Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais Samia Suluhu Hassan, ametangaza kumrejesha Januari Makamba, Mbunge wa Bumbuli, baada ya miezi sita ya kutohudumu kama waziri.

Rais Samia alitoa tangazo hilo Jumatatu wakati wa ziara yake mkoani Tanga, akifananisha hatua hiyo na adhabu ya kifamilia, akisema: "Mwanangu nilimpiga kikofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa Mama." Hakutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za awali za kumuondoa kwenye baraza la mawaziri.

Makamba, ambaye alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje kabla ya kuondolewa kazini mwaka 2024, alikumbatiana na Rais Samia mara baada ya tangazo hilo, hali iliyopokelewa kwa shangwe na makofi kutoka kwa wananchi waliokusanyika.

Urejeo wake katika serikali umeibua mjadala kuhusu uwezekano wa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ingawa hakuna tangazo rasmi lililotolewa kuhusu nafasi mpya.

Chanzo: habarileo_tz

Na nilizozipata muda si mrefu ni kuwa Dogo JM kaomba apewe Wizara isiyo na Lawama nyingi ili yasije kumkuta tena!!!!
Uchawi upo. Familia ya Makamba walikuwa na mganga wao maarufu akiitwa Mohamed Mbega kwa sasa ameshatangulia mbele ya haki na ndiye pia alikuwa mkuu wa jopo la waganga wa JK, huyo mzee alikwa kiboko sana nafikiri kuna kijana wake aliyemuachia mikoba ndiye huyu anamrudishia January chakula chake.
 
Hii kitu ina kwaza kama sio kufedhehesha mzee. Imagine kuna vijana wenye uwezo,weledi na ari ya uzalendo wanao tamani sana kupata nafasi walipambanie taifa wanawekwa kando kinachoendelea ni reshuffling ya takataka zile zile.
yaani wanapeana kama zawadi, fadhila. hivi mmiliki wa hii nchi ni nani? october watanzania show them pls. ili chochote watakachofanya wajue wapo accountable kwa wananchi, wao ni vibarua tu wanawajibika, sio wamiliki wa nchi hii.
 
Huyu mganga wa Makamba ni balaa sana. Yes!

Naweza kusema haya mambo bila nguvu Lucifer nyuma Yako utafel Kwa Kila kitu. Iwe Kwa ofisi, Biashara, music, Sanaa, mpira n.k

Kipara kaupiga mwingi Mama Kawa mpole Aisee!!!🤔🤔🤔

Ok. Nitaenda Tanga nionane nae anipe maelekezo. Kapita wapi?
 
Attachments

  • hq720 (2).jpg
    hq720 (2).jpg
    76.3 KB · Views: 1
157d3ca7737a256e3dac71983df233b6.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametangaza kumrejesha Januari Makamba, Mbunge wa Bumbuli, baada ya miezi sita ya kutohudumu kama waziri.

Rais Samia alitoa tangazo hilo Jumatatu wakati wa ziara yake mkoani Tanga, akifananisha hatua hiyo na adhabu ya kifamilia, akisema: "Mwanangu nilimpiga kikofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa Mama." Hakutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za awali za kumuondoa kwenye baraza la mawaziri.

Makamba, ambaye alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje kabla ya kuondolewa kazini mwaka 2024, alikumbatiana na Rais Samia mara baada ya tangazo hilo, hali iliyopokelewa kwa shangwe na makofi kutoka kwa wananchi waliokusanyika.

Urejeo wake katika serikali umeibua mjadala kuhusu uwezekano wa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ingawa hakuna tangazo rasmi lililotolewa kuhusu nafasi mpya.

Chanzo: habarileo_tz

Na nilizozipata muda si mrefu ni kuwa Dogo JM kaomba apewe Wizara isiyo na Lawama nyingi ili yasije kumkuta tena!!!!
 
Pasco Mayalla kaa mkao wa kula....
Kuna za ndani zinakutaja sana jina lako......
 
Mama anaupiga mwingi, mama mitano tena. Huu ni uungwana na uzazi
Yan mtu kufanya ufirauni unayoikost nchi nzima ila mamake mdogo anamsamehe sababu ni familia nanyi mnapiga makofi, uungwana huo au ungese? Mtu kashindwa kudeliva, why asamehewe kama mtoto wako wa kumzaa wakati ile ni kazi na iko na interest za watu million 68 ?. Kwanini watu stupid mnakuwaga hamna chill until we know you guys are stupid all the way ? Why in Tanzania it's easy to know the ignorant than the brave ones ?
 
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

Samia anaona kila mtanzania ni mwanae. Ndiyo maana kila kitu sasa unaambiwa hiki na mama mara kile na mama. Wewe ni Samia Suluhu na siyo mama samia suluhu.
 
Amerudishwa kundini, ni mtoto wa mama. Nape bado mtoto wa kambo..jitahidi kujikomba kwa kiwango cha hali ya juu utarudishwa.
Omba ziara ya jimboni kwako, Malaika gabriel atakutokea, nuru itakungarisha!
Kama wewe ulivyo mtoto wa kambo kwa Tundu Lissu
 
I
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

likuwa ikijulikana kwa tuliosomea Cuba 🇨🇺 kwamba Januari na Nape ni just a matter of time watarudishwa kilingeni !

Vyeo ni kwa ihsani na kujuana na kufadhiliana bhana. !

Sasa naye atapewa Wizara gani kwa sasa ??!
Au uhakika wa Uwaziri baada ya Uchaguzi ???!! 🤣🤣😅 !

Sawa bhana wengine wawe wanadhalilishwa kila waendapo na wengine wawe wanaitwa kwenye maulaji hata kama wameshiba !

Mungu wetu ni huyo huyo mmoja ambaye kwenye kila Dini wanamuita kwa jina walilofundishwa na vitabu vyao !
Mungu wa mbinguni siku moja atawaona pia wale waliomo kwenye udhalilishwaji mkubwa uliotengenezwa na wale aliowapa pesa na madaraka Nchini ambao Eti waliona wao hawastahili kukosolewa 😳!

Mama hayumo kwenye lawama hizi !
Awamu ya Nne ndio wahusika wakuu !
 
Back
Top Bottom