Rais Samia: nataka itumike "Single Source." Je, "Force Account" za JPM na "Zabuni Shindanishi" za JK zimeishia wapi? Sheria ya manunuzi imefutwa?

Kwa maana hiyo force account nayo inachelewesha?
 
Hivi kama rais alisema Mbowe ni gaidi na tayari waliokamatwa nyuma yake wameshahukimiwa unatarajia kwake kuvunja sheria ni kitu kitamsumbua? Magufuli aliiharibu taasisi ya urais sana na itachukua muda sana kuirejesha katika nidhamu yake.
Mkuu JK ndo alifanya taasisi ya urais iwe kwenye nidhamu yake? Mbona wana jamii forums mmekuwa kichekesho sikuhizi? Yani mpaka kusema wale wenzake walishahukumiwa nayo mnamuona Magufuli..!! Mbona watu wa ajabu nyie?
 
Hapo Sasa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kaleta Mchanyato, Mseto Kuna Mamlaka Zitashindwa Kufanya Kazi Zake


Hii Sasa Hivi Imewaibua Watu Kwenda BRELA Haraka Kusajiri Kampuni Tayari Kwenda Kupiga
Acha Tuone Japo Mupe....Muruke.....
Single sourcing can bring uniformity and reduce the cost of buying some critical materials of the project, if not compromised. Kwa mfano, kama mahitaji ya saruji yanajulikana na wanaotengeneza saruji wakatoa bei za kuuza, the cheapest can be given the opportunity to supply.
Shida yetu ni kupenda na kufanya rushwa. Hiko kinaweza kuwa kigezo cha kununua kitu kile kile mara nne ya bei. Kwenye hizi halmashauri zetu, kuna kina baba aambiliki wengi sana. wababe na wasiojari hata ubora wa kazi yenyewe. Imagine ndio wanakuwa mameneja wa hizo hela za ujenzi...na wale wanaojiita wasimamizi wa serikali, wazee wa chama.
Kuna wakati bila kutumia mbinu mbadala, mambo hayatakaa kuja kwenda. Nazikumbuka sana zile bilions za JK. Inahitaji moyo kuzifanyia audit leo
 
Utawaweza wabongo kwa ujuaji?
 
Issue vigezo..

Mtamlinganisha na nani na mchakato sio competitive?.

Maybe hapo kwny vigezo vya kumpat single source ndo patiliwe mkazo...for inclusivity..

Ni kweli Single source ofcourse iko fasta.,
Iwe monitored kwa karibu zaidi kuleta matokeo yanayotarajiwa...
 
Kabisa aisee nimewahi kuwasoma humu KE ambao siku zote wako jukwaa la Mapenzi wakiandika kule siasani wanaandika MADINI ya hali ya juu sana lakini ushiriki wao kule ni mdogo sana.

Kina mama tunaweza sio😅
 
Hili nalo neno
Masharti ya wafadhili/mkopo yazingatiwe
 
Anzeni na katiba ya chadema na cuf kwanza
 
Kama sikosei huo mkopo wa IMF wa $567 millions IMF wamesema kutakuwa na Audit December 2022 kama sikosei ili kuangalia kwamba mkopo huo unatumika katika masuala yaliyokusudiwa katika kupambana na COVID-19. Sikumbuki nilisoma wapi kuhusu hili. Ngoja nafasi ikiruhusu nitatafuta habari hii na kama nikiipata nitaiweka hapa.

 
Hii hapa Mkuu.

According to the IMF, Tanzania’s macroeconomic outlook hinges on satisfactorily addressing the pandemic, although significant downside risks remain due to uncertainties surrounding the course of the pandemic.

According to the Fund, Tanzanian authorities have indicated that they are committed to pursuing economic policies appropriate for addressing the impact of the pandemic and are committed to strengthening coordination and transparency to ensure that RCF and RFI resources are spent on fighting the pandemic.

These measures include publishing reports of RCF and RFI resources spent and undertaking a post-crisis audit of all pandemic-related spending.

Authorities also committed to strengthening governance and transparency to ensure that the financial resources are efficiently spent on addressing the crisis.



