Rais Samia neema ilioletwa kurejesha utu na Haki za Binadamu

Rais Samia neema ilioletwa kurejesha utu na Haki za Binadamu

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
May 13, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan alikua mgeni katika maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC). Katika mkutano huo alitunukiwa tuzo ya kutambua mchango wake wa kulinda na kusimamia haki za binadamu na utawala wa sheria ikiwa ni kipindi cha mwaka mmoja tu tangu aingie madarakani.

THRDC hawakuitoa tuzo hiyo kwa bahati mbaya ukilinganisha na masaibu waliowahi kukutana nayo katika awamu ya tano, Katika siku 100 tu za uongozi wa Hayati Magufuli THDRC walitoa tamko lao kuhusiana na uendeshaji wa serikali ya awamu ya tano.

Ripoti hiyo ilieleza kwamba katika siku hizo 100 walibaini kutokwenda vizuri kwa baadhi ya mambo yahusuyo haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, demokrasia na utawala bora. Usalama wa wanahabari ulikua wa kutia mashaka kabla na baada ya uchaguzi, ufungaji wa baadhi ya magezeti na vyombo vingine vya habari pamoja na kudai yafanyike marekebisho ya sheria.

Lakini pia sekeseke nyingi zilitokea wakati wa awamu ya tano ikiwemo uvamizi wa kituo cha msaada wa kisheria (LHRC) na kushikiliwa kwa afisa wake Tito Magoti,kukatazwa mikutano ya siasa na kutekwa na mashambulizi kwa wanasiasa. Licha ya mengi aliofanya hapa kidogo kulikua na shida.

Baada ya March 19, 2022, Rais Samia kuapishwa mara nyingi ameonekana kutaka kila kitu kifanyike kwa kufata sheria lakini pia utu na haki za wtau ziheshimiwe, Kuonyesha yuko tayari kufanya hayo akaja na mkakati wake wa 4R yaan RECONCILIATION, RESILIENCE, REFORM and REBUILD OF THE NATION.

Moja ya Hotuba zake SSH alisema yuko tayari kukosolewa na leo ukipita kwenye mitandao ya kijamii hakuna sehemu ambapo mwananchi ataacha kutoa maoni yake kuhusu muelekeo wa awamu ya sita na hakuna anaetekwa ingawa wapo waliougeuza uhuru huo kuwa chaka la kutolea matusi bila kusahau ni kosa kisheria kumtusi mtu na kumdharirisha vipi kwa Rais hakika Samia ana moyo wa utu.
 
Back
Top Bottom