Samia amesema anaunga mkono chanjo ya nyumba kwa nyumba inayopendekezwa na mkuu wa mkoa wa mbeya.
Swali hizo cost zinazotumika kulazimisha watu wachanjwe zinatoka wapi? Kwanini pesa zisielekezwe kwenye mambo mengine ya msingi.
Mama wanaomshauri wanamponza Sana.
---
Rais Samia Suluhu, amemzungumzia mhudumu wa afya anayepita nyumba kwa nyumba kuchanja chanjo ya Uviko-19, akionya kampeni hiyo isitumiwe vibaya katika kuwalazimisha watu kuchanja.
Jana katika mitandao ya jamii, kulisambaa habari na picha ikimuonyesha Ofisa wa Afya wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma akipita nyumba kwa nyumba kuwachanja chanjo ya Uviko 19 watu zaidi ya 160 kwa siku moja.
Akizungumzia leo Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalum wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma hilo, Rais Samia amesema asingependa kuona suala hilo likifanyika kwa mabavu kwa kuwalazimisha watu kuchanja.
Amesema kati ya mambo ambayo angependa ALAT kulishughulikiwa kwa kasi kubwa ni suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 ikiwemo utoaji elimu.
“Juzi na jana nilivyoingia nchini nimekuta hii agenda ya watu kupita nyumba kwa nyumba na mikoba ya sindano kuchoma watu.
“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome, asiyetaka usichome, lakini kubwa nalotaka kusema mtu hana mamlaka ya kukubali au kukataa kama anayo elimu.
“Kwani kama ana elimu yakutosha hawezi kukataa, lakini hana elimu unapita tu na mkoba wako unamwambia nikuchome nisikuchome, atakuambia usinichome,” amesema Rais.
Amewataka wahudumu wa afya kutoa elimu ya afya kwa wingi ili wananchi waone umuhimu wa kuchanja.
“Asipoona hilo hawezi kuona uchungu wa hili suala, nendeni kafanyeni kampeni kubwa watu wakubali kuchanja msiende kufanya kwa mabavu. Tupunguze vifo vinavyotokana na ugonjwa,” amesema.
Aidha amesema ndani ya nchi yetu kuna matatizo makubwa matatu na hili la uviko limejitokeza ni la nne.
Ametaja magonjwa mengine kuwa ni TB, HIV na malaria na kueleza kuwa yameshughulikiwa kwa kiasi kikubwa na kuagiza janga la Uviko-19 lishughulikiwe na watu wapate kinga.
Chanzo: Mwananchi
Mbona hakusema chochote kwa mku wa mkoa wa Mbeya juzi alipotangaza kuanza kupeleka chanjo ya UVIKO-19 nyumba kwa nyumba na kitanda kwa kitanda kwa madai eti wananchi wengi waliomba kupelekewa nyumbani kitu ambacho wananchi walengwa wanakikanusha?
Uongozi huu wa nchi utapata taabu sana kwa sababu ndani ya chama tawala kuna nguvu mbili zenye sura ya kimamlaka vikifany avitendo vinavyoashiria kuwepo upinzani hatarishi kwa usalama wa nchi kutokana mitazamo kukinzana bayana na wanaweza kuvurga amani ya nchi.
Utawala ambao ulishawahi kuwepo madarakani kuingia kwenye uongozi kwa sura mpya yenye malengo yaliyokuwepo ukiharamisha malengo yaliyowekwa na uongozi uliopigiwa kura kwa ushawishi kupitia ilani ya uchaguzi ya 2020-2025 halafu yanaletwa malengo ya 2010-2015 kutaipasua CCM kabla ya 2025 itayopelekea wananchi kuondoa imani zao kuziwekeza kutoka taasisi hiyo na haitawezekana tena kuwarubuni kubadilika.
Upinzani wa kweli utatokea ndani ya CCM na ndio utakaotoa dira sahihi kwa pwapinzani waliobanwa wamuunge mkono yupi ili kuiondoa kabisa CCM na isikukmbukwe popote katika historia ya Tanzania kwa kuwa wanadharau kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi kwa gharama nafuu ili wajikwamue na maisha magumu yanayopanda kila kukicha: mafuta juu, nauli juu, bidhaa juu, huduma dhaifu, kero zaongezeka, tozo zisizoakisi mrejesho wa huduma bora ina za staha kwa jamii, ushirikiano wa polisi na raia kudorora, wananchi kupoteza imani kwa watendaji wa serikali na umma, nishati juu, wafanyabiashara wadogo kuvurugwa kisaikolojia katika shughuli zao za kila siku za kujiingizia kipato kwa visingizio za kupanga miji yenye ramani zilizopitwa na wakati.
siasa zinatumika vibaya kuumiza raia; viongozi muwajali wananchi kwanza kabla ya malengo yenu ya kisiasa kwa kuwa hao ndio wapiga kura wenu, haki, utu, heshima na sheria zizingatiwe na kila mmoja kupitia wajibu wa kila upande.
Kuna makundi hasimu ambayo kwa namna moja au nyingine ndio wamo kwenye uongozi wa rais SSH ambayo ni ya wale wanaounga mkono falsafa za JKMrisho na lingine linaloendelea kuunga mkono falsafa za JPMagufuli hapa ndio kuna shida sio ya kitoto
Falsafa JKMrisho 'versus' Falsafa JPMagufuli refa wake anatakiwa awe mwenye mlengo wa kati kama mzazi kuvunja msigano wa makundi haya.
Ili mbegu iote ni sharti ianze kuoza ndipo ichipue; makundi hayo tajwa yote yamepanda mbegu zenye nguvu sana zilizobebwa na sera za (ubepari na ujamaa) ndani ya chombo kimoja ni lazima migogoro na ikiwezekana kuhujumiana, kuumizana, kudhoofishana na kumalizana vitatokea na kusababisha mgawanyiko ambao haujawahi kutokea tangu Tanzania izaliwe tarehe 26/4/1964 lakini tangu chama tawala kizaliwe tarehe 5/2/1977
Mamlaka iliyochukua utawala kwenye msimu wa namba shufwa (even number) na kutarajiwa kuondoka bila kurejea kwenye uongozi kwa mtindo wowote katika msimu wa namba witiri (odd number) bado unanguvu hadi 2025.
Mtindo wa uongozi uliorithi baada ya kifo cha mwenye msimu husika kujumuisha namba shufwa na namba witiri nguvu itabaki kwa mwenye msimu wa namba witiri mfano 1*2=3, 1*4=5,1*6=7, 1*8=9, 1*10=11 ambapo zao la mwisho linaonesha ni kigeugeu kwa nje linaonekana ni witiri lakini kiundani linatoa matokeo ya namba shufwa (even number) ambalo litajitokeza kwa nguvu ya kipekee mwaka 2035.
Namba shufwa ikilazimisha kuna madhara katika makundi hasimu ndani ngalawa ambapo Yona akitoswa majini chombo kitamegwa na kiboko.
*Someni alama za nyakati mtapona
*Visasi, chuki, inda, wivu, husuda na nongwa visiingizwe kwenye utendaji wa kazi na huduma kwa wananchi...........watumishi wa umma wamerejea kuwa na viburi na kuvunjia heshima wananchi wanowahudumia na ukiritimba wa taratibu umerudi kwa kasi ukichochea rushwa bila woga.....................nani ajitokeze kutoka wapi ili aingilie kati mtanziko huu?