Rais Samia ni kinara wa maslahi ya wafanyakazi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
RAIS SAMIA NI KINARA WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI.

Na Bwanku M Bwanku.

Jana Mei Mosi, Dunia iliadhimisha Siku ya Wafanyakazi na Nchi yetu ilifanya Maadhimisho haya Kitaifa Jijini Dodoma ambapo Rais Samia alikuwa Mgeni rasmi. Na Mimi Bwanku M Bwanku leo Jumatatu Mei 02, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 19 nimechambua namna toka iingie madarakani Serikali ya Rais Samia ilivyojikita kutatua kero za Wafanyakazi ili kuimarisha mishahara yao ikiwemo kupunguza Kodi ya mshahara (PAYE), kulipa malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi 75,000 na kufanya mabadiliko ndani ya Utumishi ya zaidi ya Bilioni 180, kupunguza Tozo na adhabu kwa Wafanyakazi wenye Mikopo ya Elimu ya Juu n.k.

Zaidi Rais Samia amejibu kiu ya muda mrefu ya Wafanyakazi ya kuongezewa mshahara ambapo ametangaza jambo lipo na mishahara inaongezwa. Changamoto na kero za Wafanyakazi ni zaidi ya kuongezewa mishahara hivyo kuongeza mishahara pekee yake bila kushughulikia changamoto hizo bado unakuwa hujamsaidia Mfanyakazi na ndio maana Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kuondoa kero zilizokuwa zinakula mshahara wa Mfanyakazi kabla ya kuongeza mshahara wenyewe ili maslahi ya Watumishi yazidi kuimarika. Soma Makala yangu hapa nimekuwekea na soma Gazeti zima kupitia Link hapo chini. Utafaidi.

👇🏿👇🏿👇🏿

IMG-20220502-WA0011.jpg

IMG-20220502-WA0012.jpg
 
Kiukweli ndio rais wangu Bora Toka Tanganyika ipate uhuru...watu wamekuwa na amani Sasa...hakuna kutekana na watumishi wanafanya kazi kwa amani na tija inaonekana.

NB: Yule dikteta alituchelewesha Sana ,alifikiri anapendwa kumbe ulikuwa unafiki wa watumishi tu
 
.... kupunguza Tozo na adhabu kwa Wafanyakazi wenye Mikopo ya Elimu ya Juu n.k.

.... ametangaza jambo lipo na mishahara inaongezwa.
Acha porojo, nani alikuambia kila mfanyakazi alikuwa anadaiwa na Bodi ya Mikopo? Au hayo makato ya Bodi ya Mikopo yaliwahusu watumishi wa umma tu?

Halafu unazungumzia kuwa eti 'ametangaza', amesema kima cha chini kinaongezwa kwa kiwango gani? Watu hawahitaji tena maneno maneno, wanahitaji kuona mishahara imeongezeka, mbona Uhuru Kenyata ameenda straight na kusema wages zimeongezwa kwa 12% ?
 
Acha porojo, nani alikuambia kila mfanyakazi alikuwa anadaiwa na Bodi ya Mikopo? Au hayo makato ya Bodi ya Mikopo yaliwahusu watumishi wa umma tu? Halafu unazungumzia kuwa eti 'ametangaza', amesema kima cha chini kinaongezwa kwa kiwango gani? Watu hawahitaji tena maneno maneno, wanahitaji kuona mishahara imeongezeka, mbona Uhuru Kenyata ameenda straight na kusema wages zimeongezwa kwa 12% ?
Tanzania imejaliwa kuwa na waandishi wa habari wajinga sn kama huyu Bashite
 
Hilo gazeti lako kuna mtu mwenye akili timamu amewahi kulinunua kabisa anatoa 500 ake kwa ajili ya ujinga ujinga kama huu?
 
Jambo jema ,nyongeza juu, kazi iendelee kama nchi tuko pazuri mnooo kila mtu analamba asali, kama unabisha bishana na ccm au piga ngumi ukuta ila mshahara umepanda, acha ubishi

Screenshot 2022-05-02 at 21.22.57.png
 
RAIS SAMIA NI KINARA WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI.

Na Bwanku M Bwanku.

Jana Mei Mosi, Dunia iliadhimisha Siku ya Wafanyakazi na Nchi yetu ilifanya Maadhimisho haya Kitaifa Jijini Dodoma ambapo Rais Samia alikuwa Mgeni rasmi. Na Mimi Bwanku M Bwanku leo Jumatatu Mei 02, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 19 nimechambua namna toka iingie madarakani Serikali ya Rais Samia ilivyojikita kutatua kero za Wafanyakazi ili kuimarisha mishahara yao ikiwemo kupunguza Kodi ya mshahara (PAYE), kulipa malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi 75,000 na kufanya mabadiliko ndani ya Utumishi ya zaidi ya Bilioni 180, kupunguza Tozo na adhabu kwa Wafanyakazi wenye Mikopo ya Elimu ya Juu n.k.

Zaidi Rais Samia amejibu kiu ya muda mrefu ya Wafanyakazi ya kuongezewa mshahara ambapo ametangaza jambo lipo na mishahara inaongezwa. Changamoto na kero za Wafanyakazi ni zaidi ya kuongezewa mishahara hivyo kuongeza mishahara pekee yake bila kushughulikia changamoto hizo bado unakuwa hujamsaidia Mfanyakazi na ndio maana Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kuondoa kero zilizokuwa zinakula mshahara wa Mfanyakazi kabla ya kuongeza mshahara wenyewe ili maslahi ya Watumishi yazidi kuimarika. Soma Makala yangu hapa nimekuwekea na soma Gazeti zima kupitia Link hapo chini. Utafaidi.

