Rais Samia: nataka itumike "Single Source." Je, "Force Account" za JPM na "Zabuni Shindanishi" za JK zimeishia wapi? Sheria ya manunuzi imefutwa?

Rais Samia: nataka itumike "Single Source." Je, "Force Account" za JPM na "Zabuni Shindanishi" za JK zimeishia wapi? Sheria ya manunuzi imefutwa?

Utaratibu wa single source ndio uliotumika kujenga SGR Dar-Moro na Moro-Makutopora.Utaratibu ni mzuri Kama umefanya specification za kutosha na unajua uhalisia wa gharama husika.Hivyo mkandarasi au fundi anafuata masharti yako.Huu ndio utaratibu unaotumiwa na watu binafsi zaidi.Ubaya ni kuwa baadhi ya maeneo yanaweza kuleta upendeleo lakini kwa nature ya project yenyewe sioni tatizo la single source ila umakini unahitajika.
 
Nakubaliana na wewe unachosema lakini nikisikia Rais SSH akisema wale PPRA watoe mwongozo namna ya kufanya hiyo single source.

Yote kwa yote hata ukifanya competitive tendering, huwezi kuwazuia watu wa Procurement kula. Mbona miradi mingi tunayoiona kwenye CAG report inakuwa imepatikana kwa ushindani lakini bado unakuta watu wamekula.

Naona single source itakuwa nzuri ku comply na masharti ya mkopo kwenye timing. Ila Huwezi kuzia watu wa Procurement na tender board zao kula.
Basi Mama kamaliza
Naamini yatasimamiwa...

Procurement is tricky..people play these things off books...auditor hawapati kitu

Watumishi ndani wanaformation za hatari...paperwork zimenyooka ila watu na 'percent' zao km kawaida

Na wazabuni nao ndo usiseme...bid riggers hawako nyuma wakipanga formation nani ashinde tenda ipi
Procedure zinafuatwa unadhani ni natural eliminations kumbe planned..
 
Haujui maana ya single source. Ukitumia mtindo wa Single Source hautaita quotations kutoka kiwanda cha Wazo Hill, Tanga, Mbeya, Mtwara n.k. Ukifanya hivyo ina maana unawashindanisha na itaitwa "competitive bidding" sio single source bid. Single source ni kusema kuwa baada ya kufanya tathmini ya hayo makampuni ( uwezo wake wa uzalishaji, magari waliyokuwa nayo, dealers wao n.k.) mnaamua kuwa Wazo Hill anafaa kwa hiyo ni yeye peke yake mtamuomba alete quotation ya kusupply saruji. Baada ya hapo ni negotiations kati yenu ni kuhusu bei, upatikanaji wake, kiasi mtakachonunua n.k. tu. Hamna kulinganisha bei za producers wengine ( bei ya madukani sio sawa na bei ya kwenye tenda). Katika hali hiyo, hauoni uwezekano wa mtu kuweza kuingiza maslahi yake katika mazingira ambapo mzabuni ni mmoja tu? Na vile vile mzabuni atasukumizwa na nini kupunguza bei yake wakati anajua hana mshindani?

Amandla...

Na pia single source inakinza dhumuni zima la economic stimulus kama unapeleka pesa kwa kampuni moja tu.

Kwa nini saruji ya matumizi ya serikali isinunuliwe Twiga, Tanga Cement, Dangote, Simba na Mbeya ili watu wengi zaidi wapate biashara na ajira?
 
Mkuu mbona alifafanua vizuri kabisa,kwamba hizi pesa tulizopewa inabidi tuzitumie kwa muda wa miezi Tisa kukamilisha hiyo mipango yetu...

Sasa tukisema tufuate taratibu za manunuzi ya serikali au kugawa tenda basi miezi Tisa itafika na tutakua hatujafanya jambo lolote maana taratibu za ugawaji tenda au manunuzi za serikalin zinatumia muda mrefu.

Kwaio akapendekeza itumike njia ya single source ili kukimbizana na muda ...shughuli nyingine za kwenye miradi mingine wataendelea kama kawaida na force account.
Safi sana mkuu
 
Watanzania Kila kitu tunajua,Kila kitu tunaunga mkono,Kila kitu tunapinga hata tusivyokua na uelewa navyo.
 
Nazihurumia pesa umma.
Bunge lipo kweli? Hapo sijahoji madaktari wa uchumi.
 
