Pre GE2025 Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

We want changes!
We need to see development physically!

We DON'T NEED a political drammas!
 
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

Kweli Taifa limepata mama, kwa maana hata kama mtoto ni jambaka sugu, mama hawezi muacha.
 
Yaani wanapeana vyeo kama zawadi tu ila sio utendaji bora, hii nchi wanaona kama wanaimiliki, kama ni kampuni yao vile, family company, leo anaweza kumpa mtu zawadi ya chochote hata kama alishashindwa kudeliver. Nchi za wenzetu hukuti haya mambo.
Ndio hivyo na hatuna cha kufanya zaidi ya kulalamika tu.
 
Kwakweli mama samia yupo vizuri sana,leo nimeshuhudia mradi mkubwa wa bwawa la umwagiliaji mkomazi niseme tu hongera sana mama ,octobar hatutakuangusha ,Mungu akubariki na akupe maisha marefu
 
Siasa ni hatari , kumbe aipigwa Kofi . Kofi Hilo it means ilitokea kero Fulani hivi . Ni kero ipi hiyo ? , Mimi na wewe hatuijui
malope alileta ukuwadi wa kiborn town, akala kofi.
 
Siasa ni hatari , kumbe aipigwa Kofi . Kofi Hilo it means ilitokea kero Fulani hivi . Ni kero ipi hiyo ? , Mimi na wewe hatuijui
Pleasure of the President - Balozi Kagasheki
 
Yaani wanapeana vyeo kama zawadi tu ila sio utendaji bora, hii nchi wanaona kama wanaimiliki, kama ni kampuni yao vile, family company, leo anaweza kumpa mtu zawadi ya chochote hata kama alishashindwa kudeliver. Nchi za wenzetu hukuti haya mambo.
Hii kitu ina kwaza kama sio kufedhehesha mzee. Imagine kuna vijana wenye uwezo,weledi na ari ya uzalendo wanao tamani sana kupata nafasi walipambanie taifa wanawekwa kando kinachoendelea ni reshuffling ya takataka zile zile.
 
CCM kipindi hiki ina mgombea dhaifu na asiyekubalika kuliko kipindi kingine chochote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
 
Rais Samia Suluhu Hassan, ametangaza kumrejesha Januari Makamba, Mbunge wa Bumbuli, baada ya miezi sita ya kutohudumu kama waziri.

Rais Samia alitoa tangazo hilo Jumatatu wakati wa ziara yake mkoani Tanga, akifananisha hatua hiyo na adhabu ya kifamilia, akisema: "Mwanangu nilimpiga kikofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa Mama." Hakutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za awali za kumuondoa kwenye baraza la mawaziri.

Makamba, ambaye alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje kabla ya kuondolewa kazini mwaka 2024, alikumbatiana na Rais Samia mara baada ya tangazo hilo, hali iliyopokelewa kwa shangwe na makofi kutoka kwa wananchi waliokusanyika.

Urejeo wake katika serikali umeibua mjadala kuhusu uwezekano wa mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ingawa hakuna tangazo rasmi lililotolewa kuhusu nafasi mpya.

Chanzo: habarileo_tz

Na nilizozipata muda si mrefu ni kuwa Dogo JM kaomba apewe Wizara isiyo na Lawama nyingi ili yasije kumkuta tena!!!!
 
Angekuwa magufuli asingeogopa na kuuuma na.kupuliza angesema bayana kosa la makamba na asingemwambia nimekusamehe.

Hakika hakuwa mnafiki sana JPM
 
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga leo Februari 24, 2025, amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, lakini akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

"Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu Januari (Januari Makamba) hapa aje huku, arudi kwa mama. Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi, anakufichia chakula si ndio hivyo. Sasa mwanangu nilimpiga kofi, nikamfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo," amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba

Rais mzima anatetea na ku normalize gender based violence.

Rais mzima hajui kuwa akisema kamuadhibu waziri wake, ana wajibu wa kutueleza kwa nini alimuadhibu.

Rais mzima ana normalize wakina mama kunyima chakula watoto.

Samia ni mjinga sana.
 
Back
Top Bottom