Rais Samia Ondoa hiki kikokotoo kinawaumiza wastaafu

Rais Samia Ondoa hiki kikokotoo kinawaumiza wastaafu

Ninachojua.
Take home imeshushwa ili kuongeza pensheni ya kila mwezi.
Zamani take home ilikuwa kubwa halafu pensheni ya kila mwezi ilikuwa ndogo sana.
Kitu kilicho waumiza baadhi ya wafanyakazi ambao humaliza take home yao haraka na kuteseka muda mrefu.
Wengine wanaibiwa au kuisha kwenye ujenzi na kujikuta wanashindwa kukabiliana na maisha.

Sasa hivi take home imeshushwa lakini pensheni ya kila mwezi imeongezwa kwa kiasi kikubwa sana ambacho mstaafu anaweza kukidhi mahitaji yake vizuri baada ya kustaafu kazi.

Labda ningeshauri mfanyalazi apewe uhuru wa kuchagua.
Achukue take home kubwa na alipwe pensheni kidogo au kinyume chake.
Unaongea tu, unajua formula ya kikokotoo weww?? Hela iëiyoongezeka ni ndogo sana haifanani hata na uhalisia uliopo.. kikokotoo ni maumivu makubwa Kwa mfanyakazi
 
Aisee kuna mtu kanambia polisi aliyefanya kazi miaka 30 kalipwa milioni 17[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Na yuko nao wanamlinda hapo ameridhika kabisa hana wasi wasi[emoji38][emoji38]
 
Kusema kweli
Kuna kitu hakiko sawa kwenye mifumo ya hii nchi na sio fair
Kama ni haki basi na wabunge watumie mfumo huo
 
Hiki kikokotoo kiukweli kinawapa msongo wa mawazo wazee wetu,badala ya kuwafanya wafurahie uzee wao ,kinawataabisha na kufupisha maisha yao mapema mnooo.
 
Juzi hapa mbunge Heche kaeleza jinsi Wabunge wanavyopata lumpsum ya milioni 272 kwa kazi ya miaka Mitano. Wewe Rais hukatwi kodi katika mshahara wako na Ukistaafu unaendelea kupata 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani na bado unaenda kupata mabenefit kibao ikiwemo kujengewa nyumba na Pensheni.

Rais hebu Muogope Mungu. Wafikirie watu wa chini. Kikokowa cha 33% ni dhulma kubwa, iondoe mara moja.
Akiondoe pamoja na waliokiweka ni kama kiliwekwa na mizimu maana binadamu wenye akili timamu hawezi kufanya ujinga huo
 
Sasa kama mnakataa kustaafu mapema had mnakaata miaka yenu.
Sibora kikokotoo kiwaKandamize kizenji😲
 
Kuanza kupangia watu wazima namna ya kutumia pesa ni kujipa kazi nyingine, kwa nini wabunge nao wasipangiwe namna ya kutumia ile milioni 272, wawe wanawapa kidogo kidogo.......watu walipwe stahili zao matumizi mara zote ni swala binafsi.​
Umeongea point sana.
 
Mtu mzima hutakiwi kumpangia matumizi ya pesa yake.

Wewe mpe pesa yake, atajijua mbele kwa mbele
Kwanza kitendo cha kukata pesa ya mfanyakazi na kuipeleka NSSF ni cha lazima. Kama kingekuwa cha hiari wachache wangekubali kukatwa au hakuna ambaye angekubali.

Hivyo utambue mfanyakazi anapangiwa kila kitu, kuanzia Mashahala, Nyongeza, kukatwa NSSF, Bima Nk.

Hivyo basi hata swala la Mafao na Pensheni anapangiwa vile vile.
Idadi kubwa ya Wafanyalazi wanaolipwa take home unaisha mapema sana hadi wengine kuomba kuingizwa katika Mfuko wa TASAF ili Kujikimu.
Utakuta mtu ni Mzee sana, kulima hawezi anabaki kudhalilika tu mtaani huku kamaliza take home yake mapema tu. Na hii ndio sababu ya wastaafu wengi kufariki mapema.

Kwasasa Pensheni imeongezeka kwa kiasi cha kumudu maisha ya mstaafu ya kawaida.
Na baadhi ya wafanyakazi wamepongeza mfumo wa sasa kwakuwa pensheni inalipwa ya thamani zaidi ya kiwango cha pesa kinachobaki baada ya kupewa cha awali.

Ndio maana nimesema kungekuwa na option. Kama mfanyakazi ana uhakika wa kutumia vizuri take home yake basi apewe hata yote wamalizane kabisa.
Kama mfanyakazi anapenda pensheni nzuri basi aendelee na mfumo wa sasa.

Mfanyakazi asipangiwe kama mnavyosema, na sio kweli wafanyakazi wote wanapenda mfumo wa zamani.
 
Kikotoo hakina faida yoyote kwa mfanyakazi aliyekatwa pesa zikatumika na mifuko jamii kufanyia biashara lakini lakini yeye anaambulia 1% riba kila mwisho wa mwaka kwa kiasi alichokiweka na inafanyiwa kazi riba hiyo kwa si zaidi ya miaka 10 ya utumishi hata kama kafanya zaidi ya hiyo.

Kikokotoo kiondolewe na mfanyakazi anapoacha kazi yake apewe pesa zake zote ili afanyie biashara au mradi atakaouanzisha mwenyewe sio kupangiwa haki yake namna atakavyoitumia.
Hawatakaa wafanye huu uamuzi hawa mabaradhuli
 
Mfanyakazi wa Serikali kufanya kazi miaka zaidi ya 25 bila kujenga nyumba ya kuishi
ni poor planning na kushindwa uwajibikaji.
Nyumba sio lazima iwe ya vyumba kumi.
 
