Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapo Samia anazidi kuwaumiza Sukuma Gang!

Hayo ni mambo yao CCM, yasiyutoe kwenye hoja kuu ya NO REFORM NO ELECTION
😂 😂 Ndugu yangu sukuma gang wenyewe ndio hao kina Kabudi?
 
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

Yajayo yanafurahishaaa!!
 
yaani wanapeana kama zawadi tu ila sio utendaji bora, hii nchi wanaona kama wanaimiliki,kama ni kampuni yao vile, family company, leo anaweza kumpa mtu zawadi ya chochote hata kama alishashindwa kudeliver. nchi za wenzetu hukuti haya mambo.
Kama nchi gani?
 
Watanzania wanakwambia nani kama mama. Yani wanaona ni sawa serikali kuendeshwa kama familia. Mwanafamilia akiiba huwa tunamalizana kifamilia hatupelekani mahakamani.
 
Nchi ya kujuana.Nasisi mkoa wa LINDI tunahitaji tupate hata waziri mmoja wa wizara.
 
Wale wa tunasusia uchaguz mjipange maana mwenyekiti wa kamati ya fitna amerudi.
Hii hesabu imepigwa vizuri kwa wenye siasa zenu
 
Nje ya mada.
Hivi ni nani aliegundua ukikumbatiwa upande mmoja ni lazima ugeuke na upande wa pili?
 
Amerudishwa kundini, ni mtoto wa mama. Nape bado mtoto wa kambo..jitahidi kujikomba kwa kiwango cha hali ya juu utarudishwa.
Omba ziara ya jimboni kwako, Malaika gabriel atakutokea, nuru itakungarisha!
 
Chadema wakae mkao wa kula
 
Back
Top Bottom