Leo wakati Rais akizindua mpango wa maendeleo (tafsiri "matumizi") ya pesa ya Covid kutoka IMF, amesema anaagiza watumie "single source" kwenye manunuzi na kandarasi. Kasema zabuni za kawaida zinatuchelewesha, hataki kuzisikia.
Swali langu lina sehemu mbili tatu:
hivi taratibu za matumizi ya zabuni shindanishi haziko kisheria ?
the biggest political upheaval ever in this country, ukiondoa Nyerere kufukuzwa Ikulu na jeshi kwa masaa 48, ni pale Prime Minister Lowassa na Principle Secretary Msabaha na wengine walipotimuliwa na shinikizo la tume ya Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni, procurement and tendering.
likaja wimbi kubwa la kutilia mkazo mambo ya procurement, watu mpaka mameneja kwenye mashirika na mawizara wakapelekwa vyuoni na kwenye ma semina kusomea kozi za procurement, sheria ikawa amended ikapewa meno, ikaundwa regulatory body inayoshughulikia procurement tu.... tunakumbuka ?????
haya, akaja Marehemu, akawa anauliza maafisa majukwaaani, mnatumia "force account" ? Force account ikawa habari ya mjini.
sasa leo Rais Samia katangaza anaagiza watumie "single source."
Single source ni nini?
Force account ni nini?
Na zabuni shindanishi zimefutwa lini?
na kwa nini zilikuwa haliteti tija ?
na ni wapi wameona single source au force account ni bora zaidi? Kwa ripoti gani?
tumeacha kupigwa kwenye makandarasi toka single source and force account zije ?
Na Rais anawezaje kufuta sheria ya bunge thabiti jukwaani ?????