#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

#COVID19 Rais Samia: Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu

Mtoto wa Nyerere

Senior Member
Joined
May 21, 2021
Posts
129
Reaction score
689
Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya.

Swali hizo cost zinazotumika kulazimisha watu wachanjwe zinatoka wapi? Kwanini pesa zisielekezwe kwenye mambo mengine ya msingi.

Mama wanaomshauri wanamponza Sana.

---
Rais Samia Suluhu, amemzungumzia mhudumu wa afya anayepita nyumba kwa nyumba kuchanja chanjo ya Uviko-19, akionya kampeni hiyo isitumiwe vibaya katika kuwalazimisha watu kuchanja.

Jana katika mitandao ya jamii, kulisambaa habari na picha ikimuonyesha Ofisa wa Afya wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma akipita nyumba kwa nyumba kuwachanja chanjo ya Uviko 19 watu zaidi ya 160 kwa siku moja.

Akizungumzia leo Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalum wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma hilo, Rais Samia amesema asingependa kuona suala hilo likifanyika kwa mabavu kwa kuwalazimisha watu kuchanja.

Amesema kati ya mambo ambayo angependa ALAT kulishughulikiwa kwa kasi kubwa ni suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 ikiwemo utoaji elimu.

“Juzi na jana nilivyoingia nchini nimekuta hii agenda ya watu kupita nyumba kwa nyumba na mikoba ya sindano kuchoma watu.

“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome, asiyetaka usichome, lakini kubwa nalotaka kusema mtu hana mamlaka ya kukubali au kukataa kama anayo elimu.

“Kwani kama ana elimu yakutosha hawezi kukataa, lakini hana elimu unapita tu na mkoba wako unamwambia nikuchome nisikuchome, atakuambia usinichome,” amesema Rais.

Amewataka wahudumu wa afya kutoa elimu ya afya kwa wingi ili wananchi waone umuhimu wa kuchanja.

“Asipoona hilo hawezi kuona uchungu wa hili suala, nendeni kafanyeni kampeni kubwa watu wakubali kuchanja msiende kufanya kwa mabavu. Tupunguze vifo vinavyotokana na ugonjwa,” amesema.

Aidha amesema ndani ya nchi yetu kuna matatizo makubwa matatu na hili la uviko limejitokeza ni la nne.

Ametaja magonjwa mengine kuwa ni TB, HIV na malaria na kueleza kuwa yameshughulikiwa kwa kiasi kikubwa na kuagiza janga la Uviko-19 lishughulikiwe na watu wapate kinga.

Chanzo: Mwananchi
 
Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu was mkoa wa mbeya...
Updates: Mleta hoja alikuwa mnafiki na alilenga kuchonganisha Mh. Rais na sisi wana CCM. Ujumbe wangu ulidhani Mh. Rais amesisitiza ifanyike lazima, kumbe kaonya isiwe lazima. Namuunga mkono Mama na ninatengua kauli yangu ya maandishi na kuufuta huu ujumbe hapo chini. Mungu ambariki Mama SSH, ni yeye 2025!

Naomba Mod mpigeni BAN mleta maada alileta habari nusu yenye kutuchonganisha sisi wana CCM na rais wetu huku akijua rais katahadhalisha kuhusu chanjo na hakulazimisha.
 
Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya...
Kwa hiyo unataka kutuambia yeye anaponzwa kwa kupokea ushauri tu.
Au unataka kutuambia yeye hana maamuzi wala uwezo wa kuchambua mambo?

Tufike mahala tuache kumdharau Rais

Tuelewe kwamba yeye anakubaliana na anachokiamini

Rais Samia - Nimeona Afisa Afya Tunduru akipita nyumba kwa nyumba kuchanja, suala hili lisifanyike kwa mabavu kuwalazimisha watu kuchanja​

Haya maneno hajayasema, alichosema hakuna kumlazimisha mtu chanjo na hiyo ya nyumba kwa nyumba amehofia ufanisi wake. Alichosema ni watu wapewe elimu na sio kuwalazimisha.
 
Hii ni ticket ya Mama Samia kukosa kura 2025. Stay tuned wadau. Wataenda huko vijijini watawachanja na watu watakufa na hizo hasira hakuna maneno laini yatakayowafanya watu wamsamehe Mama Samia. Tena watamuita MUUAJI! Nadhani kuna kitu wanamficha washauri wake. Watu wengi wamepoteza ndugu zao kwa sababu ya chanjo hii ya majaribio.

Screenshot_20210927-152136.png
 
Ni lini ccm imeanza kutegemea kura za wananchi kushika dola?

Unajuya ni kwa nini mpaka Mungu amechukia ameamuwa kuwatwaa mashetani waliokuwa wamevikwa ngozi za binadamu huku wakijiita wazalendo?
 
