Rais Samia ni kazi kwako kuwaacha au kuwaondoa ‘for the sake of the nation and the party’

Sawa Ng'wigulu
 
Kampeno gani mkuu
Andiko lako linaonyesha wazi kwamba kuna watu unawalenga na siyo matatizo yaliyopo kutatuliwa.

Unapokuja namna hiyo kwenye mada, kuonyesha ushabiki badala ya utatuzi wa matatizo, unakuwa kama mpiga kampeni tu.

Hakuna ninayemtetea hapa kwenye haya maswala ya wafanya biashara na mfumo mzima mbovu wa ukusanyaji wa kodi. Pande zote mbili ni hovyo kabisa, na sitegemei kwamba kutakuwa na utatuzi wa maana kwenye swala hili.
 
Kama mpaka sasa hakuna PDF maza anachemka
 
Uchawi upo mpaka Sada hii nasoma Ikulu mawasiliano no press release
Nilijua mkutano ungeisha tu basi mwigulu out
 
Kuna nyuzi zaidi ya 7 za watu wametajwa na majina kabisa mimi sijamtaja mtu
 
Kama mimi nimefanya biashara ya 100 Million na nikapatq Faida ya 20 M kwa nini nilipe kodi kwenye 120 M badala ya 20 M ambayo ni profit..?
Mkuu, hiyo ndo shida ya serikali, kuna kitu inaitwa PAYE, mtumishi wa serikali na taasisi zake, PAYE inakatwa kwenye BASIC tu ILA kwa mtumishi wa sekta binafsi, PAYE inakatwa kwenye GROSS.

Jua, watumishi hawana namna yoyote ya kukwepa au ku-negotiate na afisa wa kodi!

Wakate kodi zote kwenye kuingiza mzigo, basi!
 
Simtetei mtu ila binafsi sioni kosa so Hakuna wa kuondoa na waondoke Kwa lipi? Kodi zote zimetungwa na Bunge ,hapo ni kubadili mechanism au approach ya kukusanya ila sio ishu ya Waziri hapo.
Yaani hili Bunge kibogoyo sana. Spika yupo busy kuongezea maisha magumu wananchi kwa kutaka jimbo lake. Maisha yanakuwa magumu kwa pesa zetu kutumika kijinga sana. Hili suala la kuwa na wabunge wa vitimaalum ni upuuzi sana.
 
Kitu ambacho hukijui
Wafanyabiashara wa sasa wana uelewa mkubwa sana tofaut na Wale wa zamani
Nazani umeona hoja zao
 
Achana na matumizi ya siasa katika kutatua matatizo kwa maneno tu. Hapa sheria itumike ili kubadilisha mambo ya Kodi. Jamaa wanafuata sheria ambayo imetungwa na hao hao wanasiasa. Ili yaliyoongelewa yaweze kutendeka shurti yapitishwe na kuwa sheria. Vinginevyo ni usanii kama usanii mwingine.
 
Ukiona watu wanamtaka mama maana yake hawasikikizwi! Nikuambie tu watanzania wetu tumechoka, TRA wamekuwa wezi wakubwa na rushwa mingi, acheni watu wagome
Yaani kwani haiwezekani, kubadilisha team za wafanyakazi wa TRA kutoka sehemu moja nyeti kama bandarini, long room au mipakani, kwenda sehemu nyingine(benchi), kila baada ya kipindi fulani', Ili kupunguza kiburi wanapokaa sehemu moja kwa muda mrefu, na matokeo yake ndo haya ya kuikosesha serikali mapato yaliyokusudiwa kutokana na wafanyakazi hao kutumia 'kanuni kandamizi za TRA vibaya....mie naona labda ikiwapendeza, hili nalo pia wakalitizame......
 
TRA ni wahuni sana, walimkadiria ndugu yangu kodi ya laki 6 kwa mwaka akalipa, kabla ya mwaka kuisha akawa amepata kazi ya madarasa ya covid, mwaka kuisha acc yake ikawa inasoma parefu lkn tayari kazi za covid zimeisha, aliporudi kujadiriwa tena mwaka unaofuata wakamwambia mwaka jana tulikadiria vibaya kwahiyo kuna kodi ilisaulika ya sh 2.8mln unatakiwa uilipe ndipo tuendelee na makadirio ya mwaka huu.Unaona huo ujinga.
 
Nyerere alishasema ukiona serikali inaangaika angaika na vikodi vidogovidogo ujuwe ni serikali ya Wala rushwa, r.i.p jpm wewe uliangaika na Kodi za wakubwa ambao Sasa wanapeta
 
Sasa anajikadiria Kodi mwenyewe eti alipe 150millioni!!!!!

Huyu ni mkwepaji mkubwa wa kulipa Kodi halali na anataka kutumia kichaka Cha mazungumzo haya, alipe anacho daiwa aache janjanjanja
Sasa kwanini TRA wakashuka tena from 30bil to 10bil baada ya yule mother kuyasusa makontena bandarini? Mpaka hapo hupati kitu akilini kuwa TRA wanapanga kodi kwa mafikirio on capital invested and not on profit?
 
Inatakiwa udondoshwe mbuyu, bila hivyo mambo yatarudi palepale. TRA wanafata wafanyabiashara nyumbani, kama si kwenda kuchukua rusgwa ni nini? Tena wote hao watolewe, ili watakaokuja wajihami.
Na ni wepesi kweli kupiga simu "Unadaiwa Mill kadhaa, na inaongeleka kupata punguzo" alafu ukiwajia juu hawapigi tena🤣🤣
Ifikie kipindi hizi kodi za mafikirisho ili kutengeneza mianya ya rushwa kwa watumishi wa TRA idhibitiwe kwa kuwawajibisha wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…