Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nchi hii inashindwa kufika mahali ilipotakiwa kufika kwa sababu ya kuongozwa na watu wasiojitambua, wasiojua wajibu wao wala mipaka ya mamlaka yao.
Kuna habari zinazunguka mitandaoni kuwa eti DC wa Nzega ameamuru mkuu wa Chuo Cha Madini Nzega awekwe ndani kwa sababu alishindwa kumjibu mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea chuo hicho.
Kwanza, hawa viongozi, wote wawili ni dhahiri inaonekana hawana uelewa wa chochote kwenye mifumo ya utawala.
Chuo cha madini Nzega kipo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kama kuna matatizo kwenye branch hiyo ya UDSM, walitakiwa kuwasilidha malalamiko yao kwa mkuu wa Chuo Kikuu, UDSM, ambaye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete au Vice Chancelor wake.
Bila shaka hawa viongozi ni wale malimbukeni wa madaraka. Kwa vile tu sheria inatamka kuwa wanaweza kutoa amri ya kumweka mtu ndani kwa muda usiozidi masaa 48, kwa ujinga wa kutojua mantiki ya sheria hiyo, wanaichukulia kumweka mtu ndani ni kama adhabu, wakati lengo la sheria hiyo lilikuwa kwa kuzingatia mazingira ya nyakati na mahali. Mathalani mtu anaonekana akiwa huru anaweza kuendelea kudhuru au kudhuriwa, na vyombo vya kisheria vya udhibiti havipo eneo la karibu, basi mkuu wa mkoa au wilaya, alipewa mamlaka hayo ili kipindi hicho akiwa ndani, kitumike kuwasiliana na mamlaka husika. Unajiuliza, huyo mkuu wa hiyo branch ya UDSM alikuwa anamdhuru nani hadi awekwe ndani, jibu linakuwa moja tu, kuwa huyo DC inaonekana ni empty kabisa kichwani kwa masuala ya utawala na sheria.
Rais anapoteua watu kwenye nafasi fulani, hasa kwa nchi iliyojaa machawa, rushwa na vyombo dhaifu vya vetting, inakuwa ni kubahatisha, lakini inapodhihirika, kama ilivyo kwa hawa watu, kuwa wateule ni watu duni kiutendaji, inatakiwa kuwafukuza mara moja kabla hawajaleta madhara makubwa zaidi.