Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

Your browser is not able to display this video.
 
Yaani wanapeana vyeo kama zawadi tu ila sio utendaji bora, hii nchi wanaona kama wanaimiliki, kama ni kampuni yao vile, family company, leo anaweza kumpa mtu zawadi ya chochote hata kama alishashindwa kudeliver. Nchi za wenzetu hukuti haya mambo.
 
Chi inapita kipindi kigumu Sana hii!

Kina januari wana mabilioni ya pesa wameiba mpaka wamevimbiwa.

Magu aliwaona takataka mama akawaona lulu wakamnyea, leo anamkumbatia ili amnyee tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…