👇🏿👇🏿👇🏿

View attachment 2208301

View attachment 2208302
Mama Rais Samia God chosen one. Sent straight from above.

Kikubwa utu na mkono kwenda kinywani mengine yatajijia tu.

Mbowe ametuasa tumuunge mkono mama kulisukumiza gurudumu la maendeleo mbele. Kama mbowe kasema wewe ni nani ukatae?

nyboma
 
Kuna mtu alitugeuza mazuzu, ila mimi sio zuzu kabisa, mtoa hoja hii daganya mazuzu wengine
 
Watu wameaanza kushangilia ubora wa kuku, huku hata hilo yai halijatagwa, sembuse kutamiwa ama hata kuanguliwa. Suala la nyongeza ya mshahara bado ni ahadi.

Ni vyema watu wakasubiri mwaka mpya wa serikali uanze, ndipo waweze kuona hayo mahesabu yalivyofanyika sambamba na ongezeko tarajiwa. Kumwaga pongezi byingi bila kutimizwa kwa ahadi, ni jambo ambalo linakosa mantiki kabisa.
 
Acha porojo, nani alikuambia kila mfanyakazi alikuwa anadaiwa na Bodi ya Mikopo? Au hayo makato ya Bodi ya Mikopo yaliwahusu watumishi wa umma tu?

Halafu unazungumzia kuwa eti 'ametangaza', amesema kima cha chini kinaongezwa kwa kiwango gani? Watu hawahitaji tena maneno maneno, wanahitaji kuona mishahara imeongezeka, mbona Uhuru Kenyata ameenda straight na kusema wages zimeongezwa kwa 12% ?
Tanzania imejaliwa kuwa na waandishi wa habari wajinga sn kama huyu Bashite
Kuna mtu alitugeuza mazuzu, ila mimi sio zuzu kabisa, mtoa hoja hii daganya mazuzu wengine
Kuna mtu kasoma hii kitu
Watu wameaanza kushangilia ubora wa kuku, huku hata hilo yai halijatagwa, sembuse kutamiwa ama hata kuanguliwa. Suala la nyongeza ya mshahara bado ni ahadi.

Ni vyema watu wakasubiri mwaka mpya wa serikali uanze, ndipo waweze kuona hayo mahesabu yalivyofanyika sambamba na ongezeko tarajiwa. Kumwaga pongezi byingi bila kutimizwa kwa ahadi, ni jambo ambalo linakosa mantiki kabisa.
Mada kama hizi za kumsifia Rais na hasa kuhusu maslahi na haki za mtumishi zinawaumiza sana Wanyonge.
 
RAIS SAMIA NI KINARA WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI.

Na Bwanku M Bwanku.

Jana Mei Mosi, Dunia iliadhimisha Siku ya Wafanyakazi na Nchi yetu ilifanya Maadhimisho haya Kitaifa Jijini Dodoma ambapo Rais Samia alikuwa Mgeni rasmi. Na Mimi Bwanku M Bwanku leo Jumatatu Mei 02, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 19 nimechambua namna toka iingie madarakani Serikali ya Rais Samia ilivyojikita kutatua kero za Wafanyakazi ili kuimarisha mishahara yao ikiwemo kupunguza Kodi ya mshahara (PAYE), kulipa malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi 75,000 na kufanya mabadiliko ndani ya Utumishi ya zaidi ya Bilioni 180, kupunguza Tozo na adhabu kwa Wafanyakazi wenye Mikopo ya Elimu ya Juu n.k.

Zaidi Rais Samia amejibu kiu ya muda mrefu ya Wafanyakazi ya kuongezewa mshahara ambapo ametangaza jambo lipo na mishahara inaongezwa. Changamoto na kero za Wafanyakazi ni zaidi ya kuongezewa mishahara hivyo kuongeza mishahara pekee yake bila kushughulikia changamoto hizo bado unakuwa hujamsaidia Mfanyakazi na ndio maana Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kuondoa kero zilizokuwa zinakula mshahara wa Mfanyakazi kabla ya kuongeza mshahara wenyewe ili maslahi ya Watumishi yazidi kuimarika. Soma Makala yangu hapa nimekuwekea na soma Gazeti zima kupitia Link hapo chini. Utafaidi.

👇🏿👇🏿👇🏿

View attachment 2208301

View attachment 2208302
Akili mbovu wenzake Kenya, Congo, South Africa walitangaza juzi na viwango (%), Samia bado anabwabwaja tu halafu mnamsifia! Acheni ujinga watanzania.
 
Kiukweli ndio rais wangu Bora Toka Tanganyika ipate uhuru...watu wamekuwa na amani Sasa...hakuna kutekana na watumishi wanafanya kazi kwa amani na tija inaonekana.

NB: Yule dikteta alituchelewesha Sana ,alifikiri anapendwa kumbe ulikuwa unafiki wa watumishi tu
Mimi na familia yangu naungana na wewe kumpongeza mama kwa kurudisha Tanzania katika furaha na nuru.Shujaa alituchezea sana
 
Hakuna hela hapo vijarida vya kupongeza Raisi Raisi hakuna lolote!
 
Hizi sifa zimeanza kukera sasa.....

Maneno tupu tu mnasifia hvi,,,, je siku watumishi account zikisoma ongezeko si mtatunyonga kabisa...
 
Kinara wa masirahi kwa wafanyakazi Ni SERIKALI YA AWAMU YA NNE CHINI YA Jakaya KIKWETE . record yake huyu mzee haijavunjwa.
 
Back
Top Bottom