Na pia single source inakinza dhumuni zima la economic stimulus kama unapeleka pesa kwa kampuni moja tu.

Kwa nini saruji ya matumizi ya serikali isinunuliwe Twiga, Tanga Cement, Dangote, Simba na Mbeya ili watu wengi zaidi wapate biashara na ajira?
Kwa saruji wananunua wapi Kama sio Dangote now?
 
Mkuu JK ndo alifanya taasisi ya urais iwe kwenye nidhamu yake? Mbona wana jamii forums mmekuwa kichekesho sikuhizi? Yani mpaka kusema wale wenzake walishahukumiwa nayo mnamuona Magufuli..!! Mbona watu wa ajabu nyie?
Mkuu nidhamu ina maana pana sana. Kutimiza majukumu yako kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa hiyo ndiyo nidhamu ya kwanza. Magufuli ndiye mwasisi wa utaratibu wa kutawala bila kufuata sheria na kuingilia mihimili mingine kwake haikuwa tabu. Huko nyuma kabla yake ilikuwa ni nadra sana kuona rais akivunja sheria hovyo na kwenda kinyume kabisa na kiapo chake bila tashwishi wala hofu yoyote. Baada ya kifo cha Magufuli mama alianza vizuri na kwa hofu huku akifunikwa na kivuli cha hofu kuu kutokana na kifo cha Magufuli. Kumbuka kifo kinatisha kwa yeyote hivyo kinapotokea huwa hofu inatawala kwa muda,ila baada ya muda mfupi mama ameivaa Ile spirit ya Magufuli na ndio maana amekuwa mbaya kuliko Magufuli mwenyewe kwa sababu ukiiga tabia ya mtu mbaya utakuwa mbaya kuliko yeye.
So narudia tena Magufuli ameifanya taasisi ya urais kukosa nidhamu kuliko wakati mwingine wowote
 
Mkuu mbona alifafanua vizuri kabisa,kwamba hizi pesa tulizopewa inabidi tuzitumie kwa muda wa miezi Tisa kukamilisha hiyo mipango yetu...

Sasa tukisema tufuate taratibu za manunuzi ya serikali au kugawa tenda basi miezi Tisa itafika na tutakua hatujafanya jambo lolote maana taratibu za ugawaji tenda au manunuzi za serikalin zinatumia muda mrefu.

Kwaio akapendekeza itumike njia ya single source ili kukimbizana na muda ...shughuli nyingine za kwenye miradi mingine wataendelea kama kawaida na force account.
Acha kudanganya mifumo ya Tenda ipo kwenye Taneps na huko kuna kampuni chungumzima ni kuzishindanisha na kupata mshindi anapewa tenda, tatizo letu ni 10% kila zama zinaangalia loophole ya kupiga mpunga
 
Aisee procurement ni pasua kichwa,
Wanajionaga miungu watu wale, kazini kwetu tunamchakato wa kutimua procurement department yoote tuoutsource kazi zao kwa kampuni binafsi.
Washenzi sana, ndo maana viongozi wanakuja na haya mavitu
 
Mama afanye ref miradi ya maabara 2012-2014 nayo walitumia single source yaani mpaka Leo haijaisha kila mtumishi wa DED aligeuka kuwa mkandarasi na kulipana pesa bila certificate madudu, Takukuru wajipange haswa wapate mafungu ya ufuatiliaji la sivyo targets zinafeli
 
Hata Kama ipo kisheria hiyo Single source.
Je huko tamisemi ambapo Nina hakika hizi fedha zitaenda Moja Kwa Moja kwenye shule zetu.
Walimu wanajua taratibu hizi??? Au mpaka kutoa elimu tena???? ( Ambapo itachukua Muda zaidi).

Nashauri Mh Rais asiruhusu hili maana kuna watu watafungwa hapa.
Maana baadhi ya wataalam wa manunuzi ambao sio waaminifu wanaweza tumia mwanya huu kuwaingiza Chaka waliopokea fedha hizi katika akaunti zao.
 