Ninachojua.
Take home imeshushwa ili kuongeza pensheni ya kila mwezi.
Zamani take home ilikuwa kubwa halafu pensheni ya kila mwezi ilikuwa ndogo sana.
Kitu kilicho waumiza baadhi ya wafanyakazi ambao humaliza take home yao haraka na kuteseka muda mrefu.
Wengine wanaibiwa au kuisha kwenye ujenzi na kujikuta wanashindwa kukabiliana na maisha.

Sasa hivi take home imeshushwa lakini pensheni ya kila mwezi imeongezwa kwa kiasi kikubwa sana ambacho mstaafu anaweza kukidhi mahitaji yake vizuri baada ya kustaafu kazi.

Labda ningeshauri mfanyakazi apewe uhuru wa kuchagua.
Achukue take home kubwa na alipwe pensheni kidogo au kinyume chake.
Ulichoongea ni sahihi kabisa ila tatizo ni pale utakapo pewa take home kidogo na pensheni ya Kila mwezi isiweze kufanya jambo lolote zaidi ya kula na kuvaa. Mfanyajazi hawezi kufanya project km kujenga nyumba standard kwa kutegemea pesa ya Kila mwezi. Hilo liko wazi.

Ndio maana ukifuatilia wafanyakazi wote waadilifu wa ngazi za kawaida sio rahisi hata kununua gari kwa kutunza mshahara wa Kila mwezi. Lazina wakakope Bank ili wapate pesa ya mkupuo kununua gari. Hivyo hivyo hata ktk kujenga nyumba nzuri ya kisasa lazima atakopa mara nyingi hadi kumaliza ujenzi.

Km kupewa pesa nyingi Kila mwezi ni dawa basi wafanyakazi wengi wasingekuwa wanalilia mishahara. Kuna wafanyakazi wa umma wanavuta hadi 3-6 m lakini hao hao bado wana mikopo Bank. Mfano Kuna Walimu wanavuta take home 1,500,000 lakini hao hao wana madeni kibao. Askari Wana hadi resheni nje ya mshahara lakini unakuta wana madeni Bank na taasisi zingine.

Asikwambie mtu, pesa ya mkupuo ina manufaa sana maana unaweza kufanya jambo linaloeleweka kwa wakati mmoja, lakini ukitegemea za Kila mwisho wa mwezi utajuta hata ukiwa unapokea 2m.
 
Inategeme
Mfanyakazi wa Serikali kufanya kazi miaka zaidi ya 25 bila kujenga nyumba ya kuishi
ni poor planning na kushindwa uwajibikaji.
Nyumba sio lazima iwe ya vyumba kumi.
Inategemea anafanya kazi na ana majukumu gani ya kifamilia. Hivi unajua kima Cha chini Cha mfanyajazi wa umma ni sh. Ngapi. We acha tu. Wafanyakazi kazi wanayo.
 
Mstaafu apewe mafao yake walau isipungue asilimia 70 ya akiba yake yote. Hiyo inayobaki asilimia 30 ndio apewe kidogo kidogo. Hiyo habari ya kuanza kumpangia mtu matumizi ya pesa zake haifai kabisa na sio kitu kizuri zaidi ya kucheza na maisha ya watu. Kama kweli kumpangia mtu jinsi ya kutumia ni jambo zuri basi na wabunge kuanzia sasa nao wapewe mafao yao asilimia 33 kama wafanyakazi wanavyopewa halafu zinazobaki asilimia 67 nao wao wapewe kidogo kidogo.
 
Mheshimiwa Rais.

Nakuandikia waraka maalum juu ya hali ya mfanyakazi, hususan anayestaafu.

Nataka nikueleze kuwa, hiki kikotowo ulichokiweka hakina masilahi kwa mfanyakazi anayestaafu. Kiufupi ni dhuluma ya wazi.

Hali ya maisha imekuwa ngumu, gharama za maisha zinazidi kupanda. Kiufupi , hii 33% lumpsum unayotoa kupitia kikotowo, haitoshi, haikidhi, na ni dhulma kubwa mno kwa mfanyakazi.

Ndugu Rais, Jasho la mtu halipaswi kupangiwa masharti magumu. Haiwezekani Mfanyakazi afanye kazi miaka 30 au 35 kisha aje akutane na vijisent vya milioni 50 kama mafao ya kustaafu. Hivi ni vihela vidogo sana na siku hizi havitoshi hata kununua kiwanja na hapohapo kujenga nyumba ya vyumba vitatu.

Ndugu Rais, Hicho chama unachokiongoza kina alama ya jembe na nyundo. Nyundo ikiwakilisha wafanyakazi. Haiwezekani serikali unayoiongoza ikawa ni ya kuwagandamiza wafanyakazi.

Juzi hapa mbunge Heche kaeleza jinsi Wabunge wanavyopata lumpsum ya milioni 272 kwa kazi ya miaka Mitano. Wewe Rais hukatwi kodi katika mshahara wako na Ukistaafu unaendelea kupata 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani na bado unaenda kupata mabenefit kibao ikiwemo kujengewa nyumba na Pensheni.

Rais hebu Muogope Mungu. Wafikirie watu wa chini. Kikokowa cha 33% ni dhulma kubwa, iondoe mara moja.

Wako katika ujenzi wa Taifa

Missile of the Nation
Kama mstaafu anategemea kununua kiwanja na kujenga nyumba kwa pesa za mafao ya kustaafu basi hapo amepotea njia, hata alipwe ngapi bado kuangamia kutakuwa pale pale.

Pesa ya mafao ya kustaafu ni 'kachumbari' ya kuchangamshia maisha uliyoyajenga kipindi ukiwa anafanya kazi.
 
Back
Top Bottom