Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Rais Samia amesema Waziri mmoja amedondoshwa kwa kuwa ni kawaida kwenye safari kuna ajali zinatokea. Amesema hayo katika hotuba yake baada ya kuwaapisha wateule wake aliowateua hivi karibuni.
Rais amesema alitamani team yake ya awali amalize nayo hadi kufika ngwe ya pili (Muhula wa pili wa uongozi) hata hivyo hali imekuwa tofauti.
Amesema kwa Makatibu wakuu wengi wamebaki ila sio kama hawana makosa bali 'mama analea'.
Aidha amejibu hoja za watu wa mtandaoni wanaosema kuwa mama anawachukua watu wenye akili kwenye maeneo tofauti, amesema watu hao wakibaki huko huwa wanakosoa sana hivyo ni bora waingie serikalini wajue ilivyo ngumu kutekeleza. Pia amesema mtu akiwa na akili ndio anamuhitaji zaidi lakini watanzania wote wana akili.