 
Upigaji UMERASIMISHWA rasmi na Chifu Hang Ya. Tuombe CAG Kichere asiendelee kutishiwa maisha yake na hivyo kufanya kazi yake kwa UWELEDI mkubwa ili kuanika UOZO wa wizi, ufisadi na ubadhirifu wa trillions za walipa kodi kama alivyofanya katika ripoti zake mbili zilizopita.

Kwa mtindo huu rushwa itatamalaki na vikampuni vya mifukoni vingi vitaanzishwa, mwendazake alilaumiwa kwa Mayanga Construction huyu nae anajitengenezea mazingira.
 
Hakuna kitu kibaya kama msaidizi wako namba moja ndio anakuwa mpinzani wako namba moja. Iliwahi kumtokea Julius Caesar na Chaka Zulu. Ila hao wapinzani wao hawakudumu!
 
Pamoja na kutojua ni kipi kimesababisha kutofuatwa kwa taratibu ziilizopo; kama hakutakuwa na usimamizi mzuri, hii inatoa mwanya na inaweza leta shida haswa kweye upande wa:-
1. uwazi na uwepo wa mchakato unaofuata haki katika kuwapata Wakandarasi (transparency & fairness);
2. thamani ya pesa katika utekelezaji wa mradi (value for money) kiasi ya kupelekea miradi husika kutekelezwa kwa gharama zisizo na uhalisia.
 
Haujui maana ya single source. Ukitumia mtindo wa Single Source hautaita quotations kutoka kiwanda cha Wazo Hill, Tanga, Mbeya, Mtwara n.k. Ukifanya hivyo ina maana unawashindanisha na itaitwa "competitive bidding" sio single source bid. Single source ni kusema kuwa baada ya kufanya tathmini ya hayo makampuni ( uwezo wake wa uzalishaji, magari waliyokuwa nayo, dealers wao n.k.) mnaamua kuwa Wazo Hill anafaa kwa hiyo ni yeye peke yake mtamuomba alete quotation ya kusupply saruji. Baada ya hapo ni negotiations kati yenu ni kuhusu bei, upatikanaji wake, kiasi mtakachonunua n.k. tu. Hamna kulinganisha bei za producers wengine ( bei ya madukani sio sawa na bei ya kwenye tenda). Katika hali hiyo, hauoni uwezekano wa mtu kuweza kuingiza maslahi yake katika mazingira ambapo mzabuni ni mmoja tu? Na vile vile mzabuni atasukumizwa na nini kupunguza bei yake wakati anajua hana mshindani?

Amandla...
 
Single sourcing nilivyoelewa ni hii ya critical items of the project to be source from one supplier. Mikoa iko kadhaa. Wilaya ziko kadhaa. Ndio maana kuna mtihani kwenye single sourcing
 
Single sourcing nilivyoelewa ni hii ya critical items of the project to be source from one supplier. Mikoa iko kadhaa. Wilaya ziko kadhaa. Ndio maana kuna mtihani kwenye single sourcing
Sio hivyo. Ukiamua wewe mwenyewe ku supply items basi aina ya mkataba unabadilika ambacho sio kitu kibaya ila hautakuwa Single Source. Huo unaweza kuwa "labour based contract" kwamba mkandarasi analeta utaalamu wake na nguvu zake za ujenzi lakini vifaa kama simenti, nondo n.k. ananunua mwenye mradi na anavifikisha kwenye eneo la mradi. Hivyo vifaa unaweza kununua kwa kutumia Single source.

Amandla...
 
Unadhani hawaelewi? Ni pingapinga tu hao.

Hata kama Serikali ingekuwa na uwezo wa wakuwawekea mabomba ya asali na maziwa wangepinga tu wangesema ni matumizi mabaya ya fedha za umma zilitakiwa zikakae benki zizae riba.
 
Nakubaliana na wewe unachosema lakini nikisikia Rais SSH akisema wale PPRA watoe mwongozo namna ya kufanya hiyo single source.

Yote kwa yote hata ukifanya competitive tendering, huwezi kuwazuia watu wa Procurement kula. Mbona miradi mingi tunayoiona kwenye CAG report inakuwa imepatikana kwa ushindani lakini bado unakuta watu wamekula.

Naona single source itakuwa nzuri ku comply na masharti ya mkopo kwenye timing. Ila Huwezi kuzia watu wa Procurement na tender board zao kula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…