IMF, amesema anaagiza watumie "single source" kwenye manunuzi na kandarasi. Kasema zabuni za kawaida zinatuchelewesha, hataki kuzisikia.
Swali langu lina sehemu mbili tatu:
hivi taratibu za matumizi ya zabuni shindanishi haziko kisheria ?
the biggest political upheaval ever in this country, ukiondoa Nyerere kufukuzwa Ikulu na jeshi kwa masaa 48, ni pale Prime Minister Lowassa na Principle Secretary Msabaha na wengine walipotimuliwa na shinikizo la tume ya Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni, procurement and tendering.
likaja wimbi kubwa la kutilia mkazo mambo ya procurement, watu mpaka mameneja kwenye mashirika na mawizara wakapelekwa vyuoni na kwenye ma semina kusomea kozi za procurement, sheria ikawa amended ikapewa meno, ikaundwa regulatory body inayoshughulikia procurement tu.... tunakumbuka ?????
haya, akaja Marehemu, akawa anauliza maafisa majukwaaani, mnatumia "force account" ? Force account ikawa habari ya mjini.
sasa leo Rais Samia katangaza anaagiza watumie "single source."
Single source ni nini?
Force account ni nini?
Na zabuni shindanishi zimefutwa lini?
na kwa nini zilikuwa haliteti tija ?
na ni wapi wameona single source au force account ni bora zaidi? Kwa ripoti gani?
tumeacha kupigwa kwenye makandarasi toka single source and force account zije ?
Na Rais anawezaje kufuta sheria ya bunge thabiti jukwaani ?????
Ndiyo maana wamekuwa wakali sana siku hizi
Jamaa wamejipanga kuiba kweli kweli kwenye hii awamu.Wanajaribu kututisha ili tuogope KUHOJI madudu yao Mkuu lakini wanasahau baadhi ya Watanzania wa 2021 si kama wale wa miaka ya nyuma.
Rada za kijeshi au zile za Airports? Rada za kijeshi haziwezi kutangazwa ng'oo!!
Wewe ndio unapotosha. Single source hauiti watu zaidi ya mmoja watoe watoe bei zao. Ukifanya hivyo itakuwa "competitive bidding " na sio single source. Ni kweli single force inatumika kwa kazi za dharura ambazo haziruhusu kufanya tathmini ya maombi tofauti. Kwa mfano, kuna kisima cha mafuta kinawaka moto na mkichelewa kuuzima kitaleta athari kubwa kwa maisha na mali za watu.Mbona huwa mnapenda kupotosha mambo bila sababu?
Utaratibu wa single sourcing upo kisheria,na umekuwa ukitumika mara nyingi katika manunuzi ya serikali pale inapohitaji huduma za dharura.
Iko hivi, angalau watoa huduma watu wanaombwa kutoa bei zao,halafu mwenye bei ya kuridhisha anapewa kazi.
Zinatangazwa sana tuSingle source na force account zipo kwenye sheria mkuu. Ulishaona tenda za vifaa vya majeshi ya ulinzi na usalama vinatangazwa magazetini mkuu?
Rais ameona mbali, uzalendo na adabu ya kutumia pesa lazima, usipofanya unafungwa overMkuu single source hutumika kwa case ya miradi ya dharura( uharaka) au miradi yenye unyeti( confidential) hivyo mh. Rais ameona time tuliyonayo ni ndogo kwa mpango husika kwa hiyo miradi mingine itaendelea kufuata utaratibu wa kawaida either forced account au competitive tendering.
Hapa sawaMkuu mbona alifafanua vizuri kabisa,kwamba hizi pesa tulizopewa inabidi tuzitumie kwa muda wa miezi Tisa kukamilisha hiyo mipango yetu...
Sasa tukisema tufuate taratibu za manunuzi ya serikali au kugawa tenda basi miezi Tisa itafika na tutakua hatujafanya jambo lolote maana taratibu za ugawaji tenda au manunuzi za serikalin zinatumia muda mrefu.
Kwaio akapendekeza itumike njia ya single source ili kukimbizana na muda ...shughuli nyingine za kwenye miradi mingine wataendelea kama kawaida na force account.
Vikianzishwa sio tatizo ishu ya muhimu wafanye delivery na value for money ionekane.Kwa mtindo huu rushwa itatamalaki na vikampuni vya mifukoni vingi vitaanzishwa, mwendazake alilaumiwa kwa Mayanga Construction huyu nae anajitengenezea mazingira.