Hivi kama rais alisema Mbowe ni gaidi na tayari waliokamatwa nyuma yake wameshahukimiwa unatarajia kwake kuvunja sheria ni kitu kitamsumbua? Magufuli aliiharibu taasisi ya urais sana na itachukua muda sana kuirejesha katika nidhamu yake.
Uongo una uadui NA MAGUFULI

ALICHOFANYA MAGUFULI NI KUINDOA SERIKALI KWENYE UMILIKIWA NA WATU FULANI

SERIKALI ILIKUWA IMEWEKWA MIKONONI MWA WATU FULANI WALIJIONA WAO NDIO WAO

HIYO NDIYO FURA YETU DARAJA LA WAMILIKI WA SERIKALI LILIVUNJIKA


SEMA LABDA ULIKUWA NA BIASHARA YA MAGENDO NA SERIKALI MILIKIWA NA WATU WALIONDOLEWA
 
Uongo una uadui NA MAGUFULI

ALICHOFANYA MAGUFULI NI KUINDOA SERIKALI KWENYE UMILIKIWA NA WATU FULANI

SERIKALI ILIKUWA IMEWEKWA MIKONONI MWA WATU FULANI WALIJIONA WAO NDIO WAO

HIYO NDIYO FURA YETU DARAJA LA WAMILIKI WA SERIKALI LILIVUNJIKA


SEMA LABDA ULIKUWA NA BIASHARA YA MAGENDO NA SERIKALI MILIKIWA NA WATU WALIONDOLEWA
Hata Magufuli alifanya hivyo hivyo . Aliitoa kwa hao wachache akaipeleka kwenye kikundi chake pia. Tena kikundi cha Magufuli kilikuwa cha hatari. Watu wake ndiyo hao akina Sabaya, Makonda, Bashiru, Dotto James na Polepele ambao waliruhusiwa hata kuiba na kuua
 
Kwa mtindo huu rushwa itatamalaki na vikampuni vya mifukoni vingi vitaanzishwa, mwendazake alilaumiwa kwa Mayanga Construction huyu nae anajitengenezea mazingira.
Yani uanzishe kikampuni chako tu leo ukapewe tenda na serikali!

Thubutu!
 
Leo wakati Rais akizindua mpango wa maendeleo (tafsiri "matumizi") ya pesa ya Covid kutoka IMF, amesema anaagiza watumie "single source" kwenye manunuzi na kandarasi. Kasema zabuni za kawaida zinatuchelewesha, hataki kuzisikia.

Swali langu lina sehemu mbili tatu:

hivi taratibu za matumizi ya zabuni shindanishi haziko kisheria ?

the biggest political upheaval ever in this country, ukiondoa Nyerere kufukuzwa Ikulu na jeshi kwa masaa 48, ni pale Prime Minister Lowassa na Principle Secretary Msabaha na wengine walipotimuliwa na shinikizo la tume ya Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni, procurement and tendering.

likaja wimbi kubwa la kutilia mkazo mambo ya procurement, watu mpaka mameneja kwenye mashirika na mawizara wakapelekwa vyuoni na kwenye ma semina kusomea kozi za procurement, sheria ikawa amended ikapewa meno, ikaundwa regulatory body inayoshughulikia procurement tu.... tunakumbuka ?????

haya, akaja Marehemu, akawa anauliza maafisa manunuzi na wakurugenzi wa Halmashauri majukwaaani, mnatumia "force account" ? Force account ikawa force account.

sasa leo Rais Samia katangaza anaagiza watumie "single source."

Single source ni nini?

Force account ni nini?

Na zabuni shindanishi zimefutwa lini?

na kwa nini zilikuwa haliteti tija ?

toka single source and force account zije na Magufuli tumeacha kupigwa? Kwa ripoti gani?

Na Rais anawezaje kufuta sheria ya bunge thabiti jukwaani ?????
Haya ndiyo matokeo ya mfumo wetu mbovu.

Unakuwa na mkuu wa nchi, hata kama hana uelewa wa jambo lolote yeye ndiye anakuwa mwauzi wa kila jambo hata kama ni kinyume na sheria, na hakuna wa kuhoji uamzi wake.

Ni muhimu pawepo na njia za kumwajibisha huyu mtu hata baada ya kumaliza uongozi wake, inapobainika alifanya maamuzi ya kipuuzi.
 
Yani uanzishe kikampuni chako tu leo ukapewe tenda na serikali!

Thubutu!
Sasa kigumu ni kipi hapo?

Kama wameweza kukiuka sheria za manunuzi, itakuwa shida gani kuwa na vikampuni vya mifukoni?
 
Back
Top Bottom