Haya maneno hajayasema, alichosema hakuna kumlazimisha mtu chanjo na hiyo ya nyumba kwa nyumba amehofia ufanisi wake. Alichosema ni watu wapewe elimu na sio kuwalazimisha.
Oh kumbe. Dah mbona mleta maada kaleta nusunusu. Sema tatizo la viongozi wengi ni unafiki. Kila mtu anataka aoneshe chanjo zote zimetumika ili asifike kwa rais bila kujua kifo cha chanjo kitasababisha Mama akose kura.
 
Ni lini ccm imeanza kutegemea kura za wananchi kushika dola?

Unajuya ni kwa nini mpaka Mungu amechukia ameamuwa kuwatwaa mashetani waliokuwa wamevikwa ngozi za binadamu huku wakijiita wazalendo?
CCM siku zote tunashinda kwa halali. Mama for 2025, 2030!
 
Hii ni ticket ya Mama Samia kukosa kura 2025. Stay tuned wadau. Wataenda huko vijijini watawachanja na watu watakufa na hizo hasira hakuna maneno laini yatakayowafanya watu wamsamehe Mama Samia. Tena watamuita MUUAJI! Nadhani kuna kitu wanamficha washauri wake. Watu wengi wamepoteza ndugu zao kwa sababu ya chanjo hii ya majaribio.
Kwani unafikiri wao wanawaza kama unavyowaza wewe?
 
Ukweli usemwe na maamlaka za juu bwana yule alipotosha watu ili iwe rahisi waandamizi kutoa elimu covid na Chanjo.
 
Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya...
Chanjo ni hiyari acheni kupotosha watu wenye uwezo mdogo wa kuchanganuwa mambo.

Wakija kwako kama hutaki chanjo hulazimishwi, binafsi tayari nimechanja kwa hiyari kwa sababu najuwa kaburi halina mshirika, kila mtu atakwenda kaburini mwenyewe.

Kuna mtu hapa alikuwa akiwaaminisha wajinga wenzanke Corona hamna na tumeshamzika siku nyingi tu yeye na wapambe wake wengi tu wa karibu.

Akili za kuambiwa changanya na zako, hao mabeberu ndio wanawaletea ARV bure ili kuwaongezea siku za kuishi halafu hao hao waangaike kutengeneza chanjo ya kukudhuru?

Kuna viumbe akili zao zimekaa kama tundunla choo tu na ubongo umeliwa na fungus.
 
Oh kumbe. Dah mbona mleta maada kaleta nusunusu. Sema tatizo la viongozi wengi ni unafiki. Kila mtu anataka aoneshe chanjo zote zimetumika ili asifike kwa rais bila kujua kifo cha chanjo kitasababisha Mama akose kura.
Uzandiki tu ndo unatusumbua mkuu.

tafuta hotuba ya Mama, hili suala ameliongelea vizuri tena kwa kirefu. Viongozi wawekeze nguvu kuwaelimisha wananchi ili wachanje kwa hiari yao badala ya kuwalazimisha.

Tena akaongeza hata wakipita nyumba kwa nyumba basi wachanjwe wale tu waliokubali.
 
CCM siku zote tunashinda kwa halali. Mama for 2025, 2030!
Ukweli unaujuwa, ila mimi namuunga mkono Mama mia kwa mia, tulikuwa kwenye mikono ya washamba na makatili.

Wanamchukia mama ni kupungukiwa tu busara, tupime miaka 6 ya ukatili na miezi 6 ya huyu mama bora ipi?

Huyu mama anahitaji kupewa sapoti, kwanza ngoja tulisambaratishe kundi la mumiani wa Sukuma gang ndio turudi kwenye harakati.

Siko tayari kumuhujumu mama kuwapa nguvu mashetani wa Sukuma gang, ni heri haya majizi ya msoga huwa yanakula huku yanatuachia makombo kuliko hawa Sukuma gang ni makatili na wauwaji wakubwa.
 
Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya
Nani kasema anapita kulazimisha! anapita nyumba kwa nyumba kuelimisha na kufikisha chanjo kwa watu. Huyu anatakiwa kupongezwa kwa kuokoa maisha wa watu vijijini sio kumtungia vitu.

Kama mtu anachagua uwezekano wa kufa kwa huu ugojwa huwezi kulazimishwa maana hata ukiumwa malaria ni wewe wa kuamua kunywa dawa lakini haibadilishi ukweli kwamba chanjo ni muhimu.

Lakini kingiwa watu wengi hawajui kuna wanaokufa kwa corona hata hawajui hasa vijijini kwasababu wana magojwa mengine
 
Back
Top Bottom