Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa amesema ya kuwa ajenda ya nishati bora ya kupikia ni ajenda ya Afrika na ni ajenda ambayo ameianzisha yeye na yeye ndio champion katika kuchochea ajenda hiyo. Amesema ya kuwa anazunguka Ulimwenguni kwote kutafuta fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa Afrika kupata nishati safi na bora ya kupikia.
Amesema ndio sababu hapa Nyumbani Tanzania serikali imefanya kazi kubwa sana katika suala zima la usambazaji wa umeme mpaka vijijini na kushuka kwenye vitongoji,ili kuhakikisha kuwa umeme unafika haraka haraka.
Amesema kuwa lengo ni kuachana na matumizi ya nishati ya kuni ambayo imeathiri mabibi zetu na Mama zetu kutokana na matumizi yake.lakini pia matumizi ya kuni yameathiri sana na kuchochea mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni za kupikia.
Rai yangu kwa watanzania ni kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa tunahamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa kupikia vitu ambavyo vimekuwa vikisababisha uteketezaji wa maelfu kwa maelfu ya miti kila Mwaka, na hivyo kuharibu mazingira na uoto wa asili.
Lakini pia kwa upande wa serikali ningependa kuishauri kuwa ifanye jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa nishati hizi safi na bora kwa ajili ya kupikia ,yaani umeme na gas vinapatikana kwa bei nzuri na ya chini ambayo hata mwananchi wa kule Isalalo wilayani Mbozi Mkoani Songwe ataweza kumudu gharama zake. Mfano kama mtungi mdogo ukajazwa kwa shilingi Elfu kumi au elfu 15 itavutia na kuwashawishi watu wengi sana kutumia nishati ya gas katika kupikia.
Kwa sababu ikiwa bei ya kujaza mitungi ya gas itakuwa juu,maana yake ni kuwa mwamko wa watu kutumia nishati safi kupikia nao utakuwa mdogo , hususani kwa watu wa vipato vya chini.na hivyo kukwamisha juhudi na ndoto za Mheshimiwa Rais kuona Taifa na wananchi wanatumia nishati safi na bora kupikia . Vile vile bei ya umeme kwa unit nayo ikipungua na kushuka maana yake watu watavutika wenyewe kutumia katika kupikia pasipo hata kutumia nguvu.
Kikubwa ni kuweka mazingira ambayo yatawashawishi na kuwahamasisha watu kutumia nishati safi badala ya kuni na mkaa. Na vishawishi hivyo ni kupunguza bei ya nishati hizi ambazo ni umeme na gas .bei iwe ni ile ambayo wengi watamudu kununua na kugharamia.
Kwa sababu hata ikitokea serikali ikawagawia watanzania wote mitungi ya gas bure kabisa nakuwajazia gas ya kuanzia .lakini bei ya kujaza mitungi hiyo ikawa juu bado utaona watanzania wengi wakirejea katika matumizi ya kuni na mkaa baada ya kuisha kwa gas ile ya bure waliyokuwa wamejaziwa awali. Hii ni kutokana na kushindwa kumudu gharama za kujaza mitungi ya gas tena au kununua umeme na kuutumia kupikia.
View attachment 3074836
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.