Rais Samia ni kiongozi bora, ni mbeba maono na mvumilivu kweli

Rais Samia ni kiongozi bora, ni mbeba maono na mvumilivu kweli

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Anaweza kubezwa leo kwa anachofanya lakini akakubwa kesho na kiongozi bora hafanyi kwa ajili ya leo tu anafanya kwa ajili ya kesho. Baadhi ya nukuu na hotuba za Mwalimu Nyerere bado zinaishi mpaka leo na ukizisikiliza unaweza kufikiri ni leo ndio anazungumza. Kipindi Cha Mwalimu kuna walioshindwa kumuelewa hapo hapo na siku zinaposonga ufahamu wa kuelewa ukiongezeka wanamwelewa na Kuna wengine hawakumuelewa kabisa. Mwalimu aliishi kizazi Cha mbele Sana.

Rais Samia anajua mahitaji ya watu, ni mbeba maono. Ni kiongozi bora Sana. Inawezekana aina yake ya uongozi tukashindwa kuilewa leo lakini kesho ni mtaji wa kisiasa. Anatuandalia mazingira ya kesho.

Sio rahisi, halijawahi kuwa Jambo rahisi kwa watawala kuamua kukutana na watu ambao wakigeuka nyuma wanakutukana na hapohapo wanataka mkubaliane. Rais Samia kwa kujua yote bado anakaa na watu hao anafanya hivyo kwa ajili ya Tanzania, ni maono na matarijio ya watu. Mwalimu aliwahi kusema kiongozi bora ni yule aliyebeba matarajio ya wananchi hasa ya mpigakura.

Licha ya kutambua anachofanya Cha kukutana na upinzania pengine CCM hakiwaridhishi kabisa lakini kwa ajili ya Tanzania ameona njia hiyo ni salama na bora. Hapo ndipo tunapoona kabeba maono ya wananchi wote na si ya wana-CCM pekee.

Nasema tena, ukishindwa kuelewa anachofanya Rais Samia Sasa usilazimishe kujifanya unajua unatakiwa uwe mvumilivu wakati utafika utamuelewa.

Tunaomuelewa Sasa Rais Samia hatuteswi na kivuli Cha kuona atashindwa kuifikisha Tanzania mbele ila tunaiona Tanzania yenye maendeleo, maono ya Rais Samia ni kamili na hayana danadana wala kubumba na yanatimia kadiri mshale wa saa unaposonga mbele.
 
Ungemalizia "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti"
 
Rais SSH anaenda vizuri. Lkn kilele cha uzuri wake kitapimwa kwa upatikanji wa katiba mpya.

Maana hii katiba tuliyo nayo inamfanya rais kuwa mungu mtu.
 
Amebeba maono ya kuhamasisha ufisadi katika Taifa letu😁😁😁
View attachment 2234432
Kumuelewa Rais Samia inahitaji uwezo mkubwa wa Ufikiri na uelewa, hata kwa PHD au Uprofesa mtu alionao mara nyingine inakuwa kumuelewa bila kumsoma katikati ya mstari. Kauli hiyo Kama ulisikiliza nzimanzima ukaitafsiri nzimanzima lazima uelewe hivyo.

Rudi nyuma kidogo kabla ya hiyo nukuu uone ujumbe ulipotokea. Nakumbuka 2015 CHADEMA walikuwa wanafanya kazi kubwa Sana ya kukata hotuba za Mwalimu zinazoonyesha Lowassa hafai kuwa Rais na kutumia kipande kidogo kinachoficha ujumbe muhimu
 
Back
Top Bottom