Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Natanguliza kumpa heri na pole Mama yetu Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Haya mazonge zonge ya DP World yaliyotokea katika hii miezi karibia minne hivi yanatosha kumchosha mwanasiasa yeyote.
Yaliyotokea si bahati mbaya, ni mipango iliyosukwa na hatimaye kupata ridhaa ya Taasisi ya Urais.
Makosa tumeyaona, na ni maoni yangu kamba mama Samia ni msikivu na atayashughulikia kadri ya ushauri ulitolewa na wananci mbali mbali.
Tatizo linakuja pale waliomwingiza mama Samia katika shimo hili la kisiasa kuendelea kukaa kwenye viti vyao.
Kwanza , wale waliobuni tatizo hili lazima waondolewe na washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
Nitashangaa kama Profesa Mbarawa ataendelea kukalia kiti chake pamoja na Katibu Mkuu wake.
Wana sema Tanzania sasa imeingia into disrepute kimataifa, kutokana na suala hili la DP World.
Nchi imeingia aibu, na kuna uwezekano wa kushitakiwa na kupoteza fedha zetu za wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.
Pili, mama usijesikiliza ushauri wa kuzima moto kwa kuukalia moto na kubambika kesi zisizo na mbele wala nyuma ili kunyamazisha upinzani kwa suala la DP World.
Kesi ya Uhaini imekaa kijinga, na kila mtu anajua hilo.
Waliobuni kesi hii ya uhaini, kina IGP Wambura , wanakuingiza shimoni zaidi, gutuka ujitoe huko!
Kama kuna watu wana uwezo wa kufanya uhaini, ni wale wale ulio nao High Table yako.
Na hapo hapo niseme siungi mkono kutukana viongozi wetu, kwa kadri ya utamaduni wa nchi yetu.
Tatu, mama ukitatua hili la DP World na ukatoka salama, bado watanzania wanaimani na wewe 2025, na tusiichezee fursa hii.
Nne, Serikali yako na Bunge nadiriki kusema katika sakata hili la DP World hawajakusaidia kiuhalisia, na sababu za kufanya hivyo hazieleweki. Wengi wanajisahau kuwa mtu wa mwisho kukubali au kukataa kitu chenye kuleta hisia kama sakata la DP World ni wananchi wenyewe.
Na wananchi kiujumla wamesema bila kupepesa macho, mkataba wa DP World kama ulivyo ni HAPANA.
Mwisho nimtakie Mama Samia siku njema ili maamuzi yake yawe na tija kwake kisiasa na kwa watanzania kwa ujumla.
Week end njema.